Kujichora tattoo ni vibaya au dhambi?

Kujichora tattoo ni vibaya au dhambi?

Nafikiri nilitoa maelezo kabla ya kuhitimisha kama ni dhambi au la.
Maelezo yako yamejaa mantiki zako binafsi kuliko maandiko. Hata mimi sitaki hata kusikia habari za kujichora lakini hii inaweza kuwa sababu ya jinsi nilivyolelewa kimaadili ya jamii yangu lakini si rasmi sana kueleza ubaya wake.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Nimezoea kuona wafungwa wengi hutokea jela na tattoo, mbali ya hapo wanawake
wanaojiuza wengi walikuwa wanachora “fu.k my ass as much as u can” mgongoni au kwenye chura. Wakizeeka au wakienda kumuona daktari aibu inawapata wanaanza kusema samahani.

Sikuhizi watu huchora tattoo majina ya wapenzi wao.
Ww mrembo umejichora ipi
 
Aongeze nyama kilo ngani Mkuuu[emoji23][emoji23][emoji23]
Ujue unapoandika jambo hapa unasaidia wengi mno. Hivyo ni vyema kuandika kwa namna ya kusaidia wengi.
 
Tatoo ni dhambi maana ni chale za kisasa wanaochora wengi hupewa hizo tatoo na wakuu wao kwahyo zina maagano
 
Maelezo yako yamejaa mantiki zako binafsi kuliko maandiko. Hata mimi sitaki hata kusikia habari za kujichora lakini hii inaweza kuwa sababu ya jinsi nilivyolelewa kimaadili ya jamii yangu lakini si rasmi sana kueleza ubaya wake.
Walawi 19 kama ulivyoitaja inataka tuwe watakatifu. Na yakaelezwa mengi ya kutuweka watakatifu ikiwa na hilo la kutojichanja.
Kinyume cha mtakatifu ni mdhambi.
Hivyo tatoo ni dhambi.
 
Tatoo ni dhambi maana ni chale za kisasa wanaochora wengi hupewa hizo tatoo na wakuu wao kwahyo zina maagano
Wewe ukienda kuchora na kuandika I love Jesus ni dhambi?
 
Habari wakuu,

Kuna kisa ambacho nisingependa kukiweka hapa lakini kimenivutia kuandika kidogo ufahamu juu ya tattoo kama ni dhambi au vibaya kwa muono wangu binafsi.

Kujichora tattoo kwa sehemu kubwa ya jamii zetu inachukuliwa kama uhuni na kila tafsiri mbaya. Lakini zipo jamii za kiafrika ambazo kujichora ni sehemu ya utamaduni wao.

Kwa wakristo wengi husimamia mstari kutoka kwa walawi kuzungumzia ubaya au dhambi ya kujichora tattoo. Mstari wenyewe unasema 28 Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.

Ukipekuapekua hakuna sehemu nyingine kwenye maandiko imezungumzia ubaya/uzuri wa kujichora. Mstari huo wa walawi ni sheria aliyoweka Mungu kwa Waisraeli na si kwa Wakristo. Ukisoma walawi 19 yote utagundua yapo ambayo hayawahusu Wakristo kwa mfano maagizo ya kutovaa nguo mbili pamoja nanukuu 19 Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja. Mambo ya Walawi 19 :19

Kama nilivyosema kujichora inaweza kuwa si dhambi lakini michoro hiyo isiwe alama zinazowakilisha vitu vilivyo kinyume na Ukristo kama matusi, alama za kishetani n.k.

Kutokana na ufahamu mdogo wa vijana wengi wamejikuta wakiingia kwenye mikataba ya kishetani kupitia namna mbalimbali ya kujichora bila wao kujua. Hivyo ni bora kujiepusha au kuchukua tahadhari za kutosha ukiamua kujichora tattoo.

Vijana wanazidi kupenda kujichora wakifata mifano ya wasanii na watu maarufu wanaowapenda bila kujua 'motives' za michoro hiyo.

Wimbi linazidi kuwa kubwa sana. Tuelimishane badala ya kutishana tu.

Je kujichora tattoo ni dhambi? Karibuni kwa mitazamo zaidi ya kimaadili na kidini tuwasaidie vijana.

Religious beliefs pembeni, kuna scientific studies zimeonesha health risks za tattoos. Pengine hii ndiyo njia rahisi ya kuielewesha akili ndogo ya kibinadamu. Hayo mengine ya kiimani ni too complicated kwa akili ya kibinadamu!
 
Religious beliefs pembeni, kuna scientific studies zimeonesha health risks za tattoos. Pengine hii ndiyo njia rahisi ya kuielewesha akili ndogo ya kibinadamu. Hayo mengine ya kiimani ni too complicated kwa akili ya kibinadamu!
Interesting ...tusaidie hizo risk mkuu!
 
Kuna Watu wanafatilia mjadala huu kimya kimya na tattoo zao tayari mwilini wanasubiri facts!
 
Vijana wanapenda watu maarufu kama hawa na kuwaiga. Tuwaambie ukweli badala ya kuwatisha tu.
diamondplatnumz-1543767046663.jpg
 
Unahitaji majibu kiafya au kiimani..........kiimani sifahamu lakn kiafya ni mbaya
 
Back
Top Bottom