Kukosekana kwa intaneti: Kebo moja ya intaneti ilikatwa mapema Jumapili katika Mji wa bandari wa Afrika wa Durban, je ni hujuma?

Kukosekana kwa intaneti: Kebo moja ya intaneti ilikatwa mapema Jumapili katika Mji wa bandari wa Afrika wa Durban, je ni hujuma?

Mwambie siku nyingine awe anauliza kwanza...
Wanavyo kaza fuvu sasa mait wa bongo zero,sifuri maneno kibao, wakati wanawachagulia watoto wako course za it hawajui huu ni wito kama vile uchungaji au udocta ukija kusoma ilimradi mjomba kaniambia it inapesa ndio hao wanatuharibia sifa
 
Kwanini watanzania huko kwenye masomo ya Sayansi huwa mnasoma nini ?

Lini bara la Afrika litakuwa na uwezo wa kuzalisha yenyewe huduma ya internet bila kutegemea huduma kutoka kwa mzungu ?
Huduma ya internet haizalishwi, huunganishwa.
Lazima kuungana na wengine.
 
Sio kazi ambayo kila mtu anaeweza ifanya ni makampuni machache yana uwezo wa kufanya hiyo shughuli duniani.

Pili ugumu wa kazi unategemea kina cha bahari. Halafu kuna kusubiri meli iliyo free ije kufanya hiyo kazi ya haraka (muda mwingi hizo meli zipo booked) na kama kina kirefu kazi ya kukata na kutandika line nyingine inafanywa na ‘remote operated vehicles’ ni complicated operation.

Ndio maana kwenye hiyo habari ya bbc imesema kuna makampuni yameanza kuamia kwenye subsea cable zinazotokea Europe sasa kuama ni rahisi, kuamisha data za mashirika ni shughuli nyingine ambayo inachukua muda.

Wako hatua gani sijui zaidi ya maelezo ya habari.
Acha uongo wewe
Kwamba hizi tower based telecommunications systems na undersea cable networks ni reliable na zina coverage kuliko satelite ?
Unajua unachoandika wewe ?
Unajua speed ya data transmission Kwa starlink satellite ?
Unajua coverage ya starlink satellite network ?
Unajua reliability yake ?
Unajua comparison ya gharama ya kutandaza huduma ya hizo fiber optic networks na telecommunications towers Vs gharama za kutandaza huduma kwa satellite ?
Au hujui satelite moja ya starlink inaweza toa huduma na reliable coverage kwa zaidi ya nusu ya Afrika ?
Unajua Afrika jinsi ilivyo na remote places ambazo ni cost forbidding kutandaza huo ushuzi wa hayo manyaya na milingoti ?
Wakati yangeweza kufikiwa na wireless network kwa satelite more cost efficient na reliably ?

Fanya research kabla ya kuandika na kupotosha mambo
 
Unakuja kujiandikia vitu kutoka kichwani kwako halafu unataka kuwapa watu kazi ya kufanya research ambayo ungeweza fanya mwenyewe unadhani kila mtu anajiandikia mambo kama wewe.

Source ya mada ni article hapo juu kwa kiingereza.

Ndani ya hiyo BBC article mwisho kuna podcast BBC wameongea na mkurugenzi wa ‘Orange Marinę’ moja ya kampuni zinazotandaza sea cables na kufanya repairs. Kaenda mbele zaidi kuelezea tofauti ya cable na satelitę na kwanini 99% ya dunia inatumia cable.

IMG_7395.jpeg

Hao Tele-Geography ndio leading researchers duniani kwenye maswala ya telecommunication hata mashirika makubwa ya habari wanatumia sources zao. Wanakwambia cable reliable na ina uwezo mkubwa kushinda satellite.

CNN ukisoma hiyo article wanakwambia 99% ya mtandao ni underwater cable pamoja na changamoto za kukatika. Source yao Tele-Geography (tells hao jamaa wanavyo heshimika kama credible source).

The Economist wanakwambia kitu hiko hiko sea cables 99% ya mtandao wa dunia. Ndio maana huyo mzungu aliekuwa kwenye BBC podcast akaitwa mtaalamu sio mtu anaejiropokea tu.

Kama Tanzania inataka kuweka satellite waweke who cares nchi yenyewe ina viongozi wavivu kama wewe hata kujifunza dunia inavyozunguka hamtaki unataka hiyo kazi wafanye wengine kwenye dunia ya leo ambayo information ni bure.
 
Watumiaji wa intaneti nchini Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa intaneti huku watoa huduma kote Afrika Mashariki wakikiri kumekuwa na tatizo.

View attachment 2989668

Wamesema wanajitahidi kurekebisha tatizo hilo.

Huduma hiyo ilikumbwa na hitilafu katika nyaya za chini ya bahari zinazounganisha eneo hilo na dunia nzima kupitia Afrika Kusini, mtaalam wa sekta hiyo Ben Roberts aliambia BBC.

Hali kama hiyo ilishuhudiwa katika sehemu za Magharibi na Kusini mwa Afrika mwezi Machi.

Cloudflare Radar, ambayo inafuatilia uunganishaji wa intaneti, imesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi na trafiki kushuka hadi asilimia 30 ya viwango vinavyotarajiwa.

Gazeti la Citizen la Tanzania lilieleza kilichotokea kama "kuzimwa kwa mtandao ambao kumeathiri njia kuu za mtandao".

Safaricom, pia nchini Kenya, ilisema "inakabiliwa na changamoto". Airtel Uganda imesema inafahamu kuhusu "huduma ya mtandao ya mara kwa mara".

Na MTN Rwanda ilisema kulikuwa na "suala la uharibifu wa uhusiano wa kimataifa". Malawi, Msumbiji na Madagascar pia zimeathirika kulingana na Cloudflare Radar.

Bw Roberts, kutoka kampuni ya pan-Africa ya Liquid Intelligent Technologies, alisema kuwa amethibitisha kuwa kebo moja inayopitia kando ya pwani ya Afrika Mashariki, inayojulikana kama Eassy, ilikuwa imekatwa mapema Jumapili katika Mji wa bandari wa Afrika wa Durban.

Kebo nyingine pia ilikatwa. Alipuuzilia mbali uwezekano kwamba huenda ni hujuma na uongeza kuha hali kama hiyo wakati mwingine hutokea kwa bahati mbaya.

Kebo zingine zinazounganisha Afrika Mashariki na Ulaya pia zinapatikana na hatua kwa hatua huduma inapaswa kuboreshwa kwani data inapitishwa tena.

Lakini kwa vile makampuni mengi makubwa yana vituo vya data nchini Afrika Kusini uharibifu wa kiungo muhimu ambacho Eassy hutoa ulikuwa na athari kubwa.

Chanzo: BBC
kwahiyo mnafikiri itakuba bifu kati ya yanga na sundown bado linaendelea? kwanini tusitafute mbadala wa hizi mambo?
 
Wanavyo kaza fuvu sasa mait wa bongo zero,sifuri maneno kibao, wakati wanawachagulia watoto wako course za it hawajui huu ni wito kama vile uchungaji au udocta ukija kusoma ilimradi mjomba kaniambia it inapesa ndio hao wanatuharibia sifa
Yani cha tu, wabongo kazi kwelikweli 😂 😂
 
Kwanini watanzania huko kwenye masomo ya Sayansi huwa mnasoma nini ?

Lini bara la Afrika litakuwa na uwezo wa kuzalisha yenyewe huduma ya internet bila kutegemea huduma kutoka kwa mzungu ?
Tatizo wamehodhi hiyo biashara, hata tuwe na hao wataalamu hatuwezi fanya iyo kitu hivyo unavyowaza Mkuu.
 
Quran imeeleza nini kuhusu kukatika hiyo cable?
2_216.gif

Qur'an 2: 216. Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.
 
Kwahiyo internet ni shari?
 
Back
Top Bottom