Elections 2015 Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

Elections 2015 Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

Pasco


Najiuliza;
Yaliyotokea Kenya yanaweza kutokea Tanzania?
Daniel arp Moi alimpiga panga Makamu wake, Emilio Mwai Kibaki, akamteua Uhuru Kenyatta.
Mwai Kibaki akajiuliza; kulikoni?
Akajiengua KANU, akawaachia Moi na Kenyatta chama chao..
Akaunganisha nguvu na wapinzani,na wakawashinda Rais Moi, Kenyatta na KANU kwenye sanduku la kura.
Hali hiyo yaweza kuja Tanzania?
Edward Ngoyai Lowassa aungane na UKAWA kuiangusha CCM?
HAKIKA, UTABIRI WA BABA WA TAIFA UTAKUWA UMETIMIA


Lowassa Hana chake. Aliwaaminisha kuwa ndiye anayependwa, wakati alikuwa tu mgawaji wa fedha kupitia mtandao wake kujijenga na kudanganya wananchi. UKAWA siamini kama wako tayari na nitawashangaa kumpokea. Hivi huyu alifanya nini cha maana miaka 8 iliyopita baada ya kuuzira uPM?
 
Kwani Rais Lazima awe Lowasa? kama mlikula pesa zake au mliahidiwa kuwa wasemaji wa Ikulu imekula kwenu
 
Pasco ungepumzika for now
sioni kama una make sense anymore
kila ulichotuambia huko nyuma kimeenda the opposite
labda sasa ungenyamaza kwanza.......ni kama vile nyinyi wapambe wa mgombea
mna kiu na urais kuliko mgombea mwenyewe


Moja ya njia za ku-cope na shock ni kupitia kipindi cha delusion. Mpe nafasi, delusions zitaisha,mara atakapoona uchaguzi umefika na mgombea wa CCM sio Lowassa, maana bado anaamini kuna provision ya Lowassa kuingizwa kuwa mgombea wa CCM huko mbele.

Huko alikopiga biti atahamia Ukawa, wameshatangaza mgombea wao tayari ni Dr.Slaa, kwa hili UKAWA wanastahili pongezi, kujiepusha na vishawishi.

Sasa bwana Zitto, atakuwa katega antenna anasubiri kuwa courted.

more dramas.

Otherwise imefikia hatua jamaa a-wave the white flag and calls it quits. sema kama waliomzunguka ndio kina Kingunge, Nchimbi na Kimbisa, si ajabu wanamwambia usiwe na wasiwasi, Mkutano mkuu utalazimisha jina lako,JK atavuliwa uenyekiti, na wewe utakuwa mwenyekiti na mgombea wetu kwa kipindi cha mpito!!
 
Wanabodi,

CC ya CCM, imefanya kazi yake, imelikata jina la kipenzi cha wengi, Edward Ngoyai Lowassa!.

Jee kukatwa huku ndio mwisho wa ile safari ya matumaini, au ndio mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini, kwa kipenzi cha watu, kuanza rasmi safari ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa kuipeleka rasmi CCM kaburini?

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema, upinzani wa kweli, utatoka CCM. Jee hiki ndio kipindi cha upinzani huu?

Kwa miaka 50 sasa, Watanzania tumelogwa na jinamizi la CCM kiasi cha kuamini mgombea wa CCM ndie automatically atakuwa rais wa Tanzania!. Wanaopiga kura sio CCM bali ni Watanzania!. Kama Lowassa ndie chaguo la watu, CCM wakaamua kumkata, jee sisi ambao ndio watu, tumchukue Lowassa, kupitia chama kingine chochote tumuingize ikulu?

Jee Lowassa tuliombatiza jina la mwamba, ataliishi hilo jina la mwamba kwa kuonyesha umwamba wake kwa kutokubali kuchinjwa na kufanywa mbuzi wa shughuli, au lile jina la mwamba, tulimpachika tuu, ila in reality kumbe sii mwamba lolote wala chochote, bali ni kichuguu tuu?

Mimi bado ni muumini wa andiko hili lisemalo "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!", jee Watanzania tuendelee kuwatumainia hawa waashi wa CCM kuamua hatma yetu na taifa letu, au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?

Nauliza tena, jee huu ndio mwisho wa safari, au mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini kwanza kwa kuingoa CCM na kuikomboa Tanzania?

Pasco!



Lowasa atulie tu, alimsaidia JK mwaka 2005 sawa ni kweli na JK nae akampa uwaziri mkuu waongoze pamoja waondoke pamoja alafu wawaachie wengine ikifika 2015. Yeye lowasa uongozi ukamshinda sasa hana wa kumlaumu kwa kukatwa maana alikuwa hana moral authority ya kuwa raisi wa nchi hata chembe na CCM hilo imeliona.
 
Sina shaka Edo ni mwanasias wa kiungwana. Maamuzi ya chama yasimvunjie heshima yake wa uungwana uliopitiliza kwa Watz.
 
Tumetumia gharama kubwa sana kwa takribani miaka mitano tukiwa tumewekeza kwenye mbio za urais. Watu wengi wamefaidi pesa zetu kwa njia mbali mbali kama za safari kutuomba tugombee, nauli, posh, vipeperushi, tshirts, magari na posho kwa timu yetu. Sasa tumekatwa huku tukiwa tumepoteza mabilioni yetu. Tutarudishaje hayo mapesa yetu? Tunaomba basi kila aliyepata mgao arudishe basi angalau nusu ya walichopewa tupunguze hasara. Tunawaombeni jamani maana tuko katika msiba mzito hata matanga yake hayajulikani yatakwisha lini! Tunaomba maombi yenu katika kipindi hiki kigumu
Kazi ya kichwa si kuotesha nywele pekee bali ata uwezo wa kufi kili...
 
halafu Pasco ungejua huyo lowasa hana hata habari wala wazo kichwani mwake linalofanan na haya.....yule mzee muoga sana hawezi kuhama
 
Last edited by a moderator:
muda simrefu ntarudisha au kuichoma kadi ya chama changu CCM...muda simrefu ntatoa mustakabali wa uanachama wangu..Asante Kikwete kwa kumaliza muhula wako vibaya kuliko raisi yoyote..utatukanwa na kudharililishwa zaidi ya ulivyo mfanyia Mkapa
 
Wakati mwingine ni bora kukaa kimya..Lowassa alikuwa chaguo la wachumia tumbo, watumwa wa mali walopanda mbegu za magugu katika shamba la ngano na kuishi kwa matumaini - HOPE ya kwamba ONE day YES mbegu hizo zitaota baina yake na Ngano bila kugunduliwa. Wakasahau ya kwamba magugu kusubiriwa kwanza yakaota pamoja na ngano, kwa sababu huwezi ng'oa miche ya magugu pekee unaweza kung'oa hata miche ya ngano safi. Hivyo husubiria yakaota kisha kupaririwa na kuchomwa moto, watu wakavuna ngano safi na kuiweka Ghalani..

Katika mambo yote alowahi kufanya JK atakumbukwa zaidi kwa hili, na Heko CC ya CCM kwa kufanya maamuzi sahihi. Kusema kweli sitojali tena nani baina yao atakuwa rais wa JMT maadam sio Lowassa..
 
Kinachokusumbua wewe ni nini sasa?
Khaa!! Kwani wewe unaonaje? Au na wewe umepanic? Kulikuwa hakuna namna nyingine zaidi ya KUKATWA TU
A%20S%20wink.gif
 
Back
Top Bottom