Kujenga uwanja wa siti 32,000 Dodoma, Ni kukosa Maono

Kujenga uwanja wa siti 32,000 Dodoma, Ni kukosa Maono

Huko kwa Mkapa mnajaza uwanja kwenye mechi ya simba dhidi ya yanga tu na siku za matamasha ya hizo timu, na hiyo ni tangu ulipozinduliwa na mpaka sasa, haijawahi kubadilika. Yaani matukio manne tu kwa mwaka ndio yanajaza uwanja hapo Dar.

Sasa kwa dodoma uwanja wa mashabiki elf 30 unatosha kabisa ndani ya miaka hata 50 na huo uwanja utajaa endapo tu mechi ya simba dhidi ya yanga inachezewa hapo au kwenye mkutano wa Mwamposa. Uwanja mkubwa kabisa huo , wewe ndio hujui ni matukio gani yanajaza uwanja. Hata fainal ya AFcon ikipigwa hapo Senegal vs Nigeria huo uwanja haujai.
 
Uzinduzi wa mbwembwe kujenga uwanja ambao upo chini ya viwango vya fifa ni kukosa maono na kufanya siasa chafu kwenye mambo ya maana.

Uwanja wa siti 32K ni uwanja wa levo ya halmashauri kama kinondoni walivyo jenga pale mwenge.

Ilikuwaje mkapa miaka 30 iliyopita aliamua kujenga uwanja wa siti 60,000?, wakati huo pengine ulikuwa haujai lakini leo unajaa hadi kukosa nafasi.

Design ya wakati wa Magufuli uwanja ulikuwa na capacity ya siti 85,000 imekuwaje tumefilisika hadi kujenga uwanja wa siti 32,000 kwenye makao makuu ya nchi?
Hujui kama kuna mgomo baridi kuhusu maendeleo ya dodoma,Hujui kama kuna watu hawataki maendeleo kuletwa dodoma.unajua kuwa ile budget ya uwanja wa samia Arusha ilikitakiwa iwekwe ijenge dodoma. Huko maendeleo yanapelekwa kishingo upande wanaihujumu kimakusudi Dodoma. Hata ule uwanja wa Ndege wa msalato unajengea chini ya kiwango. Kwa maksud kabisaa. Progress ya ukuaji wa dodoma ni ndogo mno.
 
Usitambe sana kuwa una akili kama akili zako ndiyo hizo unazoonyesha hapa. Uwanja wa 30K ni standard nzuri tu kwa Dodoma na maeneo mengi nchi hii hata kwa miaka 20 ijayo.

Mmejifunza wapi kuwa uwanja wa kuingiza watu 30K ni mdogo? Mnataka kila mtu aende uwanjani mbona kwa Mkapa tu hapo uwanja unapelea karibu mechi zote hata zile kubwa au bado population haijawa kubwa? Watu wanajazana vibanda umiza halafu uwanja mtupu.

Elekeza nguvu huko kwenye barabara nitakuunga mkono, na nimewahi kulilalamikia hilo sana tu, ila si kwenye huu uwanja unaojengwa kwa ajili ya watumishi wa serikali na wanasiasa.
Hamtaki kupata furusa ya ku-host mashindano makubwa mfano wa AFCON, CHAN au ya FIFA peke yenu bila kushirikiana na nchi jirani miaka michache ijayo?
Hamuoni kuna faida kubwa kiuchumi endapo hatugawani wageni na nchi zingine wakati wa mashindano?
Siyo lazima tujaze Viwanja wenyewe tu.
Wageni wanaweza leta mashindano yao hapa kama Supercopa de Espana ilivyofanyika Saudi Arabia.
Pia kujenga uwanja mdogo kisha unarudia upya kujenga tena uwanja huo huo chini ya miaka 40 Ni upotevu wa pesa bure.
Hatujifunzi viwanja vya Ulaya na Amerika ya Kusini vilijengwa vikiwa na ukubwa ule?
 
Usitambe sana kuwa una akili kama akili zako ndiyo hizo unazoonyesha hapa.
Mimi sitambi bali nashangazwa umebadilika lini kutoka kiwango chako hadi low level uliyo onesha hapa.
Nakitambua kiwango chako ni kikubwa si hiki.
Nahisi umekumbwa na wimbi la kutetea mambo ya hovyo sababu za kisiasa. Achana na siasa mkuu.
 
Hamtaki kupata furusa ya ku-host mashindano makubwa mfano wa AFCON, CHAN au ya FIFA peke yenu bila kushirikiana na nchi jirani miaka michache ijayo?
Hamuoni kuna faida kubwa kiuchumi endapo hatugawani wageni na nchi zingine wakati wa mashindano?
Siyo lazima tujaze Viwanja wenyewe tu.
Wageni wanaweza leta mashindano yao hapa kama Supercopa de Espana ilivyofanyika Saudi Arabia.
Pia kujenga uwanja mdogo kisha unarudia upya kujenga tena uwanja huo huo chini ya miaka 40 Ni upotevu wa pesa bure.
Hatujifunzi viwanja vya Ulaya na Amerika ya Kusini vilijengwa vikiwa na ukubwa ule?
Kuhost mashindano peke yako ni zaidi ya kuwa na viwanja vya kuingiza watu 100K kila kimoja. Suala zima la miundombinu lazima lizingatiwe ambalo sisi tuna safari ndefu mpaka kulifikia. Na nchi nyingi hata zilizoendelea wakipata fursa za kuhost mashindano huwa wanajenga viwanja vipya, hawategemei sana viwanja vya zamani.

Nchi kadhaa kuhost pamoja ndiyo trend kwa sasa na inafanyika hivyo kwa sababu za kiuchumi, kisiasa na kijamii za nchi hizo. Inazaleta nchi hizo karibu ingawa nahisi kwa Afrika tunafanya kwa pupa bila kuwa na mipango thabiti iliyo endelevu.

Pia naomba uondoe ndoto za Tanzania kuhost Kombe la Dunia kwa miaka 50 ijayo!

Wageni hawawezi kuleta mashindano Dodoma kukufurahisha wewe, wanafanya hivyo kwa sababu za kibiashara. Tumelala hadi draw za robo fainali za CAF na mechi ya Super Cup ya CAF inafanyikia Saudi Arabia, halafu wewe una ndoto za kushindana nao?
 
Mimi sitambi bali nashangazwa umebadilika lini kutoka kiwango chako hadi low level uliyo onesha hapa.
Nakitambua kiwango chako ni kikubwa si hiki.
Nahisi umekumbwa na wimbi la kutetea mambo ya hovyo sababu za kisiasa. Achana na siasa mkuu.
Naomba nikukumbushe tu nchi hii hatupo serious katika michezo, tunabangaiza tu. Kumbuka ni mwaka jana tu Waziri alipiga marufuku watu kuvaa jezi ya klabu fulani ngeni kisa alitaka tuonyeshe uzalendo, wewe unawaza kuhost World Cup?

Uwanja wa Mkapa una miaka 20 ila haujawahi kuhost hata tukio moja la kimataifa la mashindano ya riadha hadi zile running tracks zikachakaa. Pia jaribu kukumbuka ramani ya uwanja ilitegemewa ijumuishe nini na nini ila mpaka leo havijajengwa. Viti vimechakaa, wakiambiwa wabadilishe wanakodoleana macho. Vyoo vinajaa maji na vichafu, ndiyo unataka kuhost mashindano ya dunia?

Nakukumbusha tu haya ili urudi kwenye uhalisia.
 
Uzinduzi wa mbwembwe kujenga uwanja ambao upo chini ya viwango vya fifa ni kukosa maono na kufanya siasa chafu kwenye mambo ya maana.

Uwanja wa siti 32K ni uwanja wa levo ya halmashauri kama kinondoni walivyo jenga pale mwenge.

Ilikuwaje mkapa miaka 30 iliyopita aliamua kujenga uwanja wa siti 60,000?, wakati huo pengine ulikuwa haujai lakini leo unajaa hadi kukosa nafasi.

Design ya wakati wa Magufuli uwanja ulikuwa na capacity ya siti 85,000 imekuwaje tumefilisika hadi kujenga uwanja wa siti 32,000 kwenye makao makuu ya nchi?
Hata hii reli ya umeme nakuhakikishia kama angekuwa mkwere na huyu mama tungejengewa ya disel kwa bei sawa na ya hii ya umeme
 
Back
Top Bottom