Kulikoni, mpakani na Rwanda sisi ni shamba la bibi?

Wanajua mtanzania hata avuke mpaka ni peace haendi kufanya ujambazi Kenya wa silaha anaenda tu kuburudisha nafsi na anarudi kwake Tanzania awe na passport au la sio kwamba immigration Kenya hawakuona huyo bodaboda waweza kuwa wanamjua vizuri Kenya wanamjua na aliwaonyesha sign kuwa nimebeba peaceful person ana yake ambayo sio illegal.in Kenya

Mirungi Kenya sio illegal kama Tanzania

Ila Mkenya hawezi ingia kirahisi hivyo kama wewe atakoma sababu immigration wanajua crime rate ya wakenya Tanzania iko juu mmo

Ndio maana Raisi Kagame anahangaika kudhibiti mipaka ya Rwanda ya wanyarwanda watokao na bidhaa zitokazo kwenda nje na viingiaavyo visije chafua brand ya. RWANDA ndio maana wakali mpaka wao uwe unatoka au unaingia au chochote kinaingia au kutoka

Hawataki mchezo wanataka kufanya Rwanda brand ya chochote iwe reliable

Na yuko sahihi

Point of correction - "boda hii ni one stop center". Kila nchi haizuii watu kutoka kwake kwenda upande wa pili bali kila nchi inadhibiti waingiao kwake.

Kwa mwendo wa boda hii nchi imefunguliwa zaidi ya kufunguliwa.
 
Nlienda namanga halafu nikachukua boda kanivusha upande wa kenya tukazurura weee baadae kanirudisha wala khakuna mbambamba sikua na gatepass wala paspot yaani unajiachia nia kama warombo wanavuka mpaka wakakula miraa/mirungi halafu wageuza tz wako tilalia na polisi wapo palee 😅😅😅😅

Isije kuwa Namanga ya Best Bite 😀
 
Bwege wewe 🤣🤣🤣 Namanga ya Longido, kwanza jamaa ni nimesoma A_Level Moringe Sokoine High School

Ninakazia:

"Yapo mengi ya kushangaza ila itoshe kusema kwa hakika sisi ni shamba la bibi.

Tuendelee kulea hali hizi hadi lini?"

Mwenye masikio na asikie.
 
Point of correction - "boda hii ni one stop center". Kila nchi haizuii watu kutoka kwake kwenda upande wa pili bali kila nchi inadhibiti waingiao kwake.

Kwa mwendo wa boda hii nchi imefunguliwa zaidi ya kufunguliwa.
Kwa Rwanda imeshsjijengea credibility kwa Tanzania kuwa haizalishi wakimbizi au questionable persons wa kuingia Tanzania toka Raisi Kagame ashike uongozi
Na amekuwa consistent

Hata mpaka wa Tanzania na Rwanda ungekuwa wazi upande wetu bila immigration office hiyo kazi Rwanda wangeifanya on our behalf kuogopa ku loose their credibility tuliyonayo kwao
 
Tanzania ni nchi ya kipuuzi sana mkuu. Wala usishangae kwanini watawala wameamua kuifanya nchi hii iwe shamba la bibi. Mitanzania ndivyo tulivyo.
Miinga wewe akili huna kama una chuki na Rwanda Kanye ukale
 
Zitambue tofauti hizi mpakani mwa Tanzania na Rwanda katika boda ya Rusumo:

1. Miundo mbinu upande wa Rwanda ni bora zaidi. Barabara, taa za barabarani, security cameras, majengo, fencing, furnitures nk upande wa Rwanda ni kama Ulaya.

2. Upande wa Rwanda taratibu zote katika kila idara yaani forodha, afya, polisi, immigration, usalama nk ni wazi na hakuna rushwa.

3. Waliopo kwenye eneo la serikali mpakani upande wa Rwanda ni wale tu wanaohusika kwa shughuli rasmi za hapo. Yaani wafanyakazi, mawakala wa forodha, mawakala wa bima za magari, wasafiri wavukao nk.

4. Hakuna anayeweza kuvuka kuingia Rwanda pasipo sababu wala idhini ya idara zote husika za huko yaani immigration, usalama na polisi.

5. Upande wa Rwanda wafanyakazi maisha ni kula kwa viwango vya mishahara yao.

6. Kuhusiana na Tanzania itoshe kusema huku ndiko kwenye ulaji wa urefu wa zile kamba zetu. Yaone magari ya wafanyakazi huku. Ama Kwa hakika wanalamba asali kweli kweli.

7. Eneo la serikali huku limesheni hadi wasiohusika. Kuvuka kuja Tanzania ni bwerere ambapo kama hata wapiga debe kutoka Rwanda wanajifanyia shughuli zao Tanzania kwa raha zao tumebakiza nini?

Yapo mengi ya kushangaza ila itoshe kusema kwa hakika sisi ni shamba la bibi.

Tuendelee kulea hali hizi hadi lini?
Mungu alitupa linchi likuubwa lakini akatunyima akili
 
Ukienda mtambaswala border ya TZ na Mozambique ni kinyume cha huko, pale ni ukiwa tz ndio unaona afadhali sana ila msumbiji dah..
 
PK Aliwahi kumtambia Jakaya kuwa anaweza kuendesha TZ kwa bandari ya Dar Jakaya akamjibu lami aliyojenga ukiiweka rwanda hata sebule na choo zote haienei. Alipoendelea na kiromoromo alikipata nini? Operesheni kimbunga! Alikoma!
Ndio kimekuwa cha kujivunia?

Tujikite kwenye hoja kwa mada iliyopo, sijui udogo wa Rwanda au ukubwa wa Tanzania itakuwa kama kujidanganya tu. Tuwe serious kwenye mipaka yetu
 
Kwa Rwanda imeshsjijengea credibility kwa Tanzania kuwa haizalishi wakimbizi au questionable persons wa kuingia Tanzania toka Raisi Kagame ashike uongozi
Na amekuwa consistent

Hata mpaka wa Tanzania na Rwanda ungekuwa wazi upande wetu bila immigration office hiyo kazi Rwanda wangeifanya on our behalf kuogopa ku loose their credibility tuliyonayo kwao
Ungekuwa umejirisha kuwa One Stop Border Posts (OSBP) zinafanyaje kazi usingeandika hayo:

NB: Kwenye border posts hizo illegal immigrants anadhibitiwa anakokwenda siyo anakotokea.
 
Ndio kimekuwa cha kujivunia?

Tujikite kwenye hoja kwa mada iliyopo, sijui udogo wa Rwanda au ukubwa wa Tanzania itakuwa kama kujidanganya tu. Tuwe serious kwenye mipaka yetu

Hadi tustukie M23 wamebadilisha mwelekeo ndipo tutapata akili.

Kwa mpaka huu nchi Iko wazi hadi (maadui) watakuwa wanatushangaa.
 
Hadi tusukie M23 wamebadilisha mwelekeo ndipo tutapata akili.

Kwa mpaka huu nchi Iko wazi hadi (maadui) watakuwa wanatushangaa.
Tumelala sana.

Tungekuwa serious hata wale wa Ethiopia na wasomali wasingeweza kupita kwenye mipaka yetu.
 
Du hii kali mno, mpaka wa Rwanda 🇷🇼 na Tanzania 🇹🇿 ni mpaka kweli upande wa Rwanda 🇷🇼 ila Tanzania mmmmm, huu mpaka sijawahi kufika, ila wa tunduma/nakonde unaweza kucheza bao upande wa Tanzania na kuagiza uletewe hindi la kuchoma kutoka nakonde na ukaletewa within 10mins!,tembea uone

Huu unapendeza kote ni shamba la bibi. Kunagomba inapokuwa msumeno kukata upande mmoja. Hilo tisa hayo mafyongo mengine nayo mbona shughuli?
 
Zitambue tofauti hizi mpakani mwa Tanzania na Rwanda katika boda ya Rusumo:

1. Miundo mbinu upande wa Rwanda ni bora zaidi. Barabara, taa za barabarani, security cameras, majengo, fencing, furnitures nk upande wa Rwanda ni kama Ulaya.

2. Upande wa Rwanda taratibu zote katika kila idara yaani forodha, afya, polisi, immigration, usalama nk ni wazi na hakuna rushwa.

3. Waliopo kwenye eneo la serikali mpakani upande wa Rwanda ni wale tu wanaohusika kwa shughuli rasmi za hapo. Yaani wafanyakazi, mawakala wa forodha, mawakala wa bima za magari, wasafiri wavukao nk.

4. Hakuna anayeweza kuvuka kuingia Rwanda pasipo sababu wala idhini ya idara zote husika za huko yaani immigration, usalama na polisi.

5. Upande wa Rwanda wafanyakazi maisha ni kula kwa viwango vya mishahara yao.

6. Kuhusiana na Tanzania itoshe kusema huku ndiko kwenye ulaji wa urefu wa zile kamba zetu. Yaone magari ya wafanyakazi huku. Ama Kwa hakika wanalamba asali kweli kweli.

7. Eneo la serikali huku limesheni hadi wasiohusika. Kuvuka kuja Tanzania ni bwerere ambapo kama hata wapiga debe kutoka Rwanda wanajifanyia shughuli zao Tanzania kwa raha zao tumebakiza nini?

Yapo mengi ya kushangaza ila itoshe kusema kwa hakika sisi ni shamba la bibi.

Tuendelee kulea hali hizi hadi lini?
na kule hakuna demokrasia kama yetu PK yupo madarakani kwa zaidi ya miaka 20 sasa
Maendeleo hayana chama ni eidha tuwe na kiongozi anaetanguliza masilahi ya nchi na wananchi wake ama ipatikane katiba mpya
 
Hadi tustukie M23 wamebadilisha mwelekeo ndipo tutapata akili.

Kwa mpaka huu nchi Iko wazi hadi (maadui) watakuwa wanatushangaa.
Tanzania hii au unaongea ipi

Kiongozi wa wa waasi mkuu wa kongo wa kikundi cha ADF ambacho kiliikuwa kazi yake kutandika kongo na kushambulia Museveni alikamatwa Gongo la mboto ,Dar es salaam kikundi chake kilipoua Askari wa Tanzania wa umoja wa mataifa walioko kongo akakakabidhiwa serikali ya Uganda sijui walimfanya nini ila alibebwa juu kwa juu toka Gongolamboto hadi Uganda akabidhiwa kwao kuwa mtu wenu anayewasumbua huyu hapa. Walimpata ndani ya wiki mbili tu akiwa mumiliki wa biashara kibao Dar es salaam zikiwemo guest house ,nk akiwa kafoji documents zote kupoteza kuwa traced
 
Usalama tz huwa Kama hawakuoni/hawapo,siku muhimu ikifika wanakudaka aisee Kama panzi
 
Rwanda ni kama Mkoa wa Tabora na wanaiba madini ya Kongo huwezi lingasha na linchi likuubwa kama Tz hata hivyo hakuna cha maana walichituzidi kuanzia barabara hadi majengo marefu. Acha kudanganya [emoji34][emoji34]
Ukubwa wa nchi ni excuse ya kipumbavu sana, kwa nini ukubwa tusiufanye kuwa advantage.
Unaweza ukaorodheshewa nchi kubwa zaidi ya Tanzania na zenye infrastructure nzuri sijui utatafuta excuse nyingine au la.
 
Nitajie halafu angalia na resources walizonazo
 
Back
Top Bottom