KULA SANA BATA HATA KUKU WOTE LAKINI KAMWE USIWASAHAU NDUGU ZAKO.

KULA SANA BATA HATA KUKU WOTE LAKINI KAMWE USIWASAHAU NDUGU ZAKO.

Kwangu huu ni ujumbe bora sana👏🏽.Tunajisahau sana mkuuu inafika mahara ndugu zako unawaona ni mapimbi tu kisa umewazidi kipato unasahau kwamba damu ni nzito kuliko maji utawatukana utawaonyesha jeuri ila siku una tatizo ndo hao watakao kutawaza unapojinyea na wala hawatakuacha watakomaa na ww mpaka mwishl.Jamani mali isitufanye tudharau ndugu zetu .mkuu shukrani sana kwa kutukumbusha kupenda ndugu.
Nashukuru sana ndugu yangu, hapa wengi wanasema vibaya ndugu zao lakini sio sawa. Ndugu ni watu muhimu sana
 
KULA SANA BATA HATA KUKU WOTE LAKINI KAMWE USIWASAHAU NDUGU ZAKO.

"Kama MUNGU amekujalia uwezo mzuri wa kiuchumi, weka nguvu kwa ndugu zako pia.

Usiwasahau ndugu zako kwasababu ipo siku utawahitaji na usipowahitaji wewe basi tutawahitaji sisi kwaajili yako.

Siku ukiumwa au kupata matatizo yoyote hatutawatafuta rafiki zako bali tutawatafuta ndugu zako ili wajue jinsi ya kukusaidia kama ndugu yao.

Hakikisha kwenye mafanikio yako hauwafingii vioo ndugu zako, hao ni watu muhimu sana kwako hatakama leo unawaona kama hawana umuhimu kwenye mafanikio yako.

Yamkini MUNGU amekuinua wewe kwaajili yao. Yaani wamebeba baraka zako bila wewe mwenyewe kujua.

Tuwapende na kuwajali ndugu zetu. Usiwavimbie na kuwaona kama hawajielewi kwasababu hawajafanikiwa kama wewe.

Tumeshashuhudia watu wengi sana wakipatwa na tatizo au wakiwa wamepoteza maisha kwenye mazingira tatanishi chakwanza huwa tunauliza ndugu zake wapo wapi?

So kula sana bata hata kuku wote lakini kamwe usisahau ndugu zako.

Kama unakubaliana na mimi na unawajali ndugu zako gonga like, comment twende sawa."

I'm Mr George Francis
Lawyer & Contents Creator
Hayajakukuta
 
Back
Top Bottom