Kuliko Bilion 34 kujenga soko Kariakoo bora soko lihamishwe



Tutafika Insh'Allah..ukweli tuna hiyo changamoto wala hatuwezi kukata. Hii Hamidu city ni ipi? 😀😀😀
 
Hilo unalolisema angeliweza kulifanya Jiwe tu!
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Kama issue ni kuwaweka wamachinga mahali pazuri basi tuhamishe kiwanda cha urafiki na hata ile millenia business park, tujenge kariakoo kubwa ya kutisha ya ghorofa hata nne majengo makubwa kwa ajili ya wamachinga. Na tuweke miundo mbinu ya usafiri wa umma, kuingia na kutoka.

Hata mwekezaji mchina ameshajenga fremu hapo kiwandani, amewapangisha wamachinga
 
Mh!! Mbona Urafiki hatunacho tena¡?!
 

Vyote vinawezekana na ni vitu muhimu.

Soko jipya Kariakoo na miundombinu rafiki ni vizuri ijegwe. Na pia mapendekeze yako mengine yote yanaweza kufanywa kwa pamoja.
 
Mama ametoka kwenye mkutano na akapiga kelele ili pesa ya kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi itoke. Kwa picha ya Hong Kong ilivyozungukwa na msitu na miji mingine kwa waliotembelea nchi zilizoendelea, mama angefanya uamuzi wa kujenga mji mpya wenye sifa zote za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi au bonde la Muhimbili/Jangwani lingepandwa miti ili wakazi wa Dar wapate Oxygen kwa miaka ijayo la sivyo joto litaua raia.
 
Kwa sababu kuna daraja tayari, kwa nini hiyo hela wasi plan kujenga soko kubwa Kigamboni? kuna space na mji ndiyo unajengaka kwa sasa.
 
point.

Kariakoo hakuna hata sehemu ya kusema utapumzika walau unywe soda ambapo pana miti na hewa safi. kila sehemu majasho matupu.
 
Kwa sababu kuna daraja tayari, kwa nini hiyo hela wasi plan kujenga soko kubwa Kigamboni? kuna space na mji ndiyo unajengaka kwa sasa.
Yani tena siyo kigamboni tu, vitongoji vyote vilivyo pembezoni mwa jiji vingejengewa masoko makubwa kama hayo ili kuondoa msongamano katikati ya jiji hao wamachinga wasambazwe huko pembezoni mwa jiji.
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Ni kweli kabisa Tanzania hatujafikia hali ya kukataa wamachinga wasifanye biashara barabarani
 
point.

Kariakoo hakuna hata sehemu ya kusema utapumzika walau unywe soda ambapo pana miti na hewa safi. kila sehemu majasho matupu.
Shida kweli, na hiyo mijasho kwa asilimia kubwa ni ma pumzi ya watu wengine maana kila mtu anatoa carbon dioxide Na hakuna miti ya ku absorb co2 na ku release Oxygen.
 
Ya ubungo bilioni 200 ,hii itakuwa trilioni 4 tunaweza
 
Mkuu umetisha,enzi za mwalimu mzee kawawa alitaka kule gymkhana watu walime mahindi,wazee wa nchii jii bana
 
Mama bado akili imelala sana bado yuko na kichwa kizito sana katika kufanya maamuzi, sio kila dodoso analowekewa mezani anaitikia tu?

Na hili linajidhihilisha serikali ya awamu ya sita (6) ni dhaifu sana, yaani analetewa pendekezo eti soko kubwa lijengwe jangwani, tunapiga makofi na kushangilia? tumerogwa siyo bure.

Jangwani hii ambayo mvua ya saa moja ikinyeesha panajaa maji lukuki, kwa maoni yangu ni vyema Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akapatengeneza ili kumaliza tatizo la mafuriko kwanza na sio kukurupuka na kwenda kuwekeza hayo mabilioni huko.

Sitaki kuamini kama bado hajajifunza kwa kilichotokea kwenye makao ya mabasi ya mwendo kasi, mabasi mengi ya mwendokasi kila mara huaribika sababu ya mafuriko ya mara kwa mara.

Hivyo hilo soko ni vyema akapendekeza lijengwe sehemu nyingi eidha apeleke bunju ama mbagala huko.
 
Ya ubungo bilioni 200 ,hii itakuwa trilioni 4 tunaweza
Ubungo billioni 200 tulipigwa. South Africa walijenga 4 tier interchange kwa $84million, Ghana wamejenga 4tier interchange kwa $94million sis vidaraja viwili billioni mbili[emoji23]. Pale jangwani tukijenga ya kwetu kwenda faya, Magomeni, salender, karume, kinondoni studio haizidi $250 million. Ndege moja ya Dreamliner tumenunua $248 millioni tumeagiza nyingine moja $248 + $248 =$496 millioni tunabeba mizigo guangzhou sasa hv mchina mwenyewe anashangaa Dreamliner pekee la mizigo airport ni la Africa [emoji23].

Labda nikuulize wewe hapo unajiskiaje binafsi kuwa na madege mawili ya $496million au kuwa na madaraja ya yanayoungana kwenda faya, magomeni, salender, karume hadi kinondoni studio ipi itakusaidia wewe binafsi?interchange ya south Africa $84 million interchange ya Ghana $94 million
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…