Kukoroma Dawa yake nini? Nafikiria kumuacha mchumba wangu sababu hii

Kukoroma Dawa yake nini? Nafikiria kumuacha mchumba wangu sababu hii

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
2,254
Reaction score
5,161
Huyu dada ni mzuri na nina enjoy sana kuwa naye. Shida kuu ni moja. ANAKOROMA USIKU. Silali kwa kweli.

Mimi mtu akikoroma siwezi pata usingizi hata iweje. Nmeshalala naye zaidi ya mara 20. Usiku anakoroma vibaya sana. Hata nimwamshe nimlaze vipi haipiti dk anakoroma.

Sometime naweza msemesha akajibu ila sekunde 30 nyingi anarudia kukoroma. Naombeni mnisaidie kama kuna dawa ya tatizo hili. Sababu otherwise naona itakuwa ngumu mimi kuwa nalala naye.

Maana kiukweli huwa nikishtuka nikakuta anakoroma ndo silali tena. Nakwazika, nakereka mpaka mwisho. Siwezi pata usingizi kabisa.

Je, nifanyeje? Of course ana mwili. sijui kama ni kigezo kuwa ni unene....but mbona nmesha date sana wenye maumbo namba 8 na hawakoromi? Why yeye?
 
Wanawake wanatuvumilia mengi sana sisi wanaume.

Sisi wanaume tuna matatizo mengi zaidi ya hayo,uchafu,kuvuruga vitu chumbani,kunuka mdogo kutokana na masigara,pombe ugoro,kufungulia miredio usiku,kunuka mapua,vingi sana
 
Wanawake wanatuvumilia mengi sana sisi wanaume.

Sisi wanaume tuna matatizo mengi zaidi ya hayo,uchafu,kuvuruga vitu chumbani,kunuka mdogo kutokana na masigara,pombe ugoro,kufungulia miredio usiku,kunuka mapua,vingi sana
Aisee umemaliza mkuu.
Kama kuna watu wanavumilia mengi basi wanawake. Imagine jitu linavuta sigara, haogi, ana kitambi kilo 100, mchafu mchafu meno ya njano ila mwanamke anaishi naye kiroho safi.

Jamaa atulie tu na mrembo
 
Ikiwezekana nipe mchumba wako nilale naye kwa mwezi mmoja,nimsikie na kumchunguza kwa kina kwa nini anakoroma baada ya hapo nampa tiba kutokana na tatizo lake.
Karibu PM.
 
Kumpenda mtu maana yake ni kumvumilia na kutafuta suluhisho juu ya changamoto zenu..........
Hekima ikimjia pengine ataelewa maana pana ya maisha. Wahenga walisema -hujafa hujaumbika- hivyo haimaanishi kwamba mguu uliompendea nao mwanamke mpaka kufikia hatua ya kumuoa una garantee ya kuuona milele-pengine waweza kukatika kwa ajali. Swali la msingi, je, baada ya mguu wa mwenza wake kukatika atamwacha? 😁 😁 😁 kwenye maisha chochote chawezekana.
 
Mie niliishi na kumpenda sana binti alikua naakoroma, alikua anajamba sana, alikua na maradhi maradhi. Sikuwahi kufikiria kumuacha. Nimekuja kumuacha kwa kuwa mchoyo wa mchezo basi!
Na ilikua pini hasa.
Maisha ni zaidi ya tunavyoyaona na kuyachukulia, pengine mwandishi hajui kwamba yeye pengine ni kilema,mgonjwa au mwenye matatizo mtarajiwa. Je, atajisikiaje jamii ikimtenga kutokana na hali yake?
 
Back
Top Bottom