Kukataa kumuuzia mteja bidhaa kisa chenji

Kweli kabisa dogo mpumbavu tu kuna muda unakuta wateja hamna yeye badala ya kutafuta chenchi anachezea simu,
Akatafute wapi hiyo chenchi?

Na vipi kama kabla ya huyo mteja boya kuja , kuna mteja mwingine alitangulia kisha dogo akatafuta chenchi akakosa..?

Mnapoambiwa chenchi hakuna eleweni na muende kwenye maduka mengine.
 
Watu hawaelewi, wapo hapa kuropoka tu.
 
Nikunyenyekee? We fala kweli yanii, kwenye biashara hakuna swala la kunyenyekeana kiboya, lipa nikupe huduma au bidhaa upite hivi.

Boya kweli yani, we umefata bidhaa au kunyenyekewa?[emoji23].

Uniporomoshee matusi kiboya, mbona watakuokota mbele ya biashara yangu.

Labda kama ulimaanisha ikiwa utakuta mhudumu wa kike.
 
Ilinikuta bukoba hiyo tena pale center. Nina elfu5 nataka mswaki na dawa ya meno. Jamaa akanijibu katafute kwanza chenchi kwa wale boda boda ukipata njoo ununue. [emoji28][emoji28] ilibidi tu niachane na habari za kuswaki siku ile
😳🙋
 
Watu wengi humu mnaongea tu na kumlaumu dogo kwa kusema hana chenji. Ok mimi nimeuza duka la rejareja zaidi ya miaka 10 ngoja niwape uzoefu wangu kwenye chenji.

Asubuhi na mapema watu wengi wenye shida na chenji huwa wanaenda madukani unakuta mtu anatoa elf 10 ananunua kitu cha mia 3. Sasa ukihudumia watu kama hawa 5 mpaka 6 kwa asubuhi yani saa 4 inafika huna chenji kabisa na kushindwa kutoa huduma. Yani siku nzima ww kazi yako itakua kuenda kuomba chenji kwa wafanyabiashara wenzio na huwezi amini ni ngumu sababu ya ushindani. Ule muda unafunga duka kuzunguka kutafta chenji unakosa wateja.

Jinsi ya kumanage chenji ni akili kwenye biashara muda mwingine muuzaji unabidi uwe mchoyo wa chenji ata kama unazo hasa mida ya asubuhi na mchana maana ndo unaanza siku na usipokua makini siku nzima inaharibika. Utakosa mauzo makubwa kwa huruma zako. Kwenye biashara roho ngumu ni lazima iwepo
 
watu wanaongea tu humu hawajawahi kuuza duka la rejareja hasa la vitu vya nyumbani vya kila siku. hapo tatizo la huyo muuzaji ni simu ila sio chenji
 
Sijui kama wanakuelewa !!
 
Kwenye hili bandiko lako nimejifunza, pesa si kila kitu; 'barter trade' ikirudi itawatesa wengi.
Naona ulivyofadhaika una hela na hujahudumiwa, na muuzaji haoni umuhimu wa hiyo hela.
 
[emoji2][emoji2] Uporomoshe maneno tena!!
Siku ukijifanya kichaa na ukakutana muuzaji kichaa ndo utajua hujui.
 
Kaka upo sawa kabisa hao wanaongea tu kwa sababu hawajui, mimi hapa mwenyewe nipo dukan sasa hiv tena duka langu kaja mtu na ten anataka maji ya 500 sasa sikua na chench, nimezunguka maduka yote ya jiran nikakosa mpaka nikaenda mtaa wa pili vuta picha hapo nimeacha ofis wazi nazunguka tu kutafuta chench. Karibia dk 15 sipo nazunguka tu. Sasa hiv kila anayekuja na pesa ya kurudisha chench namwambia sina tu hakuna namna.
 
Hichi kinauma sana,kuna hawa wamama wa kwenye stand ukiwaona wanavyohangaika na chench ili apate hyo mia 6 ya maji alaf niende dukani kwa mtu nitake juice ya 3.5k aninyime naumia sana,
 
Tusichokijua:[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Kuhusu kuchezea simu tatizo hilo , ila kuhusu chenji unaweza kumlaumu bure , kuna siku mzunguko unakuwa mbaya kila anayekuja ni elfu kumi, unaomba mpaka unachoka , saa nyingine wengine hawakupi chenji kiroho mbaya, nipo dukani naelewa how inakuwa , inafika sehemu huna namna kwa sababu ya chenji
 
Kweli kuna siku mzunguko unakuwa kila anayekuja ana elfu kumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…