Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

Kweli kabisa, mifano iko mingi mno, nimeshashudia wenye majumba kama hayo wakikimbilia kukaa na watoto wao baada ya kuona upweke, ila wajuwa mambo ya ufahari tena...
 
View attachment 1273865

Watu mnachekesha kweli nani kakuambia kujenga nyumba kubwa ni hasara? wewe kama huna uwezo pita hivi. nyumba kubwa ni faida kwa familia hata kama wakioa na kuolewa bado watakuja kusalimia na watoto wao na wake zao na waume zao sasa kama ukijenga room 2 au 3 unategemea wakwe zako wakalale hotelini au kwa jirani? hebu acheni ujinga mnasingizia hasara kumbe umaskini tu. mimi kwetu nyumba ina vyumba 7 na bado tunaongeza kwasababu familia imekuwa kubwa mno wakija hapatoshiii nasema nyumba kubwa raha asikuambie mtu wewe kama huendagi kutembea kwenu hata krismas shauri zako unapitwaaa
 
Kasome tena, hata kwenye vitabu vya Mungu kuna mfalme Suleimani alijenga
mjengo wa haja.
We ni mfalme? ndo hayo mambo yakufanya kwa vile Mfalme Suleiman alifanya......pima maisha yako.......
 
View attachment 1273865

Una familia ya watoto wanne, umefanikiwa kimaisha watoto wanasoma na unajenga nyumba ya ghorofa vyumba 12 vya kulala.

Kwanza gharama za ujenzi ni kubwa, baada ya ujenzi kutunza nyumba ya vyumba 12 ni gharama kubwa sana. Hata ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.

Nyumba ya vyumba vinne mpaka sita inatosha, pembeni unaweza kuweka houseboy quarter na guest wing.

Ukiwa mzee wewe na mke wako au mume wako kuishi kwenye nyumba ya vyumba 12 wakati watoto wote wana miji yao nayo ni gharama,
Sky, unazeeka sasa !!, nyumba ukiweza kuijenga maana yake una uwezo wa kujenga, ambao hawana nyumba au waliojenga nyumba ndogo usidhani walipenda, naamini kabisa ukitaka watu wakuja kuijaza hiyo nyumba huwezi kukosa, kwa habari yako ya kusema eti mtakuwa wapweke, kuna watu wengi sana nchi hii hawana makazi.
 
Mleta mada umezungumza ukweli kwa wenye mtazamo kama wako. Sisi wengine tuna mtazamo tofauti. Tokea tumeanza kujitambua malengo yetu ni kupambana ili tuje kujenga nyumba ya ghorofa moja na vyumba 6 vya kulala. Tusipoweza kulitimiza hili then we are a failure on this beautiful earth regardless of other factors.
Ni kweli mleta mada ameongea hisia zake zaidi, na hili linategemeana sana aina ya maisha anayoishi mtu lakini pia alivyokua, yawezekana kabisa wewe umezaliwa peke yako nyumbani kwenu, baba na mama yako hawana ndugu wengi unaowajua (yawezekana mleta mada akawa hivi), Automatically unakuwa huna mawazo ya kufikiria kuna siku watakuja ndugu zangu hapa, lakini kama mtu kwenu mlizaliwa say watu 6 au 8, mkifika mahala mkaaanzisha familia zenu maana ni kwamba hamuwezi kwenda nyumbani kusalimia wote kwa mpigo, nyumba ya wazazi say ina vyumba vitatu, mtakaaje pale, inapendeza saana mnapokutana ndugu kwa pamoja, bahati mbaya siku hizi watu wanaishia kusalimiana kwa njia ya simu na unapita mwaka ndug hawajaonana, numba kubwa ina raha yake, uiwa huna yes inaeleweka, lakini kama una nafasi jenga nyumba kubwa, ikiwezekana iwe na vyumba vyote self contained
 
Kwanza nikiri siko vizuri kwenye hesabu. Ila ghorofa tatu kuwa na 9000sqm ina maana kila floor ni 3000sqm. Nyumba ya wastani kibongobongo ni 150sqm ina maana nyumba yako ni kubwa kama nyumba 20 za kawaida. Labda ungeniambia ina ghorofa 7 au zaidi.
Hivi neno compound =nyumba?
 
View attachment 1273865

Una familia ya watoto wanne, umefanikiwa kimaisha watoto wanasoma na unajenga nyumba ya ghorofa vyumba 12 vya kulala.

Kwanza gharama za ujenzi ni kubwa, baada ya ujenzi kutunza nyumba ya vyumba 12 ni gharama kubwa sana. Hata ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.

Nyumba ya vyumba vinne mpaka sita inatosha, pembeni unaweza kuweka houseboy quarter na guest wing.

Ukiwa mzee wewe na mke wako au mume wako kuishi kwenye nyumba ya vyumba 12 wakati watoto wote wana miji yao nayo ni gharama,
Ushamba wako isiwe shida kwa wenye uwezo kwani vyumba 12 tatizo nini? Vyumba vingine unabadilisha matumizi kama home office, gym, home theater, bowling alley, billiards pool table, wine cellar, cigar room, strip club, bar, disco club, candy room, art room, sports bar na kadhalika. Ukiwa na hela unashindwaje gharama za kupiga rangi?
 
Kwanza nikiri siko vizuri kwenye hesabu. Ila ghorofa tatu kuwa na 9000sqm ina maana kila floor ni 3000sqm. Nyumba ya wastani kibongobongo ni 150sqm ina maana nyumba yako ni kubwa kama nyumba 20 za kawaida. Labda ungeniambia ina ghorofa 7 au zaidi.

Uwanja wangu ni zaidi ya Square meter nyumba tu ukubwa wa square meter 450 floor ya chini kati na juu. Sina shaka umeelewa
 
Mtoa mada sijui unawaza nini. Hiyo nyumba unayozungumzia ni mansion na mtu anayejenga mansion kipato chake kinajulikana ni kikubwa.

Ni sawa umwambie tajiri asinumue gari la gharama kisa service ni gharama.
Mkuu matajiri wengi uzeeni hizi mansion zima kuwa kama jela mtu anaishi kwenye chumba kimoja tu si ajabu hata sittingroom hafiki.
 
Back
Top Bottom