Uchaguzi 2020 Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!

Uchaguzi 2020 Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!

Mayala naamini tukiwa na tume huru ya uchaguzi matakeo yatakuwa haya 1..chama cha upinzani kitashika hatamu 2. vyama vya upinzani vita sambaratika
 
Haha hata wewe mkuu Paskali?Kweli halitasalia jiwe juu ya jiwe.
masoud.jpg
kipanya.jpg
kipanyaa.jpg
 
Ila Magufuli anapendwa jamani, halafu ni mchapakazi. Kweli,mwakani hamna haja ya uchaguzi,atapita tu bila kupingwa.
 
Samahani Mkuu

1. Ushindi Wa Kishindo Walikuwa Wanashindana Na Nani? Refa Wao, Sheria Zao, Mpira Wao, Uwanja Wao, Walnzi Wao, Mashabiki Pia Wao Kila Kitu Chao Hadi Ratiba.

2. Ushindi wa 99.9% Kwenye Unaoitwa Uchaguzi.... Mbona Maeneo Zaidi Ya 90% Hakukuwa Na Uchaguzi? Hii Asilimia Umeipataje Mzee?

3. Wanaweza Kutumia Wingi Wao Kubadili Katiba Kufuta Sheria Kanuni Na Taratibu Zinazoruhusu Vyama Vingi. Nadhani Hii Ni Rahisi Zaidi Kuliko Kuhamia Dodoma.

4. Kuhusu Kukubalika Na Demokrasia Tafadhali Rejea Hotuba Ya Obama Kuhusu Demokrasia Ambapo Mshindi Anapata Kura Zaidi Ya Asilimia 90 Na Sababu Zake
 
Halafu Paskali huwa una tabia ya kuwasanifu ccm chini ya Magufuli, sio kwamba hawajui unawachora. Ngoja uone watakavyo changia kwenye huu uzi.
 
Ata angekua Nyerere au Mkapa asingeweza kupata hizo kura..
Saddam aliwai kupata 100%
Hitler huyu ndo usimeme.
Bashir aliwai kupata hizo hizo
Gaddafi alipata 99.8%
2020 JPM lazma apate 100%
 
Braza'ngu Pascal Mayalla ujue hapa jukwaani una heshima kubwa sana. Lakini kwa makala zako hizi za kikuda zinakushushia hadhi na kuonekana ni kama wale njaa kali wa lumumba.

Naomba unisaidie kaka, kuna uchaguzi ulifanyika tarehe 24 ya huu mwezi? Kama kilichofanyika wewe unaona kuwa ni uchaguzi na tena unatoa pongezi kwa washindi, basi naanza kuwa na mashaka na wewe. Kama si msukumo wa mkuno wa njaa ya tumbo, basi unaanza kupoteza utimamu wako.

Hivi kwa uelewa wako, vyama vya upinzani kwa sasa vinashindanishwa na nani? Ccm au serekali?
Unaanza kuwa au umeshakuwa mtu wa hovyo. Si kwa kujipendekeza kwako huko.

Njaa mbaya sana.
 
Paskali kwa kweli sikupendi . nakuchukuia sana kwa namna ya uandishi wako. Wewe ni mtu mwenye weledi wa mambo lakni unakuwa mpumbavu kwa kusema uwongo. Hivyo hujui figisu iliyoteka kwenye mchakato wa uchafuzi wa serikali za mitaa? ndo uipongeze CCM kwa sifa zote hizo. Call a spade , a spade not a hoe.
 
Wanabodi,

…. hongera sana CCM, Hongera Rais Magufuli, Hongera Watanzania kuikubali sana CCM, kumkubali Rais Magufuli.

Watanzania wangapi wapi waliopiga kura? Ni watanzania wangapi waliopiga kula?

…. ila ni kwa ushindi wa mezani, watu hawakupiga kura baada ya timu pinzani kuweka mpira kwapani, ….Wasiotawala Ndiyo waliweka mpira kwapani au chama dola??? .....sasa sijui kama kule kutopiga kura kuchagua nako ndiko kukubalika kwenyewe lakini maadam kwa matokeo ya mwisho mshindi ni CCM, then CCM imekubalika. Paschali nawe umeshakuwa karatasi nyepesi za maliwato..
 
Paskali ancheka na kivuli chake baada ya kupata cnhan'gaaa na mshiko pembeni
HATA WANA WA ISRAEL WAKATI WANA MKATAA MUNGU, WALIJIONA WAKO SAHIHI NA BAADHI YAO WALIKUWA NA MAWOZO KAMA YAKO. Na hayo ndo yalikuwa maombi yako watanzania. Kuwa kikwete ni dhaifu tunataka rais mkali na ......
1 Samweli 8:1-18
[1]Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli.
[2]Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba.
[3]Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu.
[4]Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;
[5]wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.
[6]Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba BWANA.
[7]BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.
[8]Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe.
[9]Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.
[10]Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya BWANA.
[11]Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.
[12]Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.
[13]Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji.
[14]Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake.
[15]Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake.
[16]Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng’ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe.
[17]Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake.
[18]Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; BWANA asiwajibu siku ile.
 
Tumeshaaminishwa inapendwa sana na Hakuna kipindi ambacho TZ Imeendelea kuliko hiki.

Wapinzani nategemea wasuse, na hivyo hata hiyo 2% ni Kura zilizoharibika.


Kuhusu Mabeberu kuingilia kati, Sitegemei maana nimegundua wako bize na mambo mengi yanayotikisa amani za dunia huku kwetu ishu za uchaguzi ni vitu vidogovidogo kwao. Wakijitahidi saana walaaandika barua.


Kutabiri ni bure wakuu, msiniponde na vyupa. Natumia mbinu za kipaskali za Trending
 
Kama Mbowe atashida bora na Ccm ishinde hata kwa 100% Mbowe anaupa upinzani wakati mgumu sana kujitetea nda ndiye atauzika.
kama anagombea tena, atakuwa ni pandikizi la CCM.
Maana ataneutralize mioyo ya watu wengi wenye kupenda upinzani hivyo kutanua goli la Ushindi wa CCM
 
Tumeshaaminishwa inapendwa sana na Hakuna kipindi ambacho TZ Imeendelea kuliko hiki.

Wapinzani nategemea wasuse, na hivyo hata hiyo 2% ni Kura zilizoharibika.


Kuhusu Mabeberu kuingilia kati, Sitegemei maana nimegundua wako bize na mambo mengi yanayotikisa amani za dunia huku kwetu ishu za uchaguzi ni vitu vidogovidogo kwao. Wakijitahidi saana walaaandika barua.


Kutabiri ni bure wakuu, msiniponde na vyupa. Natumia mbinu za kipaskali za Trending
Ukijitoa JF ndo inakuwaje kwani...
 
Back
Top Bottom