Kukataa kumuuzia mteja bidhaa kisa chenji

Kama haujawahi kufanya biashara utaona kila mfanyabiashara ni mjinga hajui biashara!,mfano umenipa Elfu 10 unataka kitu cha 500tsh hapo faida usikute ni 50tsh,halafu sina chenchi,kwahiyo niache duka na mteja ambaye sijui kama ni mwizi ama lá kisha niende kutafuta chenchi ,halafu nikiibiwa na mteja mfanyabiashara anaonekana ni mjinga!,ama mtu uende kutafuta chenchi kisha unapoteza wateja ambao ungepata faida ya 5000tsh!
Sometimes mtu akasema sina chenji inabidi uelewe maana sisi wa fanya biashara hajupeani chenchi kiboya
 
Ni kutojitambua Kwa huyo kijana. Mimi nihsaenda choo Cha kulipia afu Nina elf kumi.
Yule mama alitafuta chenji akanirudishia 9800.
 
We unazani ule muda kutoka dukan na kwenda kutafuta chenchi angeweza kupoteza wateja wangapi ambao wangeitaji huduma yake Kwa muda huo?
si hivyo tu kuna mtejs mwingne humwamini huwezi mwacha dukani ukatafte chenchi
 
We haukuwa mteja mwaminifu na ndio maana kijana hakukuhudumia..

Ni jambo la ajabu sana kuja mtandaoni kulalamika Kwa kushindwa kuhudumiwa kwa ukosefu wa chenchi.
pengine kijana alimhisi vibaya kumwacha dukani na kwenda kutafuta chenchi
 
Biashara Zina mambo mengi mkuu, wewe Kama mteja ni ngumu Sana kufahamu changamoto za biashara.

Hapo muuzaji huwenda wateja waliopita Alisha tafuta chenchi na akakosa baadae ukatokea wewe.

Au huwenda alihofia usalama wa ofisi yake. Kwako wewe unaona umemchangia 1500 ila faida ya bidhaazote ukite ni 250.

Kutoka na kuacha ofisi kwenda kutafuta chenchi ni zoezi linalo weza chukua dk 5 Kama atakoswa maduka ya karibu yake hizo dk 5 amekuacha pekeako dukani.?



Mfano mm Kuna mteja jirani kabisa anauzaga spea za magari alikua akitaka KUFANYA miamala ananipgia smu anatoa au ananambia nimtumie kias flan Kisha nifate dukani kwake si mbali nikama mita 50 kutoka dukani kwnagu.

Nikawa nafanya hivyo lakini nikaona mbona nikama nahudumia mteja mmoja lakini wakati wa kufata pesa napitwa na wateja.? Yaan kitendo Cha kufata pesa natumia kama dk5-10 wakati mwingine huku nakuta wateja Kama 4 wamenisubiri.

Nikaona huu upuuzi nikamtema kmya kmya kila akipiga sm spokei ila alilaumu Kama wewe ulivyo laumu nikamwambia ukitaka huduma njoo Ofisini kwnagu mkuu nitakuhudumia.
 
Kawaida duka linatakiwa liwe na chenchi muda wote.
Mteja akija apewe chenchi baada ya kununua bidhaa.

Usitoe chenchi kwa wanaokuja nunua vocha za 500 kwa 5000/10000
Kweli kabisa dogo mpumbavu tu kuna muda unakuta wateja hamna yeye badala ya kutafuta chenchi anachezea simu,
 
Wafanya biashara wa bongo ni malimbukeni saana na hawana huduma nzuri kwa mteja, wanahangaika Kila siku kwa waganga na manabii feki kutafuta mvuto wa biashara lakini mteja akija humfanye afurahie huduma yako.

❌ Wewe unafungua ofisi, unsjua watakuja wateja na fedha tufauti, hujaenda chenchi, mteja anatumia huduma anatoa fedha ndio unaanza kushtuka ayaaa Sina chenchi unaanza kuzurura kuomba omba mteja anasubiri nusu saa, je! Mteja huyo atarudi tena kwako?

❌ Mteja anakuja kwako kwa huduma upo bize unaongea na simu, unalazimisha kumsikiliza hata kukata simu hutaki, huku unaongea na mteja, huku unaongea na simu, kwani ukimwomba huyo unayeongea naye ukatishe kidogo ili umsikilize mteja kwa umakini vocha zitaisha? Mteja mara nyingi anataka alone anajaliwa kuliko mtu mwingine ili siku nyingine avuke maduka yote aje apate huduma kwako.

❌Mengine unakuta yanakula huku yanamsikiliza mteja, mkono mchafu wa chakula unapokea fedha. Mteja haitaji hayo, ni wewe mtoa huduma ujue utatumia mbinu gani ili muda wote anapokuja akukute makini kumuudumia sio unaokula, unamhudumia mtoto na Wala unampa lugha mbaya au Kali, hata kama amekuja mteja kisirani wewe jishushe, ili ufanikiwe kuichukua fedha yake na kesho aje tena
 
Konda hata watu 10 watoe 10,000 kila mmoja atafanya awezalo ili apate hiyo chenji, ikiwezekana hata kwa kununua.

Hakuna watu wanathamini hela kama makonda, kwao 50 ya thamani mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda benki na laki moja kaombe chenji ya buku buku na mia tano mia tano.
 
Ilinikuta bukoba hiyo tena pale center. Nina elfu5 nataka mswaki na dawa ya meno. Jamaa akanijibu katafute kwanza chenchi kwa wale boda boda ukipata njoo ununue. [emoji28][emoji28] ilibidi tu niachane na habari za kuswaki siku ile
Yaani uliambiwa utafute wewe mwenyewe? Duh mimi nilienda kwa mama mmoja anauza samaki, nikampa 10k eti akaanza kujisemesha na mama mwenzie kwa dharau hivi eti "hee mambo ya mwisho wa mwezi hayo hawana hela ndogo" afu wanacheka, i felt bad na sijarudi tena
 
Nenda benki na laki moja kaombe chenji ya buku buku na mia tano mia tano.
Me naeza nikafungua na chenji ya 300k lakini kama siku iyo chenji ni majanga unakuta kufika sa 7- 8 mchana nikawa nateseka na kuomba chenji,

Na naeza nikafungua goli bila chenji kabisa lakini siku iyo nisinyanyuke ata mara moja kwenda kuomba chenji coz unakuta siku iyo wateja wengi wanakuja na pesa ndogo au na pesa kamili,

Sijui kama umenielewa nini namanisha!
 
Mzee hakuna kitu haitabiriki kama chenji aisee!!
 
Alafu utalisikia jitu linalalama et biashara ngumu hakuna wateja, kumbe tabia yake ya uvivu na ulegevu kazin ndio inaliponza,

Hii ipo kwa waTanzania wafanyabiashara wengi sana, na sio chenji tu bali hata wepesi wa kumuhudumia mteja watu wengi hii hawana, unamkuta mfanyabiashara anajishauwa anataka umbembeleze wakati pesa yako mwenyewe, nayeye ndie muhitaji wa pesa yako,

mi huwa nikifika madukani nataka muuzaji aoneshe uhitaji na unyenyekevu ama sivyo nitamporomoshea maneno hayo mpaka ajute kufanya biashara,

Na ndio hawa hawa hawakawii kuita wenzao wachawi wakiona wamefanikiwa, kumbe siri iko kwenye namna ya kudili na wateja, unihudumie hovyo na kwa uzembe utegemee nirudi kukuungisha? Sitorudi kamwe, na sitoishia kukupita tu bali nitawashawishi na watu wengine wakukimbie ili ukose wateja akili ikukae sawa ndipo ujuwe wapi unakosea.

Tunahitaji sana Elimu ya biashara haswa kwa hawa wakurupukaji wasiojali wateja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…