Pringles my favorite snack. Imenikumbusha miaka ya nyuma wakati nipo sekondari nilikuwa na cousin wangu ( R.I.P) tunazurura town bahati tukakutana na rafiki yake mama akatupeleka min market moja akauliza niwanunuie nini Mimi nikasema Pringles cousin wangu akaulizwa na yeye anataka nini akajibu kama hicho hicho. Basi akalipia tukaondoka kufika nje couzin akaniuliza kwani hizi ni nini?? Nilicheka mno kumbe alikuwa hata hajawahi ziona nilitamani kumdanganya ili aniachie ila nikamwelekeza alivyoonja alishangaa kwa nguvu mbona vitamu hivi na toka Siku hiyo akawa mpenzi sana wa pringles.