Kujenga daraja kuunganisha Dar es Salaam na Unguja ni upotevu wa fedha za maskini. Tuachane na mpango huu!

Hii ni serikali kuwatoa watu kwenye reli tu kujadili mambo yasiyo na kichwa wala miguu; kufunikia mijadala ya hoja za CAG.

Gharama za kujenga reli kilometer kwa dollar 1.2 million ni vilio kila kukicha, bwawa la umeme limechelewa kwa sababu ya malipo ya kudunduliza.

Ndio tuanze kujadili ujenzi wa daraja ambalo ujenzi wake kilometer moja ni $51m hiyo ni kwa gharama ya 2011 kwenye daraja lao refu walilojenga China na halipiti baharini bali kwenye mto mtu..

Letu linakatiza baharini kuna ocean weather elements kwa ivyo mambo luluki yanatakiwa yaongezwe ili hilo daraja liwe stable and durable kuhimili hali ya hewa ya baharini.

Sasa Si ajabu gharama ya kilometer moja ikafika $70m, na umbali wa kutoka Paje Zanzibar; mpaka Dar ni kama 90 kilometer.

Hiyo hela tunayo au serikali inataka kuwatoa watu kwenye reli tu kwenye hoja za CAG.
 
Tume ya mipango in semaje
 
Kama la mwekezaji sawa aweke hilo tozo na tusiweke rehani mali zetu.
 
Hizo fedha watimie kujenga barabara za kuanganisha wilaya zote na makao makuu ya mikoa
 
We akili huna
 
Yule jamaa bora alikufa, angekuwepo leo Chato ingekuwa na 5* hotel
 
Mbona mnateseka kana kwamba hizo pesa mtagawana?
 
Dar to unguja siyo km 85, ni 40! Ila naunga mkono hoja, huu ni uwekezaji usio na tija, it's luxurious expenditure na Haina faida kwa taifa
 
Unataka wazifanyie nn sasa
Binadamu hatuna shukran
Unajenga daraja ambalo halitakuwa na mchango wowote kiuchumi kwa mabilioni ya fedha halafu huku unachangisha walimu Tsh 2000 ya mwenge hiyo ni akili au bangi.?

Ni faida kwa serikali kuacha kujenga hilo daraja kuliko kulijenga
 
Hizo ni ndoto ya mchana,labda kizazi kijacho
 
Kweli kabisa, nilikuwa na yule jamaa wa NSSF naye pia alitaka kufanya hii kitu kwa kutumia company inayo itwa Shanhai Construction hii company ni ya serikali ya China, wale jamaa akasema haita wezekana sababu itatumia pesa nyingi sana na Tanzania [emoji1241] haitakuwa na uwezo ya kulipa!
Ili iweze kurudisha pesa yao mtanzania itabidi alipe $100 kuvuka hilo daraja na Tanzania [emoji1241] hatujafika kiwango hicho kumtoza mwana nchi!
Wakasema ni impossible!
That was like seven years ago!
Mwenye Enzi Mungu mweza wa yote nakusihi eeh Mola tuepushe na majanga kama haya!
 

Unaona ehh
Ni Mola wetu tu anaweza kutusaidia wana nchi wa Tanzania [emoji1241] walahi!
 
Kinacho takiwa sahiv ni kuvunja muungano tu maana jamaa wananufaika na sisi kuliko sisi tunavyonufaika nao
 
Wakijenga chini ya serikali ya huyu mama niite umbwa. Hizo ni porojo tu kama za babu sani.
 
40 miles or km?
Dar to unguja siyo km 85, ni 40! Ila naunga mkono hoja, huu ni uwekezaji usio na tija, it's luxurious expenditure na Haina faida kwa taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…