Kula kula ukiendekeza inakua kama bangi, hii kitu vimenipa uraibu mbaya mno, nina collection ya makopo yake ndani

Kula kula ukiendekeza inakua kama bangi, hii kitu vimenipa uraibu mbaya mno, nina collection ya makopo yake ndani

Hii kitu ina addction moja mbaya sana

unanunua kopo la elf 6 ni kubwa unapanga ule kwa siku 3 lakini ukionja kipande tu nakuapia unaweza kufuta lote mda huo huo, ukionja ni ngumu sana kujizuia kuingiza mkono kuchota nyingine.

Pringles zipo za aina nyingi nyingi sana, binafsi zilizonibamba ni hot n spicy pamoja na bbq.

View attachment 2986627
View attachment 2986629
Haaahaa😊😊 Mimi nanunuaga@8000
 
Kweli maisha tumetofautiana sana....... wakati wengine hiyo 6,000/= tunakula siku 2.....kuna mtu ananunua udambwi udambwi wa kuchangamsha mdomo Tu...........

Ngoja tuendelee kupiga gahawa mchana upite......
1002138812.jpg
 
Hii kitu ina addction moja mbaya sana

unanunua kopo kubwa la elf 6 (kwengine hadi elf 8), unapanga ule kwa siku 3 lakini ukionja kipande tu nakuapia unaweza kufuta lote mda huo huo, ukionja ni ngumu sana kujizuia kuingiza mkono kuchota nyingine.

Pringles zipo za aina nyingi sana kwa ladha, binafsi iliyonibamba ni hot n spicy


View attachment 2986639
Mwanaume unapendeleaje vitu vitamutamu umekuwa mdada?
 
Pringles my favorite snack. Imenikumbusha miaka ya nyuma wakati nipo sekondari nilikuwa na cousin wangu ( R.I.P) tunazurura town bahati tukakutana na rafiki yake mama akatupeleka min market moja akauliza niwanunuie nini Mimi nikasema Pringles cousin wangu akaulizwa na yeye anataka nini akajibu kama hicho hicho. Basi akalipia tukaondoka kufika nje couzin akaniuliza kwani hizi ni nini?? Nilicheka mno kumbe alikuwa hata hajawahi ziona nilitamani kumdanganya ili aniachie ila nikamwelekeza alivyoonja alishangaa kwa nguvu mbona vitamu hivi na toka Siku hiyo akawa mpenzi sana wa pringles.
Watoto wa Upanga bana dah 😁
 
Kitu cha buku mtaani kinauzwa elfu 8 kwenye supermarkets zaidi kitakuwaje maarufu?😂 Hivi unajua hio hela familia inakula mlo kamili kabisa huku uswazi kwetu.
Hio 6000 ni mlo wa wiki kabisa na familia inafurahi sana michicha na sukumawiki kwa wingi nyama mpaka Sikukuu ukitaka nyama kuna mishkaki ya hasara Miguu ya kuku na utumbo wa kuku bila kusahau Pweza na Ngisi bei nafuu 200/300 unajichana unavyotaka mswahili mswahili tu
 
Back
Top Bottom