Inaonekana watu wa mipango miji wamelala na viongozi wetu akili zimeganda. Nimeona leo kwamba soko la k'koo litajengwa upya kwa Billion 34, leo siyo mwaka 1970 jamani kwanini pesa zote zitumike kujenga soko tena eneo lenye tatizo la msongamano wa watu badala ya kulihamisha soko pembezoni mwa mji? Au wazanzibari wao kila kitu wanataka kiwe karibu na feri ili wakitoka Zanzibar wasipate usumbufu[emoji23]? Maana naskia tena kuna mradi mwingine wa soko la jangwani[emoji26][emoji26].
Mimi nazani tuachane na hili soko la kariakoo tena serikali ingetumia opportunity hii kujenga mradi wa kuwezesha kariakoo kupumua kwa kubomoa lile soko na kupanda miti eneo lile na kutengeneza city park yenye bustani na benchi za watu kupumzika. Itungwe sheria iundwe mamlaka ya City park Authority ya kusimamia mambo haya kwenye miji yetu ipendeze. Tuache fikra kwamba kila eneo lazima lijengwe mji ule hauna hata sehemu ya kupumzika, mtalii akienda k'koo leo hii hakuna hata sehemu ya kupumzika labda ale chips sehemu ambayo imejaa joto la moshi wa jiko la mkaa na hewa ya mafuta ya kukaanga.
Kwanini bado serikali inakaa na kuwaza kujenga jenga sehemu yenye msongamano hata parking za magari hakuna badala ya kujenga miradi ya kuboresha changamoto za mji kama kujenga jengo la parking pale kwenye soko japo mimi ningetamani pasijengwe chochote ipandwe miti tu pale mji upumue.
Leo tunataka kufanya makosa yaleyale ya kujenga mwendokasi jangwani kwa kujenga soko jingine pale la wamachinga badala ya kujenga daraja flyover la kutoka magomeni kwenda faya au interchange ya kutoka magomeni kwenda faya kwenda salender kwenda karume na kupanda miti mirefu ya misitu jangwani ili kusaidia joto la mji kupungua.
Ukizingatia eneo la jangwani ndiyo aneo peke kwenye mji wa dar es salaam lenye unapana wa kutosha ndani ya jiji lenye kutosha kujenga 4 tier interchange ambazo kwa Africa ziko mbili tuu, moja iko Ghana na nyingine iko South Africa.
Yani pale inasukwa interchange moja matata sana kono moja linaenda faya kono jingine linaenda magomeni, kono jingine linasambaa hadi salender , kono jingine linasambaa hadi mitaa ya ilala karume, kono jingine linakatiza hadi kinondoni studio au nyuma yake pale.
Hela tunazo invest kwenye mavitu yasiyo na kichwa (madege, ma dreamliner) tunaweza tukatoa kitu cha maana sana pale jangwani chenye kupunguza changamoto nyingi sana za mji na kutujengea heshima kubwa sana kama jiji.
View attachment 1999008