MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Habari wakuu,
Kuna kisa ambacho nisingependa kukiweka hapa lakini kimenivutia kuandika kidogo ufahamu juu ya tattoo kama ni dhambi au vibaya kwa muono wangu binafsi.
Kujichora tattoo kwa sehemu kubwa ya jamii zetu inachukuliwa kama uhuni na kila tafsiri mbaya. Lakini zipo jamii za kiafrika ambazo kujichora ni sehemu ya utamaduni wao.
Kwa wakristo wengi husimamia mstari kutoka kwa walawi kuzungumzia ubaya au dhambi ya kujichora tattoo. Mstari wenyewe unasema 28 Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.
Ukipekuapekua hakuna sehemu nyingine kwenye maandiko imezungumzia ubaya/uzuri wa kujichora. Mstari huo wa walawi ni sheria aliyoweka Mungu kwa Waisraeli na si kwa Wakristo. Ukisoma walawi 19 yote utagundua yapo ambayo hayawahusu Wakristo kwa mfano maagizo ya kutovaa nguo mbili pamoja nanukuu 19 Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja. Mambo ya Walawi 19 :19
Kama nilivyosema kujichora inaweza kuwa si dhambi lakini michoro hiyo isiwe alama zinazowakilisha vitu vilivyo kinyume na Ukristo kama matusi, alama za kishetani n.k.
Kutokana na ufahamu mdogo wa vijana wengi wamejikuta wakiingia kwenye mikataba ya kishetani kupitia namna mbalimbali ya kujichora bila wao kujua. Hivyo ni bora kujiepusha au kuchukua tahadhari za kutosha ukiamua kujichora tattoo.
Vijana wanazidi kupenda kujichora wakifata mifano ya wasanii na watu maarufu wanaowapenda bila kujua 'motives' za michoro hiyo.
Wimbi linazidi kuwa kubwa sana. Tuelimishane badala ya kutishana tu.
Je, kujichora tattoo ni dhambi? Karibuni kwa mitazamo zaidi ya kimaadili na kidini tuwasaidie vijana.
Update ya mdau
mazojms; Kuchora tatoo sio dhambi wala sio upungufu wa maadili, ila utakachokichora na sehem utakayochora ndicho kinaweza kukufanya uonekane unakosa maadili.. Kiafrika tatoo zilikuwepo toka enzi na enzi kama ishara ya urembo kwa wanawake na ushujaa kwa wanaume.. technologia waafrica tuliotumia zamani ilikuwa ni salama kiafya (tatoo zilikuwa zinawekwa kwa moto au kwa kuchanwa na vitu vyenye ncha kali)tofauti na utaalam unaotumika sikuhiz.
tatoo ink(wino)una chemicals nyingi including heavy metals ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu..na zinapowekwa chini ya ngozi nyingine huingia katika mzunguko wa damu (sumu hizo zikifikia kiwango fulani katika damu husababisha kansa ya damu, Pia kiwango cha sumu hizo kikizidi kwenye damu na ini..ndio maana watu wenye tatoo hawaruhusiwa kuchangia damu.