Zitambue tofauti hizi mpakani mwa Tanzania na Rwanda katika boda ya Rusumo:
1. Miundo mbinu upande wa Rwanda ni bora zaidi. Barabara, taa za barabarani, security cameras, majengo, fencing, furnitures nk upande wa Rwanda ni kama Ulaya.
2. Upande wa Rwanda taratibu zote katika kila idara yaani forodha, afya, polisi, immigration, usalama nk ni wazi na hakuna rushwa.
3. Waliopo kwenye eneo la serikali mpakani upande wa Rwanda ni wale tu wanaohusika kwa shughuli rasmi za hapo. Yaani wafanyakazi, mawakala wa forodha, mawakala wa bima za magari, wasafiri wavukao nk.
4. Hakuna anayeweza kuvuka kuingia Rwanda pasipo sababu wala idhini ya idara zote husika za huko yaani immigration, usalama na polisi.
5. Upande wa Rwanda wafanyakazi maisha ni kula kwa viwango vya mishahara yao.
6. Kuhusiana na Tanzania itoshe kusema huku ndiko kwenye ulaji wa urefu wa zile kamba zetu. Yaone magari ya wafanyakazi huku. Ama Kwa hakika wanalamba asali kweli kweli.
7. Eneo la serikali huku limesheni hadi wasiohusika. Kuvuka kuja Tanzania ni bwerere ambapo kama hata wapiga debe kutoka Rwanda wanajifanyia shughuli zao Tanzania kwa raha zao tumebakiza nini?
Yapo mengi ya kushangaza ila itoshe kusema kwa hakika sisi ni shamba la bibi.
Tuendelee kulea hali hizi hadi lini?