saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,683
- 7,222
wazo la hovyo kabisa, daraja la umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji kuna muungano kati ya nchi hizi mbili?Ya Mungu mengi, ikitoke siku ndoa ya Tanganyika na Zanzibar ikafa daraja litakuwa na manufaa gani zaidi?
Daraja la Kigongo-Busisi lina faida gani mpaka ligharimu Tsh 716 Bilioni? Bilioni 716 ingejenga kilomita 700 barabara za lami sasa badala yake imejenga Km 3.2. Ni kichaa tu anaweza kufanya maamuzi km haya. Hii gharama hata miaka 100 ijayo haiwezi kurudi, ni ubinafsi tu wa Mwendazake. Ilitosha kuimarisha vivuko pale. Bora la Dar-Zanzibar maana litajengwa na mwekezaji na litakuwa na tozo, kidizain itakuwa ya kitalii. Na siyo km 85 km mzushi fulani alivyoweka ni km 40.Serikali ya Tanzania inafikiria kuiunga Bara na Zenji kwa daraja?
nenda kachukue akili yako kule ulikoazima. Kuna muungano kati ya Msumbiji na Tanzania? Hujasikia kuna daraja la umoja kuunganisha nchi hizi mbili? Hata muungano ungevunjia ingawa siyo rahisi mnavyofikiri nyie vitoto Zanzibar na Tanganyika zitabaki kuwa nchi jirani.Kujenga daraja dar znz ni sawa na kujenga nyumba ukweni, je ukiachana na mke itakuaje?
Yaani uende kuuza mbaazi kwenye idadi ya watu milion2 uache Tanganyika yenye watu 60milioni?Kama kweli wataanza huu mradi watz lazima tulipinge kwa nguvu zote.haiwezekani kukimbilia mradi mfu kama ule wakati kunachangamoto nying tu za kutatuaHujasema popote kuhusu faida za daraja husika likikamilika. Kwamba utaenda kuuza mbaazi unguja
Wazanzibari wote kuanzia umri wa miaka 18, watozwe tozo kila mwezi ili kufanikisha ujenzi wa hilo daraja. Maana Watanganyika hatuna shida nalo.
Mkuu, BRT tu zinawashinda, ndo wajenge daraja Dar - Znz? Kwaajili ya nini kwanza?Kama kweli hiyo fedha ipo napendekeza tujenge daraja kukatisha lake Tanganyika kwenda DRC mdau wetu mkubwa wa bandali yetu
Tuifungue ile boda kuepuka mausumbufu kibao ya Zambia. Tija ipo kubwa sana kwa reli yetu ya kati na barabara ya Dar Kigoma
HakyaMungu nawambia tutavuna sana
Niamini mimi utanishukuru badae
Nakupenda sana Tanzania
Mungu ibariki Tanzania
... na financier ni Tanganyika! Kama wanalihitaji sana ijenge Zanzibar.wasijisumbue kujenga hilo daraja maana huo muungano wenyewe hauna tija kwa waTanganyika. Soon utapoea mazima tujitegemee kama waTanganyika. Wachukue maoni ya watu wote Bara waone kama wanaupenda huo ujinga.
... na financier ni Tanganyika! Kama wanalihitaji sana ijenge Zanzibar.
I think you're too radical and aggressive as well..Dar-Unguja ni takriban kilometer 85. Tuna madaraja muhimu sana ya kuunganisha mkoa kwa mkoa au wilaya kwa wilaya yenye urefu wa mita 20 au 50 tu na tumeshindwa kuyajenga leo hii tunafikiria kujenga daraja la km 85?!
Kwanini tusipanue bandari zetu na kuimarisha usafiri wa majini kwa kuweka boat kubwa na nyingi ili gharama zipungue?
Daraja la Kigogo Busisi pekee lenye urefu wa kilometer 3.2 tu kimetigharimu billioni 700 je km 85 tena juu ya bahari ni trilioni ngapi?! Ni zaidi ya trillion 10! Hii ni gharama ya kutosha kujenga SGR kutoka Dar hadi Arusha au Kigoma! Tuachane na kujenga madaraja kama mapambo, tuache kabisa hailipi!
Mlishawahi kupinga kitu gani???Yaani uende kuuza mbaazi kwenye idadi ya watu milion2 uache Tanganyika yenye watu 60milioni?Kama kweli wataanza huu mradi watz lazima tulipinge kwa nguvu zote.haiwezekani kukimbilia mradi mfu kama ule wakati kunachangamoto nying tu za kutatua
Wewe ndo hujapevuka kiakili. Mleta mada kazungumzia hasara,ina maana kwake daraja halitakuwa na faida.Naamini haya ni mawazo ya mtu ambaye hajapevuka!
Ulitakiwa utaje faida na hasara ya kuwa na daraja kama hilo.
Daraja la trillion 10 kuunganisha waunguja million 1 na watanzania 60m?I think you're too radical and aggressive as well..
Wazo la kujenga daraja baharini kutoka Dar - Zanzibar (Unguja) honestly, sio baya na ofcoz kama uwezo wa kifedha wa kulijenga upo, basi ni vyema lijengwe haraka na mara moja..
Ishu ya kuangalia hapa ni hali yetu kifedha (kiuchumi) vs vipaumbele (priorities) katika kufanya development projects zetu kama nchi..
Hata hivyo TZS 10trn si fedha nyingi iwapo private sector itashirikishwa kikamilifu. Ni ngumu sana kwa serikali kutekeleza mradi mkubwa kama huu peke yake vinginevyo isimamishe miradi mingine yote na pia inaweza kuathiri shughuli na huduma zingine katika nchi iwapo hakutakutakuwa na umakini ktk kuachilia fedha kwenda huko pekee...