GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 4,291
- 5,786
Ni kweli!. Nilipita Rusumo tarehe 05/01/2023 kuelekea Kigali na baadae Gisenyi. Naelewa kuwa Rwanda ni nchi ndogo sana kuilinganisha na Tanzania kwenye ujenzi wa miundombinu, Lakini wenzetu linapokuja suala la ujenzi wa barabara wanasimamia kweli kweli na matokeo ni kazi iliyotukuka.
Kutoka Rusumo hadi Kigali barabara ile iko kwenye viwango vya juu sana, alama za barabarani za wima na zilizochorwa zinaonekana wazi, taa za barabarani zipo hadi Kigali. Mitaro mingi imefunikwa na cha msing zaidi ni nidhamu kwenye uendeshaji unaofuata sheria kwa kiwango kikubwa.
Kuna barabara chache sana zinazoweza kushindana na zile za Rwanda, Barabara zote zilizojengwa na Strabag zinaweza kushindana, kuna barabara moja mpya imejengwa kutoka Kabingo hadi Nduta Junction pamoja na barabara kadhaa zilizojengwa Mbeya na Tabora.....Barabara nyingi zilizojengwa siku za nyuma ni aibu tupu!.🥹
🥹