Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Bro tukutane ukiwa na 50 years ukiwa na hela nyingi alafu huna nyumba
Shida iko wapi mzee?
Wahindi wanazeeka wamepanga Kariakoo na Upanga lakini akitaka kukuhamisha kwenye nyumba yako anakupa fedha na anakuhamisha anamiliki nyumba yako uliyojenga kwa miaka 7 kwa siku moja

Tafuta pesa mkuu achana na ngonjera za kuitwa mwenye nyumba wakati unapumulia mashine kwa umasikini.
 
Kama unaweza kupanga nyumba ya kutosha familia na ikasitirika ni bora kuanza na hiashara.
Kama unauwezo wa kupanga chumba kimoja au viwili na una fakimila ya watu 6 ni bora kujibana kujenga maana utaainika sana.

Shida unakuta umepanga chumba na seble familia kubwa mpaka kufikia watoto kulala seblem kwenye makochi...
 
Nyumba nzuri unayoweza kaa na familia yenye watoto 3 ni ngapi kwa mwezi?
The same time unadaiwa ada 2.5m kwa mwaka
Bado nauli
Chakula etc
Hapo ndo ujibane kujenga
 
Hii mentality ya kiumaskini sijui imetoka wapi..watu ni waoga mnoo.katika hii thread watu walio changia positive hawazid wanne.wengi wanaogopa biashara!
 
Sina muda wa kujiuliza kwa mtu anayelialia, vifaa vikipanda tafuta hela zaidi maisha hayasimami…. ujenge usijenge kulialia haikusaidii.
Mtu amabe hushindwa kifikiria kabla ya kutenda ni MBUMBUMBUU

Fikiri kabla ya kutenda kid
 
Tengenezeni Future ya watoto wenu wakuu,acheni kukimbilia kuzika pesa..acheni ubinafsi..matokeo yake watoto wanakuja kuanza upya as if hakuwa na wazazi..
Kabisa, ilo Ni tatizo kwa familia nyingi Sana uku mtaani
 
Off course,
Pamoja na bei za vifaa kuwa juu bado tunajenga lkn pia inawezekana sana bei za vifaa ikapunguzwa ikawa na unafuu kiasi flan watu wakamudu ujenzi ulio bora
 
Unajenga taratibu ndani ya miaka kadhaa nyumba ya 30mln inaisha .

Watumishi Wana salary na Wana uhakika wa mwisho wa mwezi.
Kwanini usifanye biashara kidogo kodogo ndani ya hiyo miaka kadhaa ukapata fedha za uhakika wa kujenga nyumba ya ndoto yako kwa faida na bila stress na bado biashara ikiendelea?
 
Nyumba inakuaje liability ukiishi wewe?
Sababu umetoa pesa kuijenga and still utakua unato pesa kuihudumia.
Kitu chochote ambacho pesa unayotoa ni nyingi kuliko kinavyokuingizia ni liability
 
Mimi naona kuwa na nyumba ni muhimu sana kama huna kipato cha uhakika. Ila kama una uwekezaji wenye uhakika sidhani kama kuna haja ya kukimbilia kujenga
Yote 9&10 Kuna jamaa yupo ndani yaani seregerea now kwa case ya uhujumu uchumi wa 7b Ila Hana nyumba mtoto wake Hana sehemu ya kukaa alizoea kuishi Kila hotel hapa mjini je na huyu yupo kundi Gani lako???
 
Mkuu,
Biashara unajifunza, ni kama mwajiriwa anayekwenda ofisini kwa mara ya kwanza anajifunza kwa wengine aliowakuta na baadae anaweza kuwa mtendaji mzuri zaidi yao hata kuwa boss wao.

Kama ilivyo kwa kazi nyingine biashara pia unajifunza. Ukimwona mtu anauza vifaa vya ujenzi amejifunza, muuza nguo amejifunza, hoteli amejifunza nawewe jifunze (kama unahitaji)

Tunafahamu hatuwezi kufanya bishara wote tunachofanya hapa jukwaani ni kuelimishana na kupeana moyo na uzoefu kwa wale "wanaotaka" kufanya biashara lakini wanakosa pa kuanzia na wanatamani kupata uzoefu kwa wengine.
That's it!
 
Hapo kwenye elimu ya uwekezaji ndio umenena haswaa. Sasa hapo unaposema mtu asiwekeze kwaajilI ya pesa kodi atakuwa analipa nini? Hela haupati mara moja, ukipata leo jenga subiri ukipata nyingine ndio uwekeze....mimi nadhani mtu akishakuwa na kwake ana uwezo wa kujilipua kivyovyote maana anajua mambo yakienda kombo atakaa hata miaka miwili ajipange upya ila sisi tunaoishi kwa hisani ya baba mwenye nyumba tupo very calculating maana unajua nikibugi hapa natupiwa virago nje. Yaani ukipata hela unaogopa hata kuitumia hata kama sio muda wa kulipa kodi ...uunafikiria hivi ikifika muda wa kulipa sina itakuwaje? Yaani muda wote unawaza kodi kodI kodi
 
Yote 9&10 Kuna jamaa yupo ndani yaani seregerea now kwa case ya uhujumu uchumi wa 7b Ila Hana nyumba mtoto wake Hana sehemu ya kukaa alizoea kuishi Kila hotel hapa mjini je na huyu yupo kundi Gani lako???
Huyo nae alibugi..anakaaje hotelini na yuko na familia
 
Hizi ni fikra tu tulizo aminishwa vizazi na vizazi mkuu..Na kubadilika ni ngumu..
Mahitaji ya mwanadamu kamwe hayaishi mpaka tunaingia kaburini..Uwe na kwako,usiwe na kwako..Ishu ni je,tunawezaje kuyatimiza..
Mfano wa Mahitaji haya yapo tu..
Kula..
Afya...
Kuvaa..
Kuhudumia watoto mpaka wakue..
Utilities,(maji,umeme nk)
Kuna shughuli za kijamii wakati mwingine huwezi kuziepuka inayoambatana na gharama (misiba,sherehe,michango mbalimbali..)




Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Off course,
Pamoja na bei za vifaa kuwa juu bado tunajenga lkn pia inawezekana sana bei za vifaa ikapunguzwa ikawa na unafuu kiasi flan watu wakamudu ujenzi ulio bora

Kule juu nimekwambia bei ipande isipande no excuse ni kujenga tu, umejifanya kukaza fuvu kisha unakuja kukiri hapa…. unateseka mno.

Bei ipinguzwe na nani?
 
sio biashara mbaya,ila mtaji na malengo ya muda mrefu vizazi na vizazi yanakuwa yamezingatiwa.

tunapozunguzia hawa wafanyakaz wenye vipato dhaifu,wanataka biashara yenye return ya muda mfupi,sababu mitaji dhaifu.

hapo ndio ujenzi wa slope au chumba na sebule vyenye matoleo huzaliwa.
 
"Very calculating"
Nimependa sana huo msemo wako mama watoto, iko hivi..
Biashara zina changamoto ni kweli, unachopaswa kufanya ni kujifunza kuzizoea na kucheza nazo wakati wote na kujifunza namna bora ya kuzitatua.
Kama kuwa na nyumba yangu kutanifanya nirelax hiyo kwangu sio relief ni shida nyingine sihitaji kurelax kwasasa, huo muda utafika ila sio sasa.
Why relaxing at this age?

Inawezekana tunatofautiana kidogo lakini nikiona kuna gape fulani kwenye biashara yangu na naweza kupata pesa hata kama nalipa kodi kesho nitachukua hiyo pesa na nitawekeza, mwenye nyumba tutaongea tu si ni binadamu? halafu ukishakuwa MWAMINIFU kwenye maisha si rahisi kukwama. Naweza nikamkopa fulani nikamlipa fulani wakati nasubiri chazo fulani kitoe pesa nirudishe kwa mtu A. Lakini siwezi kukubali pesa inipite hivi hivi na nina WATU

Concept ya biashara ni pana sana.. yani ukiwa mfanyabiashara hata maisha yako binafsi unavyoongea, unavyowasiliana na watu, Mipango yako, matumizi yako, familia yako vinatakiwa viwe kibishara.

1.Jenga mahusiano mazuri na watu (marafiki wa faida) achana na kuambatana na watu wanaokata tamaa haraka.
2.Kuwa mwaminifu
3.Fanya utafiti kila mara.
4.Soma/ Jisomee ( Ongeza maarifa ya kitu unachofanya /kusudia kufanya kila upatapo fursa)
5.USIOGOPE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…