Kukurupuka katika usajili kwa Simba na Yanga ni kiashiria kuwa tuna safari ndefu sana

Kukurupuka katika usajili kwa Simba na Yanga ni kiashiria kuwa tuna safari ndefu sana

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Usiku huu nilianza kuona tetesi za usajili wa Chikwende!

Kama ni kweli, hiki ni Kielelezo kingine cha kukosa weledi katika menejimenti ya Soka!

Inawezekana Rais alikuwa sahihi aliposema Tatizo la doka la Tanzania ni Simba na Yanga!

Katika hiki kinachoitwa uwekekezaji katika hizi timu mbili, unajuliza inakuwaje kunakosekana weledi katika menejimenti ya Soka!

Hivi Simba walikuwa na Mpango wa kusajili ktk dirisha dogo, walitaka kusajili kwa malengo gani? Walijua wanamsajili nani?

Huyu Chikwende so wamemjua juzi tu? Somewhere something is wrong!

Ukiondoa Afika kusini na DRC, pengine Angola Tanzania ndio Kuna pesa za kuokota kwa wanasoka!

Hebu muangalie Sarpong, Calinyo' Mugalu, Balya, Yikpe wanatofauti gani na Watz?

Leo hii Ligi yetu imejaa Warundi! Mmakocha na wachezaji, kweli?

Mo na kina GSM wanajua kuwa wanachofanya haakina faida kwa sokala Tanzania Ila wao wmesoma upepo wanapiga hela!

Bila wadau kuamka na kuangalia huu Utopolo wa Soka letu ,tutaendelea kutambiana u-Simba na u-Yanga Basi!
 
Mchezaji ukiifunga tu Simba au Yanga wanakusajili.

Kama hakuna kabisa recruitment professionals.

Diogo Jota kabla ya kusajiliwa Liverpool alitazamwa na kufuatiliwa miaka miwili.

Sisi mchezaji anatazamwa mechi moja tu anasajiliwa.
 
Mbali na hilo juzi nimesikitika sana team captain simba na yanga wote sio watanzania. Yani raha ya simba na yanga ilikuwa zamani.

Hata ukiwa mzee unasimulia mwaka 2021 tuliwafunga simba mapinduzi cup inaleta uhalisia sasa sijui media zetu huko baadae zitakuwa zinaenda drc au ghana au rwanda kuhoji wachezaji?

Kiufupi tanzania tujipange sana maana timu inakuwa na wageni wengi kama tegemeo kuliko wazawa.
 
Viongozi wengi wa hivyo vilabu ni CCM anzia TFF mpaka unakokujua wewe hawataki mjadili haki zenu juu ya maendeleo ya nchi wao wanataka mjadili huo uhuni wa Simba na Yanga huku wao wakiendelea Kula na kusaza kama unaona mbali unawezagundua hilo lakini kama kufikiri vizuri basi utabaki kuwa oyaoya.
 
Ukiondoa Afika kusini na DRC,pengine Angola Tanzania ndio Kuna pesa za kuokota kwa wanasoka! Hebu muangalie Sarpong,Calinyo' Mugalu,Balya,Yikpe wanatofauti gani na Watz?
Yaani na Bwalya unataka kusema hastahili kuwapo Simba? Hapo hata sitakuelewa. Mtanzania gani ambaye hayupo Simba unayemfananisha na Bwalya ili asajiliwe kama mbadala?
 
Viongozi wengi wa hivyo vilabu ni ccm anzia TFF mpaka unakokujua wewe hawataki mjadili haki zenu juu ya maendeleo ya nchi wao wanataka mjadili huo uhuni wa Simba na Yanga huku wao wakiendelea Kula na kusaza kama unaona mbali unawezagundua hilo lakini kama kufikiri vizuri basi utabaki kuwa oyaoya
Kama ninakuelewa kwa mbali hivi, yaani ni kama sasa kinachoendelea kule Tocha au?
 
Mbali na hilo juzi nimesikitika sana team captain simba na yanga wote sio watanzania. Yani raha ya simba na yanga ilikuwa zamani.

Hata ukiwa mzee unasimulia mwaka 2021 tuliwafunga simba mapinduzi cup inaleta uhalisia sasa sijui media zetu huko baadae zitakuwa zinaenda drc au ghana au rwanda kuhoji wachezaji?

Kiufupi tanzania tujipange sana maana timu inakuwa na wageni wengi kama tegemeo kuliko wazawa.
Aliyekwambia lazima captain wa timu awe mzawa nani?

Auba ni mwingereza? Messi ni mspain? Mechina watford captain wa Man U alikuwa Mctominay ambae sio Muingereza.

Hebu elekezeni lawama zinazostahili, sehem sahihi.
 
Kwanini mnapenda kuangalia sana ulaya wamefanya nini? Msiwe jamii ya kuiga kila kitu. mimi nazungumzia ladha ya mpira nilioufahamu na sasa.
 
kwa nini mnapenda kuangalia sana ulaya wamefanya nini? msiwe jamii ya kuiga kila kitu. mimi nazungumzia ladha ya mpira nilioufahamu na sasa.
Huo mpira haujaufahamu peke yako, hata sisi tumekuwa tukiufatilia.

Hebu niambie kuna kasoro gani kepteni akiwa sio mzawa, ladha inapungua au? Je ni kipi kigezo cha mtu kuwa kepteni
 
Mbali na hilo juzi nimesikitika sana team captain simba na yanga wote sio watanzania. Yani raha ya simba na yanga ilikuwa zamani...
Wewe sio mwanamichezo kabisa. Lengo moja la michezo ni kuunganisha watu pasi na kujali ni wapi wametokea. Najua unaona ni uzalendo ila si kila sehemu ni ya kufanya uzalendo ni kama ilivyo katika kuvaa viatu ni kitu kizuri ila si busara kupanda navyo kitandani.
 
Bongo POLITICS everywhere. Sisi ni kama tunafanya maigizo, hakuna mipango yenye kuleta tija badae.

Wanaofaidi kwenye sekta ya michezo ni viongozi na wafanyabiashara kuliko wanamichezo wenyewe.
 
Kama ni kweli Chikwende kasajiliwa Yanga basi subirini performance yake uwanjani kisha judgement zifanyike
 
Bongo POLITICS everywhere. Sisi ni kama tunafanya maigizo, hakuna mipango yenye kuleta tija badae.

Wanaofaidi kwenye sekta ya michezo ni viongozi na wafanyabiashara kuliko wanamichezo wenyewe.
Simba na Yanga ni miradi ya watu.

Kuna wanaopiga pesa pale na kuna wanatumia hizo Clubs kujenga jina na baadaye kujitafutia ulaji kwenye siasa: Aden Rage, Abbas, Manara, Mrisho Gambo et al
 
Waambie Simba SC wenzako. Yanga SC tulishatoka huko. Tunasajili kwa malengo na ufundi.
 
Mbali na hilo juzi nimesikitika sana team captain simba na yanga wote sio watanzania. Yani raha ya simba na yanga ilikuwa zamani.

Hata ukiwa mzee unasimulia mwaka 2021 tuliwafunga simba mapinduzi cup inaleta uhalisia sasa sijui media zetu huko baadae zitakuwa zinaenda drc au ghana au rwanda kuhoji wachezaji?

Kiufupi tanzania tujipange sana maana timu inakuwa na wageni wengi kama tegemeo kuliko wazawa.

Mkuu hili la unahodha nalo pia ni lazima awe mtanzania ?
Anyways kapteni wa Simba ni Mtanzania mwenzetu John Bocco. Sasa sioni msingi wa kwamba mtu ambaye ni mtanzania ndio lazima awe nahodha kwenye mechi inayoihusu Simba au Yanga.
 
Back
Top Bottom