Kukataa kumuuzia mteja bidhaa kisa chenji

Kukataa kumuuzia mteja bidhaa kisa chenji

SECRET AGENT

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
254
Reaction score
497
Habarini wana JF,

Juzi kuna jambo limenitafakarisha sana nmeenda dukani haya maduka ya bidhaa za rejareja ni barabaran kuna maduka kadhaa na kuna banda la chips na salon.

Nmefika kwanza nmemkuta muuzaji kijana hivi kwa kukadiria miaka 17 au 18 anachezea simu yupo bize sana ikabidi nimshtue kwa kugonga meza ndo akashtuka na kunisikiliza. Nkamwambia naomba juice ya embe ya elfu moja na maji ya mia tano, nkatoa noti ya Elfu Kumi, huwezi amini dogo alinirudishia pesa akasema sina chenchi broo kanunue kwa maduka mengine.

Nkawa kama sijamuelewa vizuri nikahisi anasema juice hamna wakati naziona kwenye shelfu, nakmuuliza unasema juisi hamna? Akasema broo chenchi sina ila juice ipo kanunue duka lingine tu.

Nlimuangalia sana yule dogo akarudi kukaa na kuendelea kuchezea simu yake. Aisee wenye maduka kuweni makin na hawa vijana wanaowauzia au kama ni ndugu yako umeweka akuuzie kuwa nae makini.

Imenishangaza sana kwa sababu alikua na uwezo wa kutoka kuomba kwa wafanyabiashara wenzake pale nje.
 
Ilinikuta bukoba hiyo tena pale center. Nina elfu5 nataka mswaki na dawa ya meno. Jamaa akanijibu katafute kwanza chenchi kwa wale boda boda ukipata njoo ununue. [emoji28][emoji28] ilibidi tu niachane na habari za kuswaki siku ile
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Aisee
 
Unajua anaweza akawa anafikilia, na wewe umekuja kununua juisi ili tu upate chenchi.

Kuna muda chenchi ni hadimu sana aise, mtu akija na 10000 kununua kitu cha 500 sometime inakata sana maini. unaweza kosa chenchi ya kumpa mtu atakae kuja kununua bidhaa yenye faida zaid ya hio juisi.
 
Ni sawa lakin kibiashara inakubomoa, unadhan naweza kuja siku nyingine kununua dukan kwako, kuna watu unampa elf kumi unahitaj bidhaa ya mia tatu anapambana mpka anapata chenchi, anafanya hivo kwa sabab ya kujenga ukarbu na mteja.
 
Mimi kukwepa usumbufu, ninge angalia na bidhaa anayochukua ina impact gani kwenye vitabu vyangu. na pia nacheki na bei ya bidhaa anayonunua.

Nisipopendezwa namwambia chenchi shida sana ndugu. kiroho safi tu!
 
[emoji23] Mzee Soma vizuri ulichokiandika af imagine una duka umemuachia dogo auze anafanya hayo mambo
We unazani ule muda kutoka dukan na kwenda kutafuta chenchi angeweza kupoteza wateja wangapi ambao wangeitaji huduma yake Kwa muda huo?
 
Unajua anaweza akawa anafikilia, na wewe umekuja kununua juisi ili tu upate chenchi.

Kuna muda chenchi ni hadimu sana aise, mtu akija na 10000 kununua kitu cha 500 sometime inakata sana maini. unaweza kosa chenchi ya kumpa mtu atakae kuja kununua bidhaa yenye faida zaid ya hio juisi.
Kama mfanyabiashara unatakiwa ujipange kuhudumia wateja wa aina zote; kwa kuwa huyo aliyekuja Leo kununua bidhaa ya 500, kesho anaweza kuja kununua bidhaa ya Bei kubwa, Kama amefurahia huduma aliyopata.

Akikosa huduma leo, kwa sababu ya kukosa change, anaweza asikanyage tena kwako kabisa!
 
Back
Top Bottom