Kukosea kupiga simu kwanini iwe kwa watu wa kabila moja?

hata wanaosumbua kwa kupiga simu huduma kwa wateja kwenye mitandao ya simu yote ni wasukuma....wanapiga simu customer care hadi usiku wa manane ili wakusalimie tu muhudumu....[emoji16]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
🤣🤣🤣sina majibu
 
Ni kweli, wakifuatiwa na wamasai kwa mbali
 

Na wanakupigia kwa kujiamini kweli kweli...utasikie ubhebhe
 
Hao watu wasumbufu sana halafu ni wagumu sana kuelewa mtu unamwambia umekosea lakini waapi anarudia tena mara nyingi huwa navua koti la ustaarabu na kuvaa la matusi.
Nikigunduaga kuwa amekosea...najitambulisha...mimi ni afande Glenn kituo cha...huwa wanakata simu fasta🤣🤣🤣
 
Kweli kabisa yaani !
 
Nakazia [emoji419]

Ukikosea tarakimu kwenye namba uliyokusudia kuipigia basi... atapokea mtu wa usukumani 90%

Ukiwa na namba ambayo hujaitumia siku nyingi siku ukiipigia tu... utapokelewa na mtu wa kanda ya ziwa 95%

Ukiona namba ngeni tu inakuletea stori tofauti (unakuta hawezi Kiswahili kabisa au hawezi vizuri, anakutaja kwa jina ambalo hata hulijui, anakuuliza swali au anakupa taarifa ambayo huelewi imeanzia wapi inaishia wapi na wakati mwingine anakushutumu umeiba namba ya mtu aliyekusudia kumpigia na anakukomalia kabisa anakwambia mbona hii namba nawasiliana naye kila siku- akimaanisha hajakosea namba)... hii kwa 99.9% huwa ni WASUKUMA

Nadhani ni kutokana na wingi wao... ni kama vile Wanaijeria kwa Africa au Wachina na Wahindi kwa dunia nzima

Angalia mitandaoni utakuta hao watu watatu wamejaa sana kila sehemu. Kwenye WhatsApp ukiona namba ya nchi ya kigeni tu basi ni mnaijeria (tena mara nyingi matapeli). Mitandao mingi, applications na videos nyingi mitandaoni (YouTube, Facebook, Twitter, na kadhalika) zinazofundisha maswala mbali mbali hususani ya kiteknolojia, vichekesho na mautundu mbali mbali ni za wachina na wahindi wakifuatiwa na Wanaijeria
 
[emoji38][emoji38][emoji38] ni kweli kabisa,namba yangu ya Airtel haipiti siku tatu bila kupokea simu ya msukuma au mmasai.
Hili la airtel kuna ukweli maana chuoni ilibidi nibadili namba yangu fulani ya airtel kwa kadhia hii enzi za HAKATWI MTU (nilikuwa kila siku napigiwa na wasukuma na hawanielewi hata nikiwaelewesha)

Nilipobadilisha namba nikawa sipati idadi kubwa kama ile halafu nilipohamia huku airtel haishiki kwahiyo nikawa kwa kiasi kikubwa sikumbani nao tena

Kipindi kile mpaka nabadili namba ingekuwa ndo sasahivi labda wangepigwa sana hela na masela wangu maana nilikuwa nawashirikisha wadau kwenye usumbufu ninaopata.

Nakumbuka mmama mmoja alikuwa kila siku ananiita "kaka Saidi" basi akipiga anasema nimefanana hadi sauti na huyo kaka yake halafu anasema wakati mwingine anampata kaka yake kwa namba hiyo hiyo wanaongea wakati mwingine ananipata mimi basi ikawa tumezoeana kabisa
 
Kwa nn uwe ni wewe tu?

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu walininga balaa.. kila wakipiga simu unasikia Jofureeee kinehee. Nawaambia mm sio jofuree umekosea. Unasikia Hiiiiiii kwani wewe nani[emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Simple iko hivi lain unayotumia huna hatimiliki nayo kuna msukuma alikua anatumia sasa ngosha huyo akaacha kuitumia ndio ukapewa wewe kwa hiyo ndugu zake kina ngosha watakusumbua sanaa sababu wanajua line ni ya ngosha mwenzako najipigia tu vitoto vya chuo cha amazon kila siku. Vinapiga simu maana kuna mwalimu wao alikua anatumia line hioo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…