Kujenga daraja kuunganisha Dar es Salaam na Unguja ni upotevu wa fedha za maskini. Tuachane na mpango huu!

Kujenga daraja kuunganisha Dar es Salaam na Unguja ni upotevu wa fedha za maskini. Tuachane na mpango huu!

Serikali ya Tanzania inafikiria kuiunga Bara na Zenji kwa daraja?
Daraja la Kigongo-Busisi lina faida gani mpaka ligharimu Tsh 716 Bilioni? Bilioni 716 ingejenga kilomita 700 barabara za lami sasa badala yake imejenga Km 3.2. Ni kichaa tu anaweza kufanya maamuzi km haya. Hii gharama hata miaka 100 ijayo haiwezi kurudi, ni ubinafsi tu wa Mwendazake. Ilitosha kuimarisha vivuko pale. Bora la Dar-Zanzibar maana litajengwa na mwekezaji na litakuwa na tozo, kidizain itakuwa ya kitalii. Na siyo km 85 km mzushi fulani alivyoweka ni km 40.
 
Kujenga daraja dar znz ni sawa na kujenga nyumba ukweni, je ukiachana na mke itakuaje?
nenda kachukue akili yako kule ulikoazima. Kuna muungano kati ya Msumbiji na Tanzania? Hujasikia kuna daraja la umoja kuunganisha nchi hizi mbili? Hata muungano ungevunjia ingawa siyo rahisi mnavyofikiri nyie vitoto Zanzibar na Tanganyika zitabaki kuwa nchi jirani.
 
Kwann comments nyingi mnaweza kuwa muungano unaweza kufika mwisho? Embu acheni uchawi
 
Hwajamaliza kujenga Dodoma wamehamia kweny daraja 😂😂😂hilo daraja halipo na sio kitoto ...Azam wana boti za kifahari waache tu watu wapande boti huku bara kweny majiji miundombinu ni mibovu eti ukajenge daraja huko zenji.
 
Hujasema popote kuhusu faida za daraja husika likikamilika. Kwamba utaenda kuuza mbaazi unguja
Yaani uende kuuza mbaazi kwenye idadi ya watu milion2 uache Tanganyika yenye watu 60milioni?Kama kweli wataanza huu mradi watz lazima tulipinge kwa nguvu zote.haiwezekani kukimbilia mradi mfu kama ule wakati kunachangamoto nying tu za kutatua
 
Population na uchumi wa Zanzibar ni kidogo mno kwa daraja kama hili itakuwa hasara!
 
Kama kweli hiyo fedha ipo napendekeza tujenge daraja kukatisha lake Tanganyika kwenda DRC mdau wetu mkubwa wa bandali yetu
Tuifungue ile boda kuepuka mausumbufu kibao ya Zambia. Tija ipo kubwa sana kwa reli yetu ya kati na barabara ya Dar Kigoma
HakyaMungu nawambia tutavuna sana
Niamini mimi utanishukuru badae
Nakupenda sana Tanzania
Mungu ibariki Tanzania
Mkuu, BRT tu zinawashinda, ndo wajenge daraja Dar - Znz? Kwaajili ya nini kwanza?

Watu wenyewe wako 1,000,000 wenye bajet isiyozidi tsh 500bn kiuhalisia kwa mwaka, sawa na wizara kadhaa.

Kuna kipindi ilisema, serikali ya Japan, ilisema hata wakiwajengea daraja hilo kwa mkopo, TZ itabidi itumie pato lake lote la taifa kulipa deni kwa miaka 50.

  • Wanatumia umeme bure, wanabebwa kila idara.
  • Wanakopa kwa gharama za waTanganyika.
  • Wanamiliki ardhi na mali za waTanganyika ILHALI kwao ni marufuku kwa wabara kuwa hata mjumbe wa shina.

Kisha muingie gharama kwaajili ya wao kuvuka tu?

Naona tumeamua kufuga MCHWA na KUPE.
 
wasijisumbue kujenga hilo daraja maana huo muungano wenyewe hauna tija kwa waTanganyika. Soon utapoea mazima tujitegemee kama waTanganyika. Wachukue maoni ya watu wote Bara waone kama wanaupenda huo ujinga.
 
... kwa uchumi upi ulioko Zanzibar actually Unguja wa kujenga daraja la gharama to that extent? Kununua urojo au? Kupeleka mbaazi au?

Mkisikia China bara inaunganishwa kwa daraja na Hong Kong au Macau hivyo visiwa ni economic giants; uchumi wa Afrika urudi darasani; hawajengi tu fahari ya macho!

Member mmoja katoa wazo kuunganisha Tanganyika na DRC at least that makes sense!
 
wasijisumbue kujenga hilo daraja maana huo muungano wenyewe hauna tija kwa waTanganyika. Soon utapoea mazima tujitegemee kama waTanganyika. Wachukue maoni ya watu wote Bara waone kama wanaupenda huo ujinga.
... na financier ni Tanganyika! Kama wanalihitaji sana ijenge Zanzibar.
 
Dar-Unguja ni takriban kilometer 85. Tuna madaraja muhimu sana ya kuunganisha mkoa kwa mkoa au wilaya kwa wilaya yenye urefu wa mita 20 au 50 tu na tumeshindwa kuyajenga leo hii tunafikiria kujenga daraja la km 85?!

Kwanini tusipanue bandari zetu na kuimarisha usafiri wa majini kwa kuweka boat kubwa na nyingi ili gharama zipungue?

Daraja la Kigogo Busisi pekee lenye urefu wa kilometer 3.2 tu kimetigharimu billioni 700 je km 85 tena juu ya bahari ni trilioni ngapi?! Ni zaidi ya trillion 10! Hii ni gharama ya kutosha kujenga SGR kutoka Dar hadi Arusha au Kigoma! Tuachane na kujenga madaraja kama mapambo, tuache kabisa hailipi!
I think you're too radical and aggressive as well..

Wazo la kujenga daraja baharini kutoka Dar - Zanzibar (Unguja) honestly, sio baya na ofcoz kama uwezo wa kifedha wa kulijenga upo, basi ni vyema lijengwe haraka na mara moja..

Ishu ya kuangalia hapa ni hali yetu kifedha (kiuchumi) vs vipaumbele (priorities) katika kufanya development projects zetu kama nchi..

Hata hivyo TZS 10trn si fedha nyingi iwapo private sector itashirikishwa kikamilifu. Ni ngumu sana kwa serikali kutekeleza mradi mkubwa kama huu peke yake vinginevyo isimamishe miradi mingine yote na pia inaweza kuathiri shughuli na huduma zingine katika nchi iwapo hakutakutakuwa na umakini ktk kuachilia fedha kwenda huko pekee...
 
Zinatafutwa hela za uchaguzi kibaya ni kwamba kila mtu anavimbisha mifuko mchuano tutauona usishangae msoga akihama upande
 
Yaani uende kuuza mbaazi kwenye idadi ya watu milion2 uache Tanganyika yenye watu 60milioni?Kama kweli wataanza huu mradi watz lazima tulipinge kwa nguvu zote.haiwezekani kukimbilia mradi mfu kama ule wakati kunachangamoto nying tu za kutatua
Mlishawahi kupinga kitu gani???
 
Naamini haya ni mawazo ya mtu ambaye hajapevuka!
Ulitakiwa utaje faida na hasara ya kuwa na daraja kama hilo.
Wewe ndo hujapevuka kiakili. Mleta mada kazungumzia hasara,ina maana kwake daraja halitakuwa na faida.
 
I think you're too radical and aggressive as well..

Wazo la kujenga daraja baharini kutoka Dar - Zanzibar (Unguja) honestly, sio baya na ofcoz kama uwezo wa kifedha wa kulijenga upo, basi ni vyema lijengwe haraka na mara moja..

Ishu ya kuangalia hapa ni hali yetu kifedha (kiuchumi) vs vipaumbele (priorities) katika kufanya development projects zetu kama nchi..

Hata hivyo TZS 10trn si fedha nyingi iwapo private sector itashirikishwa kikamilifu. Ni ngumu sana kwa serikali kutekeleza mradi mkubwa kama huu peke yake vinginevyo isimamishe miradi mingine yote na pia inaweza kuathiri shughuli na huduma zingine katika nchi iwapo hakutakutakuwa na umakini ktk kuachilia fedha kwenda huko pekee...
Daraja la trillion 10 kuunganisha waunguja million 1 na watanzania 60m?

Unajua trillion 10 tungefanya nini nayo katika nchi ambayo bado watoto wetu wanakaa chini shuleni, hakuna huduma mzuri za afya, watu hawana uhakika na chakula, hakuna maji safi, umeme, etc?!

Kwanini watanzania mnapenda kuchulia mambo yote poa tu?
 
Back
Top Bottom