Kula kwa jasho ni kuhangaika kutafuta riziki sio lazima utoe jasho la mwili au ufanye kazi za nguvu ya mwili

Kula kwa jasho ni kuhangaika kutafuta riziki sio lazima utoe jasho la mwili au ufanye kazi za nguvu ya mwili

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
KULA KWA JASHO NI KUHANGAIKA KUTAFUTA RIZIKI SIO LAZIMA UTOE JASHO LA MWILI AU UFANYE KAZI ZA NGUVU YA MWILI

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kuna kasumba ambayo inatesa baadhi ya vijana wa kiume ndani ya jamii huku wakinukuu maandiko ya kwenye Biblia Kuwa "Mwanaume atakula kwa jasho"

Wengi hujikuta wakifanya kazi za nguvu na kutoa jasho bila akili kwa kisingizio cha kula kwa jasho. Alafu mwisho wa siku matokeo huwa madogo au hakuna kabisa

Elewa, kula kwa jasho haimaanishi kuwa ili upate riziki lazima jasho la mwili likutoke. Sio lazima.

Kinachozungumziwa hapo ni kuwa mwanaume lazima uhangaike na kutafuta riziki.
Kabla ya laana hiyo mwanadamu hakuwa anahangaika kupata riziki. Kazi yake ilikuwa kufanya kazi na uhakika wa kupata úlikuwepo.

Lakini baada ya laana
Inamlazimu kutumia jitihada ili kupata riziki aliyowekewa.

Kuihangaisha akili yako pia ni sehemu ya kuvuja jasho.

Ndio maana siku hizi kazi nyingi sio za kuvuja jasho la mwili lakini lazima uhangaike.
Hata zile zilizokuwa zinatoa watu jasho la mwili siku hizi zinarahisishwa, mfano Kilimo, siku hizi kuna zana nyingi za kilimo kama Matrekta, vifaa vya kuvuna, kupukuchua n.k.

Kuhangaisha akili ndio jasho lililoongelewa hapo.
Kwa sababu zifuatazo

1. Binadamu ndiye kiumbe mwenye akili na utashi kuliko viumbe wengine duniani.
Mungu asingeweza kumwambia binadamu atumie nguvu za mwili ilhali nguvu hizo hana.

Watu wote walioelewa andiko hilo kwa namna ya nguvu mwili walijikuta wakiwa maskini na vibarua kwa wale wenye Akili.

2. Tunda lililoliwa lilikuwa la ujuzi wa mema na mabaya.
Na adhabu ililenga ujuzi wa maarifa
Yaani pasipo maarifa huwezi kuishi maisha mazuri.

Kwa leo taikon acha apumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Leo, Dar es salaam
 
Hivi ukisimamia ukucha si unatoa jasho, vijana wa Dayoo pigeni kazi kama isemavyo Biblia.
 
Jasho litoke mkuu, hata kama kwa kufanya mazoezi basi😂

Ukivunja utaratibu wa Mungu subiria balaa tu, mara sukari presha na matatizo kibao tatizo ni kutokutoka hata kajasho kidogo
 
Jasho litoke mkuu, hata kama kwa kufanya mazoezi basi😂

Ukivunja utaratibu wa Mungu subiria balaa tu, mara sukari presha na matatizo kibao tatizo ni kutokutoka hata kajasho kidogo

Diet inatosha kabisa
Mtu anayekula Balanced Diet hana haja ya mazoezi
 
Contextual... shughuli za kiuchumi za kipindi hilo neno linaandikwa zilikuwa zinahusisha kutoa jasho tu.

Si ndio?
 
Contextual... shughuli za kiuchumi za kipindi hilo neno linaandikwa zilikuwa zinahusisha kutoa jasho tu.

Si ndio?

Hapàna
Shughuli kama ufugaji aliyokuwa amefanya Habili mtoto wa Adamu ya kuchunga mifugo sio shughuli ya kutumia nguvu na kutoa jasho. Ni shughuli ya kuongoza (kuchunga)

Kula kwa jasho ilikuwa adhabu iliyolenga kuhangaika, kutokupata kitu kirahisi, kutumia jitihada n.k.
 
Back
Top Bottom