Kujivunia maendeleo makubwa ya sekta ya barabara ndani ya miaka 60 ya Uhuru bila kumtaja Hayati Magufuli ni makosa makubwa ya kihistoria

hakuna mwenye muda mchafu wa kumtaja huyo mungu wenu
 
Kwanza.. Alikua anatimiza wajibu wake kama wazir husika wala hakua anapigana ili barabara zijengwe! Pili.. hizo ni kodi za watz wala hakua anatoa pesa na ideas yeye barabara zijengwe wap yeye alikua anatimiza muongozo na dira ya maendeleo ya chama. Tatu.. JK kipind chake ndipo zimejengwa km nyingi za barabara. Hivyo bas nan anapaswa kukumbukwa kweny hili??
 
Na hapa Tanzania hatuna barabara bali tuna vibarabara vingi
 
Hao mawaziri wa ujenzi huko nyuma hawakulipwa mishahara?

Kuita madaraja au barabara majina kuna kosa?
Kama unataka kutoa sifa kwa mabarabara basi Mkapa ndiye anastahili. Mkapa ndiye alileta mapinduzi ya barabarani nchini. aliunda Bodi ya Mfuko wa Barabara (Tanzania Road Fund) ambayo iko empowered kukusanya fedha za barabara kupitia petroli na dizeli tunayonunua kama una gari. Hiyo ndiyo fedha inayo finance ujenzi wa barabara just in case ikisikia chanzo cha ndani. Kwa hiyo JK na Magufuli wamekuta MKAPA kawatengenezea.

Pili Mkapa aliunda TANROADS sambamba na huo mfuko wa maendeleo ya barabara

Mkapa alijenga barabara a Singida- Shelui- Nzega- Mwanza na kufanya Watanzania wa Bukoba na Mwanza waache kupita Kenya na Uganda wakienda makwao.
 
Wakati Road fund inaanzishwa JPM alikuwa wapi? Wakati Tanroada inaanzishwa JPM alikuwa wapi.

Nani alikuwa msimamizi wa pesa za Road fund ili kujenga mabarabara kwa zaidi ya miaka 20? Nani alikuwa msimamizi wa Tanroad kwa zaid ya miaka 20? Kama sio hayati JPM?

Unadhani kwa nini Hayati Mkapa alimuita askari wa Mwavuri?
 
Kweli kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
June 8 2015 kumbe Magu alikuwa Rais tayar?
 
Magufuli hakwepeki nchi hii hata walie, wagale gale, wakiamka watakuta SGR yenye sura ya Magufuli.

Hata walie wagale gale wakiamka watakuta Bwawa kubwa la umeme lenye sura ya Magufuli.

Hata walie wagale gale wakiamka watakuta flyovers zenye sura ya Magufuli.

Hata walie wagale gale wakiamka watakuta ndege kubwa zenye kupendeza lkn zina sura ya Magufuli.

Hata walie wagale gale wakiamka watakuta barabara pana zenye viwango lkn zina sura ya Magufuli.

Hata walie wagale gale wakiamka watakuta meli kubwa pale ziwa Victoria yenye sura ya Magufuli.

Hata walie wagale gale wakiamka watakuta madaraja ya kisasa yenye sura ya Magufuli.

Hata walie wagale gale wakiamka watakuta kampuni ya Twiga inayosimamia madini ya Tanzania ina sura ya Magufuli.

Hata walie wagale gale wakiamka watakuta Dodoma ina sura ya Magufuli.


Magufuli hakwepeki, Magufuli ndiyo muanzilishi wa Tanzania mpya, Magufuli was the real deal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati mbaya wakati wa awamu yake ya urais barabara hazikujengwa na zile alizokuta zimeanza pia zilisimama. Alijitahidi kujenga kilometa chache kwenye makao ya wilaya/mitaa.
 
Kuwa na akili kidogo, kwa hiyo ufisadi huo ni Magufuli kaufanywa?
 
Sio kila wakati lazima kufanya porojo, za kisisa, aliochemka ntu aambiwe hapa umechenka, alipo fanya vema aambiwe hapa umefanya vyema, uchumia tumbo ndio hasara ya taifa hili, hapa ndio wanapoibuka akina sgang na wote wafananao na wao.
 
Kuwa na akili kidogo, kwa hiyo ufisadi huo ni Magufuli kaufanywa?
Habari za Magufuli kuwa fisadi Papa kwa kupiga ufisadi wa TZS 1.5 trilioni ziliandikwa kila mahali ikiwa ni pamoja na hapa JF lakini kwa sababu ya wewe kuwa mjinga unataka kushindana na mimi ila mradi unipotezee muda.

Hukufuatilia ripoti ya CAG?Hufuatilii yanayoendelea katika nchi yako?


 
Ukitaka hivyo basi, watu wanaostahili sifa ni wale ma technicians walioendesha ma grader kusawazisha na kumwaga lami. Maana yeye alikuwa msimamizi wa sera ya ujenzi tu, na Katibu Mkuu ndiye alikuwa afisa masuruli
 
Ukitaka hivyo basi, watu wanaostahili sifa ni wale ma technicians walioendesha ma grader kusawazisha na kumwaga lami. Maana yeye alikuwa msimamizi wa sera ya ujenzi tu, na Katibu Mkuu ndiye alikuwa afisa masuruli
Umekosa hoja, inaonekana una chuki binafsi na hayati JPM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…