GE2025 Kujiuzulu kwa Polepole na maswali 7 yanayofikirisha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Naona Polepole kawapiga na kitu kizito kisogoni ndo maana chawa mmepaniki. Hamkutarajia.
 
 
nitakujibu swali moja baada ya moja baadaye mkuuu , acha tufanye kazi kwanzaaa
 
Mimi kampuni zangu zinadai pesa za kandarasi 6 za ujenzi wa barabara tangu mwaka jana.
Hela ziko wapi!!??
 
Hatuna muda wa kufikiria tena Wala kusoma mafikirio ya mtu
 
Polepole ni msalia ya Mwendazake, hawezi kuona hiyo picha kubwa (big picture) uliyoiweka kwa vile Samia AMENG'ARA katika performance tofauti na matarajio ya Sukuma Gang waliotaka kumpora madaraka.
Rais hutizamwa kwa mambo mengi ya nchi sio mnamuelezea kama unamuelezea waziri wa wizara tu, wakati huu matukio ya wasiojulikana yamezidi kupamba moto na jeshi la polisi ndio linatuhumiwa katika huu uongozi wake ila hadi sasa ni kama watanzania inabidi tukubali kuwa hiyo hali ni sehemu maisha yetu hatuoni Rais Samia kushughulikia hili ili apewe hizo sifa.
 
Wewe umevaa miwani ya mbao huwezi kuona mafanikio ya Samia
Hao wasiojulikana mwanzilishi wao ni Magufuli na idadi ya walioptea kipindi chake inafika 400 na zaidi (MKURANGA, kibiti na Rufiji). Kumbuka vile viroba vya kuokotwa baharini.
 
Kumbe ni hoja za Uchawa🚮🚮🚮🚮
 
Polepole ameona amekaribia kufa hivyo hataki kuondoka na dhambi za kuua na kuteka alizoshiriki utawala uliopita, atulie na wenzake waendelee kuteka
Mkuu acha aseme. Kuna mtu alitubu msalabani akielekea kufa na kutangaziwa msamaha.
Maneno ya polepole tena akimwandikia Rais yana impact kubwa sana na yamewachanganya kuliko mimi na wewe hata tungetumia tarumbeta.
Kwanza atakuwa kama kafungua zizi sasa kila mtu atataka kutoka nje naye aseme. Wamekwisha! Kumbuka huyu alikuwa balozi Cuba na nchi za Caribbean hivyo wote wanataka kujua kwa nini kajiuzulu
 
Assnte kwa and andiko ila kuna vitu vya kuzingatia;

Binafsi huwa nashangazwa sana na watu wanaohoji ni kwanini mtu aliyefanya jambo la maana hakufanya jambo hilo kipindi flani. Mi nadhani cha muhimu ni kuangali, je. Alichofanya ni sahihi na kuishi humo. Soma biblia kuhusu mtu aliyeitwa sauli na baadae kuwa Paulo.

Nadhani ni wakati muafaka sasa wa watu na vyama vya siasa kujikita kwenye hoja anazozitoa mtu badala ya kumshambulia yeye binafsi. Tunapoenda, watu wataanza kuamini kuwa ukiwa na mawazo tofauti kwenye chama, utashighilulikiwa
 
Wewe umevaa miwani ya mbao huwezi kuona mafanikio ya Samia

Hao wasiojulikana mwanzilishi wao ni Magufuli na idadi ya walioptea kipindi chake inafika 400 na zaidi (MKURANGA, kibiti na Rufiji). Kumbuka vile viroba vya kuokotwa baharini.
Sasa ndio tungetegemea kuona huu uhalifu unakomeshwa katika huu uongozi wa Samia ila cha ajabu ndio tunaona mambo yanazidi kukomaa watu wanatekwa na kuuliwa wazi wazi kabisa na watu wenye kujitambulisha kama polisi. Sasa mnapoelezea huu uongozi wa rais Samia msifumbie macho na mambo kama haya kana kwamba hayapo au hayamuhusu rais Samia katika uongozi wake, mnaweza mkaona mnaeleza mafanikio yake ila kumbe yaliyomshinda ni mengi au mabaya zaidi kuliko hayo mnayohisi ni mafanikio yake.
 
System nzima imeoza kuna majangili yameikamata yanapeleka wabunge wawili wawili Doto na ndugu ake, Mchengerwa na mke wake, Ridhiwani na mama ake, Wasira anapambana ukoo wake ujae kwenye mfumo, Makamba n.k wapuuzi wengine
 
Sasa mtu kama Mdude_Nyagali alikuwa na faida gani zaidi ya kutukana viongozi??
 
Huna hoja, kajipange ndiyo urudi. Samia mi-5 tena
 
Kuongezwa bajeti ya afya Kuna mdaidia nini mtanganyika wa kawaida.?
Kumuona tuu Dr JKCI 35000
Kujifungua kwa upasuaji 300000
Kutahiriwa 50000
Kila dawa hospital ya serikali ni juu ya pharmacy za watu binafsi
 
JAMAA HANA UZALENDO WOWOTE ZAIDI YA UZALENDO WA TUMBO LAKE
Ni kweli inawezekana hana,lakini ni wangapi wako tayari kuachia nafasi zao zenye masilahi kwa matumbo yao?naona hilo la uzalendo wa tumbo lake slow slow kama amelikataa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…