Kula dagaa kuna faida kuliko kula samaki wakubwa

Tofauti na samaki wakubwa, mtu anayekula dagaa anakula hadi mifupa yake. Sasa mifupa ina madini mengi sana ya calcium. Madini hayo ndiyo hujenga mifupa ya viumbe wote.

Binadamu anayekula dagaa anakuwa na mifupa imara sana kuliko alaye samaki wakubwa, hasa kwa watoto ambao wanakua. Kwa kweli haitakiwi mlo ukose dagaa.
Hatukatai ni kweli. Lakini kama huna yakununulia samaki mkubwa na unayo fungu 2 za dagaa si ndio hapo unaambukia kula dagaa kila wakati!
Asante Kwa kutupa fundisho.
Hata asiye na ya nyama ananunua matumbo!.
 
Mboga yangu pendwa na ambayo hainikinai. Naweza kula mwaka mzima kwemyw wali aj ugali hususani wakichanganywa na Bamia au Nyanya chungu huku kuna limao na pilipili kwa mbaliiii au wawekwe nazi tosha. Sikuwa najua hizo faida za kula na mifupa yake. Ngoj nimwambie mama Manka kesho aandae.
 
Tofauti na samaki wakubwa, mtu anayekula dagaa anakula hadi mifupa yake. Sasa mifupa ina madini mengi sana ya calcium. Madini hayo ndiyo hujenga mifupa ya viumbe wote.

Binadamu anayekula dagaa anakuwa na mifupa imara sana kuliko alaye samaki wakubwa, hasa kwa watoto ambao wanakua. Kwa kweli haitakiwi mlo ukose dagaa.
Dagaa wapi

Wa ziwa victoria, Tanganyika,Nyassa au wa kilwa ?
 
Tofauti na samaki wakubwa, mtu anayekula dagaa anakula hadi mifupa yake. Sasa mifupa ina madini mengi sana ya calcium. Madini hayo ndiyo hujenga mifupa ya viumbe wote.

Binadamu anayekula dagaa anakuwa na mifupa imara sana kuliko alaye samaki wakubwa, hasa kwa watoto ambao wanakua. Kwa kweli haitakiwi mlo ukose dagaa.
Kuna jamaa mwingine nilimsikia akisema, ukila nyama ni vipande viwili tu vinavyojenga protini ya mwili. Vingine ni makapi tu. Hii njaa itatufunua mambo mengi
 
Kwamba dagaa ni bora kuliko pande la Sato[emoji1][emoji1]

Nb: ni umasikini tuu unatufanya tule dagaa
 
Back
Top Bottom