Kula dagaa kuna faida kuliko kula samaki wakubwa

Kula dagaa kuna faida kuliko kula samaki wakubwa

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Tofauti na samaki wakubwa, mtu anayekula dagaa anakula hadi mifupa yake. Sasa mifupa ina madini mengi sana ya calcium. Madini hayo ndiyo hujenga mifupa ya viumbe wote.

Binadamu anayekula dagaa anakuwa na mifupa imara sana kuliko alaye samaki wakubwa, hasa kwa watoto ambao wanakua. Kwa kweli haitakiwi mlo ukose dagaa.
 
Watu watakuona umetoa pumba na wengine watakukejeli kuwa umeishiwa lakini ukweli uko pale pale dagaa kwa afya ni bora kuliko samaki wa kawaida.
Uzuri tumbo huwa halibagui kinchoingia ikifikia mahali vimeng'enyo vinataka kuchukua fungu lake la mwili haviangalii umekula pilau au umekula viazi manumbu au umekula dagaa au samaki wakubwa
Ndo maana kanda ya ziwa ni vigumu sana kupata magonjwa ya tezi la shingo na ukosefu damu au anemia sababu ya dagaa.
Dagaa zina madini mengi mno ya chuma na calcium
 
Asante kwa ushauri ila huku Canada dagaa ni chakula cha matajiri ni bei juu sana, kuku tu ndo bei che hata ukiwa homeless unaimudu
Hebu mshaurini mcanada mwenzenu aliyekuja huku asituzingue na madharau ya nchi yetu
 
Back
Top Bottom