GE2025 Kujiuzulu kwa Polepole na maswali 7 yanayofikirisha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Umeacha mambo muhimu and it's obvious umeyaacha kwa makusudi kabisa.
Two wrongs don't make anything right, vipi haujazungumzia bibie kuendelea utekaji, utesaji na uuaji? Vipi kuhusu Wamasai kuhamishwa kama ng'ombe wanaoswagwa kutoka katika makazi yao na hayo makazi kupewa Waarabu kwa makubaliano ambayo hayako wazi? Kuna usiri wa nini? Vipi bandari za Tanganyika kugeuzwa shamba la bibi huku za Zanzibar zikibakia kuwa untouched?
 
Nepotism at it's peak.
 
Polepole ni masalia ya Mwendazake, hawezi kuona hiyo picha kubwa (big picture) uliyoiweka kwa vile Samia AMENG'ARA katika performance tofauti na matarajio ya Sukuma Gang waliotaka kumpora madaraka.
Ameng'ara? Labda kama ameng'ara kwenye kalio lako.
 
Umekuja kumsifu Bi Kizimkazi na kumwimbia mapambio tu kamakawaida yenu lakini hujajibu hoja wala kubadilisha fikra za yeyote kusema tuna Rais hapo

Tanzania mpaka hapa tulipo hatuna kuongozi wa nchi, bali tuna kundi/genge la wahuni na washenzi fulani tu ndo wanaiburuza nchi hii watakavyo huku mama yenu akiwa kama kinyago au picha tu isiyo na maana yeyote

Sisi hatuna shida na historia ya nyuma ya mtu. Lakini anayetoka na kukiri kwa kinywa chake na kuamini moyoni mwake kuwa, nchi hii kwa sasa inahitaji mabadiliko ya kimfumo na kiutawala na kuungana na wanaodai mabadiliko hayo na tukamwangalia na kuona kuwa amebadilika, huyo ni mwenzetu

Kwa ujasiri wa Polepole kutema marupumarupu ya ubalozi na kukosoa serikali na boss wake hadharani, anastahili kuungwa mkono

Lakini, we are very carefully. We are still scrutinizing his honesty yet
 
Porojo ndefuu pumba tupu
 
Tunamsaidia kufanya nini?
Magu alipendwa na wengi mno huku mtaani hata kifo chake watu 45 walipoteza maisha wakimuomboleza.. ila huyu hapendwi hadi na wanawake wenzie ni Rubbish President
 
Mleta mada katumia nafasi ya kumshushua mwenzao wakati akipiga Kampeni kwa Samia kwa kuweka takwimu ambazo ni wajibu wa serikali kutimiza hayo; lakini anasahau kuwa mizani (kwa bahati mbaya siku hizi siyo analog tena, imekuwa digital) ya upande wa ili ni nzito zaidi ya hayo aliyoyapigia chapuo yeye.

Nikikaa hapa na kutazama huo upande wa pili, nitajaza kurasa; na muda huo kwa sasa sina. Itoshe tu kusema kuwa la msingi zaidi ni HAKI ya mTanzania kuwa HURU kumchagua kiongozi yeyote anayemtaka yeye, bila ya kusumbuliwa, wala kuwa na mashaka ya kura yake kuhesabiwa. Samia hili kwake ni sumu, na hili ndilo linamwondolea heshima yoyote ya kuwa kiongozi wa nchi. Sasa tunasubiri auwe waTanzania ili aendelee madarakani kwa nguvu.

Utajenga mashule ya kueneza ujinga huo uendelee; utajenga mahospitali ya watu wajinga wasiokuwa na haki yoyote ya kuwachaguwa viongozi wao?
Unajenga mahospitali kujaza wagonjwa wenye msongo wa akili? Tena mahospitali ambayo huduma zake wananchi hawana uwezo nazo?

Sijasema chochote katika uharibifu unaofanywa na Samia juu ya raslimali za taifa hili; na zaidi sizungumzii kuwatengeneza waTanzania kuwa watwana ndani ya nchi yao wenyewe! Kiongozi asiye amini wananchi wake kuwa na uwezo.

Hizo shule zinajengwa zifanye kazi gani, ya kutengeneza watwana; badala ya watu wanaojiamini na kuamini uwezo wao wa kujiletea maendeleo yao wenyewe?

Hili ni jibu la haraka haraka, bila ya mpangilio maalum, kuonyesha ubovu wa uongozi wa Samia Suluhu Hassa; mtu asiyekuwa na dira yoyote juu ya nchi hii! Mtu aliye okotwa tu; na kuewa uongozi wa nchi ambayo hana uchungu wowote juu yake!.

Mwisho: Sasa kaishika CCM, yeye na GENGE lake, siyo CCM Chama cha wananchi tena. Hili nalo tumpongeze; wakati akichochea mifarakanyo kati yetu wenyewe, kwa kujenga makundi kwenye jamii zetu, ili tufarakane zaidi?
 
Ndio ulaghai wenyewe huo. Hawa watu wanapenda sana kutumia hadaa nyingi na ulaghai kujionyesha kuwa wamefanya kazi kubwa, wakati ni hewa tupu!
Haajawahi kuwa na serikali yenye uongo mwingi kama hii ya Samia Suluhu Hassan.
 
POLE FISADI NA NUSU WALIOTAKA UBUNGE 2020 WANAMJUA VIZURI SANA
OCTOBA NI TIKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

MAMA ANAFANYA KILA SEKTA YEYE TU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…