Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Nyumba yako umeikatia Bima .?..Basi tushuke kidogo..Ina Title Deed?
Kama la.. basi jua unajifariji

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app

Sijaelewa maswali yako yamelenga kwenye nini, mfano Yes nyumba haina bima so what? Unadhani hapa nchini kuna nyumba ngapi zenye bima? Karibia nyumba zote hazina bima lkn hiyo haizuii watu kujenga
 
Kama huna kipaji cha biashara, kopa, jenga nyumba. Unaweza ukazika pesa kwenye biashara ikaoza na kuwa mbolea, ila ukizika kwenye nyumba, mbegu itaota na kutoa matunda. Ila kama una kipaji cha biashara, kopa, wekeza, utajenga nyumba nyingi zaidi. Kujenga ni muhimu!!! Hivi kwa mwaka mwenye nyumba anakupiga ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kujenga ni jambo la maana sana, ila siyo kwa mkopo wala kwa ajili ya kuweka kama dhamana kwenye mkopo baadae, nyumba yako ya kuishi ibaki hivyo
 
Miaka kadhaa mingap? Unajua mwalimu wa shule ya msingi mwenye take home ya 340k akichukua hyo mil 10 kwa makato ya 200k kila mwezi anabaki na 140k kwa miaka 7..
Huyo mtumishi akiwa na familia inayo mtegemea pia ana ndugu wanamtegemea..ataishije kwa kipindi chote hicho na hana posho wala marupurupu yoyote.
Na mbaya zaid nyumba haitaisha kwa pesa hyo..ataishi kwa kuacha kadi mitaani na kuwa omba omba..

Hyo ndo hali halisi.
Anaweza akakopa pia na kuanzisha biashara na kisha biashara ikafa na kupoteza pesa zote alizokopa huku akiendelea kulipa huo mkopo na akiteseka kwa kuishi kwa nusu mshahara. Hata wewe ulikopa 12m ukaziweka kwenye biashara na zikapotea zote huku ukiendelea kuishi kwa nusu mshahara.
 
Hapa Tanzania watu wengi huchukulia kujenga na kumili nyumba ni hatua kubwa ya mafanikio katika miasha. Wafanyakazi wengi hukopa na kuishi na madeni ya viwanja na nyumba maisha yao yote ili tu wasikae katika nyumba za kupanga.

Pia wafanyakazi wengi wako tayari wasiwe na chanzo kingine chochote cha kipato kwa kuelekeza pesa yao yote wanayoipata katika ujenzi wa nyumba badala ya uwekezaji unaoleta fedha ili tu waishi katika nyumba zao wenyewe.

Katika muktadha wa utaalamu wa kifedha ni sahihi hasa kwa vijana kuelekeza nguvu na pesa zote katika ujenzi badala ya kuwekeza pesa katika biashara ambazo zitazalisha pesa zaidi na baadaye ndipo suala la ujenzi wa nyumba lifikiriwe baada ya kuwa na uhakika wa mtiririko mzuri wa kipato cha uhakika?
Kujenga ni jambo la msingi sana ila mtu ajenge kwa mujibu wa uchumi wake unavyomruhusu.
Biashara ni sawa pia ila chance ya kuzeekea kwenye nyumba za watu ni kubwa usipokuwa makini. Wafanyabiashara wengi wanacontradict mtaji na faida.
 
Maisha hayana formula. Mnao ona nyumba ni kikwazo cha maisha ya biashara itakuwa si wazoefu wa biashara. Ukiwa na nyumba mfanyabiashara ndio dhamana yako. Waulize wafanyabiashara wasio na asset nyumba wanavyozodolewa na mabank. Nimejenga na nafanya biashara najua umuhimu wa vyote.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Tusidanganyane bwana hakuna raha kama kukaa kwako kuondokana na makodi na kero za mwenye nyumba! unakuta unapanga nyumba huruhusiwi chochote mfano hata kufuga kuku wala mbwa zaidi ya kupanda maua tu na unatoa kodi ndefu wakati ukiishi kwako una uhuru na husumbuliwi kwa kodi ya mwezi wala mwaka. Kodi yoyote sikuzote inaumiza
Nilifuga mbwa nyumba ya kupanga ,niliishia kulalamikiwa na wapangaji wenzangu kuwa analeta viroboto na nikaambiwa na mwenye nyumba nitoe mbwa wangu au nihame ...niliamua kumpatia jamaangu akamfuge morogoro huko

Hakuna raha kama kuamka kwenye nyumba yako ,ukiwa na familia yako
 
Hapa Tanzania watu wengi huchukulia kujenga na kumili nyumba ni hatua kubwa ya mafanikio katika miasha. Wafanyakazi wengi hukopa na kuishi na madeni ya viwanja na nyumba maisha yao yote ili tu wasikae katika nyumba za kupanga.

Pia wafanyakazi wengi wako tayari wasiwe na chanzo kingine chochote cha kipato kwa kuelekeza pesa yao yote wanayoipata katika ujenzi wa nyumba badala ya uwekezaji unaoleta fedha ili tu waishi katika nyumba zao wenyewe.

Katika muktadha wa utaalamu wa kifedha ni sahihi hasa kwa vijana kuelekeza nguvu na pesa zote katika ujenzi badala ya kuwekeza pesa katika biashara ambazo zitazalisha pesa zaidi na baadaye ndipo suala la ujenzi wa nyumba lifikiriwe baada ya kuwa na uhakika wa mtiririko mzuri wa kipato cha uhakika?
Human BASIC NEEDS maisha ni nyumba mzee hata iwe yamabati
 
Bro tukutane ukiwa na 50 years ukiwa na hela nyingi alafu huna nyumba
utakua kituko mbele ya jamii mwisho wa siku umekufa watu ndo wanajua kutamba kote mjini kumbe huna hata kibanda cha kulala

familia yako inarudi kijijini kwakushindwa kulipa kodi...

huniambiaa chochote kujenga muhimu bana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom