Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

moja ya malengo yangu ni kumiliki nyumba kwenye kiwanja cha hekari zaidi ya 15 yenye mabafu ya kisasa ya kuogea 8 achilia mbali vyumba vya kulala, ukumbi wa sinema, sebule 3 na mengineyo jumba liwe zaidi ya bangaroooo.... yasipofanikiwa sasa nitajenga nyumba ya kisasa ya vyumba 6 yenye kila kitu kinachoitwa cha kisasa kwenye uwanja usiopungua heka 4 to 5
 
moja ya malengo yangu ni kumiliki nyumba kwenye kiwanja cha hekari zaidi ya 15 yenye mabafu ya kisasa ya kuogea 8 achilia mbali vyumba vya kulala, ukumbi wa sinema, sebule 3 na mengineyo jumba liwe zaidi ya bangaroooo.... yasipofanikiwa sasa nitajenga nyumba ya kisasa ya vyumba 6 yenye kila kitu kinachoitwa cha kisasa kwenye uwanja usiopungua heka 4 to 5
Halafu analala nani[emoji852][emoji849]?
 
N
View attachment 1273865

Una familia ya watoto wanne, umefanikiwa kimaisha watoto wanasoma na unajenga nyumba ya ghorofa vyumba 12 vya kulala.

Kwanza gharama za ujenzi ni kubwa, baada ya ujenzi kutunza nyumba ya vyumba 12 ni gharama kubwa sana. Hata ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.

Nyumba ya vyumba vinne mpaka sita inatosha, pembeni unaweza kuweka houseboy quarter na guest wing.

Ukiwa mzee wewe na mke wako au mume wako kuishi kwenye nyumba ya vyumba 12 wakati watoto wote wana miji yao nayo ni gharama,
Nyumba kama hii ni matumizi mabaya ya fedha,bora ujenge uweke eneo la jimu,bwawa la kuogelea na vitu vingine kuliko kujenga nyumba kama guest house
 
Huu ni mtazamo wako.. unaheshimiwa. Exposure.. Umasikini.. kusaidia ndugu na vizazi na vizazi.
Nani amesema ukijenga ghorofa unasimamisha huduma zingine?
Kwa kukusaidia tu: Watu waliojenga ghorofaz wana nyumba zingine ambazo ndugu zao wanazitumia.
Wana biashara zao zinazosaidia ndugu na vizazi.
Wamewekeza kwenye miradi itakayosaidia vizazi na vizazi.
Na pia wanaojenga maghorofa huku Africa wengi wao wanapambana kutafuta mkate huko overseas. Meaning exposure siyo tatizo.

Yote huanzia kichwani kwa mpangaji. Anahitaji nini ktk maisha yake.

Wengi wenye limited pocket kama wewe ndo mna mawazo mbano.. kuwa kujenga nyumba kubwa kumepitwa na wakati.. Its not true.
Umeongea vema na ni kweli nina limited pocket.....lakin having limited pocket doesn't necessarily means sina big dreams ama situation yangu ni permanent......Lakini i want to assure you kwamba hata nikiwa na unlimited pocket "big castle" will never be my dream kwasababu sijifikiri mimi mwenyewe nawaza na wengine kwenye uzao wangu.....siwezi invest 2 billion kwenye kitu kitakashindwa kuzalisha in 50 years to come.....Ndo maana nimesema watu wengi kama wewe tunaotokea kwenye umaskini mnakuwa na poverty mentality kwamba kwa vile baba hakuweza kujenga nyumba ya ghorofa ni lazima nijenge kwa ajili ya ufahari tu nakuwa onyesha watu sisi tumetokea familia ya Mushi (kwa mfano) wakati mjomba wako wakaribu yuko kiraracha kwenye nyumba ya udongo......think beyond not just for your self........Angalia kwa mfano ghorofa la billionea Msuya taking into account current status ya watoto......wakiachiwa unafikiri wanaweza kuli maintain kuwa kwenye standard kam baba yao alivyoliacha? lakini angalia at the same time investment ya baba yao ya Hotel ndo inayo wasomesha nakuwapatia mahitaji......Mimi i will go for a small house regardless ya kiasi gani ninacho the rest i will invest......
 
Dunia sio Mji udumuo. So tafuta sehemu ya kujibanza make Mungu keshatuandalia makao, ili alipo nasi tuwepo.
 
Nimetafakari na nimerudi. Jumba kubwa sometimes ni zuri kusudi kila mtu na kitanda chake, siku ya kugawa dozi ndo mnashare, siku nyingine kila mtu na hamsini zake.
 
Cha muhimu fanya kile kitachokupendeza kulingana na uwezo wako.

Yaani maskini ajenge nyumba ya vyumba viwili na Bakhresa nae ajenge hivyo hivyo si matumizi mabaya ya utajiri?

Mola akikiruzuku mali basi pamoja na mambo mengine ishi sehemu nzuri, kula vizuri, vaa vizuri, tembelea gari zuri nk
(usisahau kuwasaidia wasiojiweza)

Elewa mada, hapa hatuongelei kuishi vizuri, bali kujenga nyumba kubwa ya kuishi familia.
 
Hakunaga umoja kwenye familia za ngozi nyeusi.na hii husababishwa na wazazi kupendelea mmoja
Ni kweli Ila wengine hujenga ziwe Kama generational houses ndio maana mfano kwa matajiri wa huko kwa wenzetu ni kawaida kuona nyumba inamilikiwa na familia kwa miaka 50/100.
Ila hili kwetu ni gumu
 
Mimi nikashaona mtu kajenga nyumba kubwa ya kuishi familia huwa namuona ni ng'ombe tu.
 
Ukijenga nyumba kubwa sana ukifa watakaobaki wataliuza maana hawataweza kihudumia.
 
Mleta mada acha kupiga chenga...hasara kuu ya nyumba kubwa ndugu yangu ni....WAGENI WATAFANYA KWAO..WATAHAMIA...hakuna asiejua kashkash za kuwa na familia kubwa hapa jijini....
watu wakiona jumba kubwa wanahamia...sasa wahamie watu 5..na wewe na mke na watoto na beki 3..labda watano..mnakua kumi (10)...lazima upaki gari..na bado hawajaanza tabia zao halisi...utahama kwako
Hili ni tatizo sana
 
Mleta mada acha kupiga chenga...hasara kuu ya nyumba kubwa ndugu yangu ni....WAGENI WATAFANYA KWAO..WATAHAMIA...hakuna asiejua kashkash za kuwa na familia kubwa hapa jijini....
watu wakiona jumba kubwa wanahamia...sasa wahamie watu 5..na wewe na mke na watoto na beki 3..labda watano..mnakua kumi (10)...lazima upaki gari..na bado hawajaanza tabia zao halisi...utahama kwako

Hili halina ubishi kwa nchi masikini
Jamaa juzi ananiambia kajenga nyumba ya gorofa tatu kwa ushawishi wa mke wake
Jamaa yuko nje ya nchi akirudi home anakuta nyumba imejaa na wengine wanamuita ANKO hata hawajui
Inabidi ashukie hotel tu
Sasa huu si utumwa kwenye nyumba yako mwenyewe
Waafrika shida sana
 
Mbinguni kuna makao mazuri sana, ya nini kuhangaikia mapito ya hapa duniani huku tukijua tunapita tu.... bwana Yesu yuko bize kutuandalia makao mazuri kwa kila mmoja wetu.

Farijianeni kwa maneno hayo, mengine yote ni ubatili mtupu.... na hata usiku utapokwisha.
 
Back
Top Bottom