Kukomesha wizi wa kura wa NAPE, kwanini tusipige kura kwa utaratibu wa kujipanga nyuma ya mgombea

Huko ndiko watachezea wanavyotaka...easily manipulated
You will leave a electronic trail. However good you are you can not do it without leaving your footprint. Then how because manual hand counting have been manipulated since 1995.
 
makes sense
 
Kwa teknolojia ya mawasiliano ilivyokuwa inawezekana kabisa kupiga kura eg jumamosi na usiku huo huo au kesho yake jumapili, tukawa tumejuwa matokeo ya urais ya nchi nzima.
 
Unataka kuturudisha nyuma enzi za Moi? Moi ndiye alifanya hivi. Kweli wakenya wamapitia misukosuko mingi. Hii system ina madhara makubwa sana.
Yes Kenye waliwahi pitia njia hii. Ipi isiyokuwa na madhara? Mpaka sasa tuko kwenye madhara ya system hii hii ya sasa.
 
Yes Kenye waliwahi pitia njia hii. Ipi isiyokuwa na madhara? Mpaka sasa tuko kwenye madhara ya system hii hii ya sasa.
Labda ya kupigia kura kanisani, msikitini na mahekalu ya Wahindi😁
 
dah, aisee umewaza mbali, ila kama ingekuwa hivyo, kuna chama fulani cha mbogamboga kingetoa machozi.
 
Yes Kenye waliwahi pitia njia hii. Ipi isiyokuwa na madhara? Mpaka sasa tuko kwenye madhara ya system hii hii ya sasa.
Madhara ya kura za siri ni ya kujitakia lakini madhara ya kuunga mlolongo ni ya lazima. 1. Mgombea anapata urahisi wa kuhonga na kuhakikisha mhongwaji amempigia kura. 2. Utaleta visasi baada ya kura. 3. Watu hawatakuwa huru kuchagua mtu wamtakaye. 4. Upigaji kura utakuwa wa vurugu na mgumu sana kwani itabidi wapigaji wakusanyike sehemu moja kwa muda uliopingwa na ukichelewa kidogo imekua kwako.
 
uko sahihi kwa kila neno. lakini tunalinganisha pros and cons za systems mbali mbali.
 
Mleta mada hilo wazo sidhani kuwa ni feasible kuna vituo vina Wapiga kura mamilioni unaongelea kura za udiwani na viongozi serikali za mitaa huongelei uchaguzi wa uraisi na ubunge uraisi na ubunge haiwezekani
 
CCM hawakubali hili
 
Ujui kura zina ibiwa namna gani na tume ya uchaguzi pamoja na ccm...icho ulicho pendekeza hakuna kitu kitasaidia...ccm na tume ya uchaguzi wana chapa kura nyingi kisha wanatia tiki kwenye kisanduku cha mgombea wao kisha wanagawia makada wa chama chao cha ccm ..kinacho fanyika kada mmoja anakuwa na kura kama 4 tayari zimesha tikiwa mtu wao anapo enda kupiga kura anachukua karatasi za kura na kutia tiki kisha kwenye kudumbukiza kwenye sanduku la kura anatoa na zile 4 alizo zificha na kutumbukiza na ile aliyo jaza mwenyewe. Hivyo ivyo ulivyo pendekeza wewe ni bure maana wana ccm watakuwa na kura feki na kutumbukia kwenye sanduku la mgombea wao
 
Dar es salaam wapiga kura wakijipanga nyuma ya mgombea msitari utafika kigoma
Unawaambia Dar wajipange nyuma Ya Samia .Huo msitari utafika kigoma

Jiji lina watu inaingia milioni 6 uwaambie wajipange nyuma ya mgombea
Hata sasaivi tunajipanga nyuma ya mgombea, hebu litazame vizuri zoezi la upigaji kura kwa makini.
 
Hiyo yote hiyo inafahamika. Utaratibu huu mpya una masharti yake ikiwa ni pamoja ni kuwa Unainyanyua juu karatasi ya kura moja mawakala wa wagombea wengine waione waione na si kutumbukiza tu wakati umeshika lundo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…