KULA SANA BATA HATA KUKU WOTE LAKINI KAMWE USIWASAHAU NDUGU ZAKO.

Jamni ndugu jau muelewe hili
Marafiki tunaweza kuchagua na kuchange as much as we want lakini ndugu huwezi kuchange.

Mungu akishakupa hao ndio ndugu zako huwezi kuchagua ndugu wengine. Pamoja na madhaifu yao kama mimi na wewe tusivyo wakamilifu basi tusiwaache.

Siku ukipata shida tutawatafuta ndugu zako.
 
bado hujakutana na ndugu vichomi, utajuta hata kumkaribisha kwako. Kama una ndugu kwa maana ya ndugu hongera sana....ni hayo tu
Hakuna mkamilifu. Hata marafiki tunakutana nao vichomi hivyo hivyo lakini bado ndugu zetu ni wa muhimu sana.

Bata unakula na marafiki arafu ukiumwa ndugu zako ndio watakaolala hospitali kukuuguza.
 
Ndugu wanafiki sana
Wanafiki mno
Yaani anatamani akuone una teseka hivi hivi aiseee
Hata marafiki wapo wanafiki pia. Wanaotamani kuona hatufanikiwi kuwazidi wao wapo wengi. Mungu amekupa hao watakuwa ndugu zako milele. Huwezi kusema nimehama ukoo sasa nipo ukoo wa kina Kimario wakati wewe ni kina milanzi wa Mtwara.

Usiwasahau ndugu zako
 
Ujakutana na majanga ya ndugu..
Bora mtu baki
 
Bora rafiki mnafiki ila sio ndgu..
Ndugu anapokufanya ubaya hua inauma sana mkuu
 
Kwangu huu ni ujumbe bora sana👏🏽.Tunajisahau sana mkuuu inafika mahara ndugu zako unawaona ni mapimbi tu kisa umewazidi kipato unasahau kwamba damu ni nzito kuliko maji utawatukana utawaonyesha jeuri ila siku una tatizo ndo hao watakao kutawaza unapojinyea na wala hawatakuacha watakomaa na ww mpaka mwishl.Jamani mali isitufanye tudharau ndugu zetu .mkuu shukrani sana kwa kutukumbusha kupenda ndugu.
 
Hakuna mkamilifu. Hata marafiki tunakutana nao vichomi hivyo hivyo lakini bado ndugu zetu ni wa muhimu sana.

Bata unakula na marafiki arafu ukiumwa ndugu zako ndio watakaolala hospitali kukuuguza.
ila sijaongelea marafik mm, nimeongelea ndugu,
 
Tenda wema nenda zako. Kama unaweza kuwatendea wema watu baki haitakuwa sawa ukiwaacha ndugu zako.
 
Hapana mkuu, si kwa ndg wote.


Kuna ndg wanaroho mbaya kupitilia, wanatamani kusikia habari zako zikiwa.

#Hana kitu.(masikini)

#Marehemu.


#Anaumwa hoi.


#Kwa sasa ni kichaa.


Kama umebahatika kuwa na ndg wema shukuru sana.


Binafsi mpaka kufikia hapa, nimepata sapoti kubwa sana kutoka kwa watu baki tena hasa nilipopatwa na changamoto kwa muda mrefu (maradhi)


Nadhani Mungu amenionesha kuwa hao ndio ndg wa ukweli maana walinifaa kwa dhiki na mpaka ktk raha (kazi) koneksheni bado imetoka kwa wao.
 
Ujakutana na majanga ya ndugu..
Bora mtu baki
Kuna ndugu kweli wanamajanga wanaweza kukuchukia kisa unawasema wabadilike hata kukuroga tu mlingane hilo lipo.Ila sizani kama kwenye ukoo wote utakosa hata wawili wanao jielewa washike mkono.Wachanga,Wakinga kwa nn wanaweza????Sometime sisi wengine tunapenda uungu mtu yaan unataka uabudiwe.
 
kuna muda ndugu zako ni marafiki zako......ndugu hawa wa damu nao walikufungia vioo wakati unajitafuta ulivyojipata tu ghafla vioo vimeshushwa.
 
[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Mi ndgu zangu kiukweli ni watu wa kukatishana tamaa tuu licha ya ku a hakuna mwenye navyo vingi ila tuu wanamaneno ya hovyo sana
 
Mimi ktk maisha yangu ntamsaidia MTU yeyote ilimradi anastahili Masada wangu na uwezo ninao.
 
Hivyo hoja ya kusema kuna siku utapata msaada inakufa.

Wema ni hiyari sio lazima.
Atakuja kuwa too disappointed kwa kufanya mambo huku akiamini atapata Masada

Huyu hajui jamii zilizo na huo mfumo Kama wapemba , waarabu ,wahindi.

Hao ndo wenye utamaduni wao Ila waswahili kusaidiana niki-maslahi zaidi na nature huwa haimlipi MTU wa hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…