Bado ni mapema sana ndugu, Kuku huanza kutaga wiki ya 20-24, ambao kiwastani ni miezi mitano hadi sita.
Nimefanya hiyo biashara japo zamani kidogo na vifaranga nilikuwa nachukua interchick, wastani wa kuku kutaga ni miezi sita na mpaka kufikia wa saba hadi nane wanakuwa wameshachanganya sana, endelea kuwalisha kwa kiwango stahiki huku pia ukiwapa na majani ya kutosha kama inawezekana.
Egg boost nadhani ungewapa baada ya kuanza kutaga, nadhani si vizuri kuwapa Egg boost kabla ya kuanza kutanga japo ni kwa uzoefu wangu tu na sio kitaalamu.