Kuku wangu 1 anataga mayai 3-4 ndani ya masaa24!

Kuku wangu 1 anataga mayai 3-4 ndani ya masaa24!

Habari za uzima Wana jf🙏

Kwa heshima kubwa Sana nimekuja kwenu hapa.

Pamoja na kwamba hapa Kuna utani na mizaha ya hapa na pale
Naomba tuiweke kando
Tujadiri hili.

Mimi ni mfugaji mzoefu na Nina uzoefu kweli hasa kwenye kuku.

Kwa siku za Hivi karibu kuku wangu amenifanya niwaze sana maana sijawahi ona kuku ndani ya masaa24 umekuwa kawaida sana kutaga mayai3 na siku nyingine 4!

Naelewa ya kwamba process ya kutengezeka Kwa yai Moja hutumia masaa24.

Lkn Kwa kuku huyu imekuwa tofauti. Asipotaga mayai 3 basi kesho yake mchana ata Taga yai kubwa sana kama hapo kwenye picha.

Ipo Hivi Kila siku usiku anataga mayai 2-3 na mchana anataga yai 1 Yale ya usiku mara zote yanakuwa tepetepe kama yanvyooneka kwenye picha.

Je hii imekaaje ?
Wataalamau wa mifugo karibuni sana

Kuku huyu ni sasso anafugwa kienyeji simpi madawa Wala madini kama DCP nk simpi inshort anaishi kienyeji 100%

Karibuni
Atakua changamoto huyo
 
Kwa kua hayo ni maajabu, tunaomba uje nae 88 huyo kuku na bango kubwa likisema kuku anae taga mayai 3 kwa siku.

Lazima ushinde taji la maonesho bora na huyo kuku tumnunue kwa dola
 
Back
Top Bottom