Kukosekana kwa maji kumenisabisha kujisaidia haja kubwa mbali na ofisi

Kukosekana kwa maji kumenisabisha kujisaidia haja kubwa mbali na ofisi

Kwa kweli kuna kipindi tulikuwa na maisha mazuri mpaka tukasahau matenki ya maji.

Sasa wale tuliopo na ofisi ambazo vyoo vyetu vya kuflash na plan za ofisi swala la tank la maji hakuna.

Kila mwanadamu lazima kutoa taka mwili. Nipo ofisini mara nasikia hali si nzuri, kwenda chooni hakuna maji na ningetumia ukatili bila maji lazima ningejulikana kuwa mimi ndio nimeingia. Ikabidi niwashe gari kwenda nyumbani kwa sababu ofisi na nyumbani si mbali kama dakika 12.

Kilichonisaidia zaidi ya hapo ningeharibu CV ya choo cha ofisi na CV za taka taka zote wangeziona
Ulienda Home kukata gogo au?
 
Ofisini dakika 12 unaenda na gari??...unalalamikia maji hakuna alafu unachangia mabadiliko ya tabia nchi kwa kutuchafulia mazingira na mafuta yako unayochoma unataka maji yatoke wapi kanyeeeee
 
Mkuu maji yote yanaishia kwenye large intestine, mzigo unashuka kwenye descending colon na kutua kwenye sigmoid colon na kugonga kwenye rectum hakuna maji huko ndo mana ukishusha mzigo huoni maji. Ukikaa mda mrefu lazima uwe mgumu tu eneo hilo maji Yanakuwa yameshanyonywa na large intestine utakojoa sana hayafiki kwenye mavi unajidanganya tu.
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ni zamu yenu sasa wanyonge na nyie mnyongwe,maana matajiri walishaishi kama mashetani sasa ni wakati wao kuenjoy... Vumilia mkuu hata mwaka haujaisha.
 
Shida yote yanini bakisha mv yako nyumbani kwako
 
Hapo ndo utaona umuhimu wa kuishi bush, au kuwa karibu na pori lolote
 
Dah!! pole sana mkuu kwa huo mgao wa maji huko mjin, pembezoni mwa ziwa huku jamaa zinaachia tu mzigo kwenye mawe na pembezon mwa ziwa, hawa jamaa wa BMU (Beach management unit) nahisi wanakula tu pesa bila kuwajibika
 
Mbona mnakuwa wakali!

Mjini kuna magari mangapi road?

Mpaka muone jamaa kuwa na gari ni bonge la issue!!

Ama anajikweza!?

Nyie jamaa mna dhiki sana
Baadhi ya watu wana akili za kimaskini sana. Yaani mtu kueleza kuwa ana gari inakuwa suala kubwa!!! Huko kwa wenzetu wanaotengeneza na walioanza kutumia magari tena yakiwa mapya siyo haya mitumba tunayotumia huku: Sasa hivi wanageukia baiskeli kwa ajili ya mazoezi. Wanatumia magari pale kwenye ulazima sana.....

Ifikie mahali tuone mtu kumiliki gari kuwa ni kitu cha kawaida sana kwa sasa.

Nimemaliza. Ukiamua kutoa povu ruksa......
 
Back
Top Bottom