Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Kama unajua ni hulka ya binadamu...itafika wapi ndo ujue upo stable?
Unapopata ela na wazo la ujenzi wewe fanya
Ukiweza kujenga nyumba ya kuishi bila mkopo huku ukiendelea kuwa na kipato cha kukutosheleza mahitaji yako muhimu na ukiwa na akiba.
 
Mimi nimechangua kujenga kwanza kabla ya kuanzisha biasha au kimiliki gari
Nkimaliza kama nipo hai Basi nitafungua biashara
Nyumba natumia kama ngazi tu ya kuyafikia malengo mengine hata nikianguka bas niwe na sehem ya kuishi.
 
Mimi nimechangua kujenga kwanza kabla ya kuanzisha biasha au kimiliki gari
Nkimaliza kama nipo hai Basi nitafungua biashara
Nyumba naktumia kama ngazi tu ya kuyafikia malengo mengine hata nikianguka bas niwe na sehem ya kuishi.
Biashara utakayoanzisha baada ya kujenge nyumba mara nyingi ni ya kuganga njaa tu si kwa ajili ya mafanikio makubwa.
 
Umeongea vizuri sana, kuna dhana potofu sana kwamba kila mtu anaweza biashara, wakati si kweli kabisa. Miaka ya nyuma niliwahi kuwa na mchepuko nikaufungulia biashara, tena kwa kukopa pesa mahala, lipa kodi ya fremu miezi mitatu, nunua mzigo wote, leseni etc... Nikapotea kikazi kama miezi mitatu hivi, aisee kurudi fremu nyeupe!! Nikakuta sanduku zima kajaza nguo na vikoro Koro vipya. Nikafuatilia kwa jirani zake story walizonipa nikachoka, nikamwambia funga fremu hiyo. Baada ya mwezi binamu yangu from village alipoona pamefungwa akaniomba na yeye ajaribu hiyo hiyo biashara kwenye hiyo fremu. Basi nikampa nusu mtaji na kulipa kodi mwezi mmoja, aisee alikomaa after three months fremu imejaa kupita ilivyokuwa mwanzo, na aliendelea mpaka akawa na maduka mawili.
 
Bro tukutane ukiwa na 50 years ukiwa na hela nyingi alafu huna nyumba
Hata nikifika 50 sina hela siwezi kuogopa nianze kujibana kisa nijenge. Tofauti yangu na wewe ni moja, wewe kila senti ukipata unawaza ununue tofali ujenge kozi kadhaa mimi nawaza hela hio nitaizalisha vipi zaidi na zaidi.
 
Biashara kabla ya ujenzi unatakiwa uwe makini sana, biashara ina sayansi yake. Nashauri jenga kwanza huku unafikiria hiyo sayansi ya biashara. Kumbuka katika mahitaji makuu ya binadamu, nyumba ipo ila biashara haipo, tafakari.
Chakula [emoji3591]Malazi/nyumba [emoji3591] Mavazi
 
Ukiwa unafanya biashara unaishi kwenye nyumba ya nani?

Au huwa unakaa pangoni kama Gaidi
 
Hata nikifika 50 sina hela siwezi kuogopa nianze kujibana kisa nijenge. Tofauti yangu na wewe ni moja, wewe kila senti ukipata unawaza ununue tofali ujenge kozi kadhaa mimi nawaza hela hio nitaizalisha vipi zaidi na zaidi.
Sasa hivi unaishi kwenye nyumba ya nani?
 
Biashara sio kila mtu anaweza kufanya
 
Kuna swala pia la kutambua nyakati majira na fursa. Kwa mfano, wakati mimi naanza kupata pata pesa angalau, viwanja vilikuwa vinapatikana kuanzia mbezi makonde , mbezi jogoo kuelekea tegeta , kwa bei chini ya tzs 3,000,000.
Wakati huo mimi niliamini katka kufanya biashara na kupata pesa ambayo kwayo jambo la 'ununuzi wa kiwanja na ujenzi wa nyumba lingerahisika. Kwa bahati mbaya, kabla malengo hayajatimia biashara zikayumba na mpaka leo zina survive, na 'sijaweza 'kupata kiwanja maeneo hayo, maana sasa bei haishikiki.
Kwa hiyo maamuzi mengine ni vizuri yakafanyika katika mu da muafaka ili kuepusha majuto ya baa dae , maana mambo na /maisha kwa ujumla yanaweza kubadilika usivyotarajia..
 
Aisee inabd ujenge kwanza ,mambo ya biashara yatafuata ,labda kama huna familia ,muhimu ni kujenga nyumba unayoimudu kwanza ,watoto na mke wapate pa kukaa

Kwanza kama umeoa na uko na mwanamke anayejielewa hawezi kushauri ukope hela ufanyage tu biashara na huna hata kiwanja mmepanga tu.
 
Biashara sio kila mtu anaweza kufanya
Wape/ wakopeshe/ingia ubia na wanaoweza kufanya biashara waongeze mtaji na faida kubwa ugaiwe na wewe usiyeweza biashara.
 
Kanunue hisa,ingia ubia na wanaojua biashara au jenga fremu za kupangisha.
 
Na mimi nashangaa, wakati una save pesa ambayo ungelipa kodi.....
Wafanyakazi wengi wanajenga nyumba za kuishi kwa mikopo yenye riba kubwa. Hakuna pesa wanayo save kwa sababu nyumba inakuwa haizalishi huku wakirejesha mkopo wenye riba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…