Kukamatwa kwa Mtanzania Kiongozi wa Waasi nchini Msumbiji: Kwanini hakuripotiwi na Vyombo vyetu?

Nani kathibitisha uraia wa huyo jamaa- au kuongea Kiswahili ndio uthibitisho wa Uraia. Mambo haya hayaitaji papara- viache vyombo vya habari vifanye kazi yao ya uhakiki wa Taarifa. Vyombo vya Tz vikitangaza bila uhakika ni kwa faida ya nani? Wanalichafua Taifa gani? BBC wao wapo kwenye mashindano ya breaking news- ya vyombo vya habari vya kimataifa.
 
Kwann sasa walimuua Azory aliyetaka kutoa Siri za kuuwa kwa watu wasio na hatia kwa kuhisiwa tu.
 
WELL SAID
 
Kuna ajira na kazi, tofautisha vitu hivyo. Ukikosa ajira unaweza ukapata au ukafanya kazi badala ya kujiingiza kwenye makundi haya ya kihalifu
Bora ukalime bange kuliko kujiunga na makundi ya hao wahuni mbona huwa awalipwi chochote zaidi ya ugali maharagwe baada ya kulambishwa propaganda feki.
 
BBC sio Tbc taarifa zao huwa ni za uhakika wanzifanyia uchunguzi.
Check BBC eyes kwa taarifa zote za uchunguzi.
Huyo Ali mbona anafahamika kwa wakazi wa vijijini jirani na Msumbiji hata familia yake inafahamika.Ni muhuni fulani hivi asiyeijua dini zaidi ya mambo ya kuiga.
 
Uislamu umefanya dunia kuwa sio sehemu salama ya kuishi.Badala Mungu awapiganie watu,eti watu wanampigania Mungu,huyo Mungu ni wa kutiliwa shaka.
Umechanganya hapa ugaidi sio uislamu bali gaidi anaweza kuwa muislamu au dini yeyeto.
Hakuna gaidi anaepigania dini wote ni wahuni tu upingana na dini.
 
Hadi sasa amefahamika kwa jina moja tu la Ali ila bado naendelea kufuatilia huko msumbiji japo hali ya usalama haipo poa
Rwanda wazee wa misitu ya Congo wapo huko wataweka mambo sawa.
Soon watz watarejea mtupweshi,macimboa,nk kuchimba ruby watajirike.
Ni wahuni wachache awafiki hata 1000 vijana wa Kagame watashughulikia mwaka huu hauishi hali itakuwa poa.
 
Huyo hawezi kuwa MTanzania, shida hapo ni hiyo rasilimali ya mafuta/gesi huko Cabo delgado, na mabeberu ndio yanatuchonganisha wenyewe kwa wenyewe huku yanafyonza tu, kila mtu atumie akili zake vizuri.
Kwann wachonganishe wakichonganisha watavunaje sasa hizo raslimali.
Kwann wachonganishe hali wanawezapata raslimali yoyote nchi yeyeto kama wawekezaji bila tatizo.
 
Kwani tanzania si ndiyo kiwanda cha kupika na kuwaanda ‘magaidi’ ambao baadaye wakisha pindua serikali zao wanakuwa ma rais. Akina machel, M7, kabila, netto hawa woote waliku aga ‘magaidi’
Tza chuo cha kuandaa madikteta, madikteta wote waliopindua nchi zao wametokea wamepikwa Tza.
Ugaidi ni neno la siku hizi, zamani waliitwa wapigania UHURU.
 
Hizo silaha za kisasa wapate wapi hao wahuni silaha zao kubwa ni kufanya vitendo vya kikatili na kurekodi video na kutuma Ili kutisha watu.
Wale hawana kambi maalumu wangekuwa nayo ni rahisi kuwamaliza.
Ngumu kuwamaliza kwa haraka sababu ya kujichanganya na raia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…