Kulikoni, mpakani na Rwanda sisi ni shamba la bibi?

Kulikoni, mpakani na Rwanda sisi ni shamba la bibi?

akili kama mtoto wa kindagati,poiti hapo ni wizi unao fanywa na maafisa wa serikali ndio maana kuna tofaoti kati ya rwanda na tz
Akili yako ni kisoda kwamfano hao wanyarwanda wakikaza wamefikia wapi kimaendeleo😅😅
 
Mtoa mada ametembelea border moja alafu anakuja na conclusion kwamba tz ni shamba lá bibi ,ni kuulize umeshawahi tembelea border ya tunduma, Nakonde what is your take on that? Maana ukienda upande wa nakonde hapaeleweki ila ukija tunduma kumependeza na watazania ndio wanafanya shughulii nyingi za uchumi upande wa Zambia hapo utasemaje? labda ni kupe somo kidogo border inakuwa nzuri kiuchumi kwa wakazi wa eneo lille pale ambapo panakuwa hakuna sheria kali za kutoka na kuingia kwa raia wa nchi zote mbili kwa baadhi ya kilometres mfano mzuri ni border ya tunduma nakonde raia wanaishi peaceful sababu ya business interaction ya raia wa nchi zote mbili mtazania akita anaenda kununua mafuta ya kupakaa upande wa Zambia na mzambia akitaka anakuja nunua mchele upande wa Tanzania .kwa upande wa border Rwanda tz kuachia warwanda kuja kufanya kazi tz hivyo ndivyo inapaswa kuwa kwa nchi pande zote kwa baadhi ya kilometres free border movement ili ku create business opportunities kwa wakazi wa maeneo hayo ya mipakani.
Unachanganya mambo kwa kuelewa nusunusu jambo husika.

Hao wakazi wa mpakani na shughuli zao ni jambo tofauti kabisa na utekelezaji wa taratibu za uvukaji mpaka.
 
Hoja sio udogo wa eneo ni umakini na ufanisi katika kusimamia majukumu uliyopewa.
Ulivyojibu ndo uhalisia wa watanzania wengi, siyo watu makini katika maeneo mengi, ujuaji mwingi na ubabaishaji ndio sifa yetu.
Alichokiandika mtoa Uzi, ni sahihi kabisa. Tumewahi kusafiri kwenda Rwanda kikanisa, ukweli sote tulishangaa, ofisi ya uhamiaji upande wa Tanzania tuliambiwa kusanyeni hati zenu na kuzikabidhi,zikagongwa zote,hakuna aliyehangaika kutazama sura ya mtu.
Tulipofika upande wa Rwanda, tuliambiwa kila mtu ashike hati yake mwenyewe, wamuone ni yeye mwenye hati hiyo.
Yanaweza kuwa ni mambo madogo,lakini yanaashiria uzembe uliokithiri kwenye maeneo mengi Tanzania.
Ukweli tunajitaji kubadilika sana.
Rwanda ni jambo la kawaida kuyaona mabomba ya maji ya chuma yamepita kando ya barabara na hakuna anayejaribu kukata eti akatengenezee mkokoteni, njoo Tanzania Sasa, vibao vya barabarani kikiwa cha chuma hakimalizi wiki.
Ukweli usiopingika bado tuna tatizo kubwa mno. Suala la kuwa wengi kuliko Rwanda siyo hoja ya msingi, pia tuna viongozi wengi na watendaji wengi zaidi ambao ni wazembe pia.
Mkuu 'mundaliku', nilitaka kupita harakaharaka katika kusoma michango iliyowekwa kwenye mada hii.

Niliposoma mstari wako wa kwanza kabisa wa mchango wako, ikanilazimu niusome tena kwa mara ya pili kabla ya kwenda mbele zaidi.

Hata hivyo, mara ya pili haikutosha, ilibidi nitulie kidogo maneno hayo yaniingie vizuri akilini.

"--- umakini na ufanisi katika kusimamia majukumu---"

Matatizo ya Tanzania yapo hapo kwenye hayo maneno machache..

Matatizo yapo kila sehemu ndani ya serikali yenyewe, viongozi wa serikali, hadi kwetu sisi wananchi wenyewe.

Kiujumla ni kama tamaduni yetu, kufanya mambo bila umakini.

Athari zake ndiyo hivi tunavyoona.

Tunajitangaza tunafungua nchi, lakini ni wazi hatuna taratibu za kudhibiti takataka zinazotokana na ufunguzi huo. Sisi hilo halituhusu!

Lakini ninaelewa, tukitaka kubadili hali hiyo tunaweza kabisa. Kwani wao Rwanda wanaweza kivipi
 
Rwanda ni kama Mkoa wa Tabora na wanaiba madini ya Kongo huwezi lingasha na linchi likuubwa kama Tz hata hivyo hakuna cha maana walichituzidi kuanzia barabara hadi majengo marefu. Acha kudanganya 😠😠
Shida huelewi concept ya mtoa mada, hata ukiwa na nyumba kubwa unahitaji usafi usiseme mwenye nyumba ndogo anafanya usafi Kwa sababu ana nyumba ndogo .usafi ni usafi tu
 
Yule bibi ili paswa hatubu kwa kauli yake ya kijinga .(kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake ) hii ni kauli ya kiongozi wa nchi dah
 
Zitambue tofauti hizi mpakani mwa Tanzania na Rwanda katika boda ya Rusumo:

1. Miundo mbinu upande wa Rwanda ni bora zaidi. Barabara, taa za barabarani, security cameras, majengo, fencing, furnitures nk upande wa Rwanda ni kama Ulaya.

2. Upande wa Rwanda taratibu zote katika kila idara yaani forodha, afya, polisi, immigration, usalama nk ni wazi na hakuna rushwa.

3. Waliopo kwenye eneo la serikali mpakani upande wa Rwanda ni wale tu wanaohusika kwa shughuli rasmi za hapo. Yaani wafanyakazi, mawakala wa forodha, mawakala wa bima za magari, wasafiri wavukao nk.

4. Hakuna anayeweza kuvuka kuingia Rwanda pasipo sababu wala idhini ya idara zote husika za huko yaani immigration, usalama na polisi.

5. Upande wa Rwanda wafanyakazi maisha ni kula kwa viwango vya mishahara yao.

6. Kuhusiana na Tanzania itoshe kusema huku ndiko kwenye ulaji wa urefu wa zile kamba zetu. Yaone magari ya wafanyakazi huku. Ama Kwa hakika wanalamba asali kweli kweli.

7. Eneo la serikali huku limesheni hadi wasiohusika. Kuvuka kuja Tanzania ni bwerere ambapo kama hata wapiga debe kutoka Rwanda wanajifanyia shughuli zao Tanzania kwa raha zao tumebakiza nini?

Yapo mengi ya kushangaza ila itoshe kusema kwa hakika sisi ni shamba la bibi.

Tuendelee kulea hali hizi hadi lini?
Usilinganishe mkoa na nchi
 
Maneno tu ya mitandaoni na chumvi nyingi! Mbona tulikuwepo na hatukuyaona.
Kwan opereshen ya kufukuza wahamiaj bongo ina athiri nn kagame
Kagame na Rwanda hawawezi kuishi hata sekunde moja! bila kuiba raslimali za nje au kutegemea nchi za nje:
Chakula asilimia 88 kinatoka either Rwanda au Tanzania. Alipogombana kidogo na Uganda alikimbilia Tz kuyajenga wapate mlo! Shamba la bibi liko kongo! jamaa anaexport mbao na madini wakati hana hata kimojawapo. JK alipotaka kukomesha M23 ndipo ugomvi ulikoanzia!
 
Usilinganishe mkoa na nchi
Jamaa hajazungumzia nchi Wala mkoa amezungumzia yanayojiri mpaki mwa Tanzania na Rwanda

Yani Rwanda wapo smart katika majukumu Yao na Tanzania ni Bora liende

Watanzania uwezo wetu wa kiutendaji na uwelewa wetu upo chini sana

Hata huu Uzi unathibitisha hilo Uzi unaongelea mpaka wa Watanzania na Rwanda wachamgiaji wengi Naona wanachangia kuhu ukubwa wa nchi ya Tanzania na Rwanda
 
Zitambue tofauti hizi mpakani mwa Tanzania na Rwanda katika boda ya Rusumo:

1. Miundo mbinu upande wa Rwanda ni bora zaidi. Barabara, taa za barabarani, security cameras, majengo, fencing, furnitures nk upande wa Rwanda ni kama Ulaya.

2. Upande wa Rwanda taratibu zote katika kila idara yaani forodha, afya, polisi, immigration, usalama nk ni wazi na hakuna rushwa.

3. Waliopo kwenye eneo la serikali mpakani upande wa Rwanda ni wale tu wanaohusika kwa shughuli rasmi za hapo. Yaani wafanyakazi, mawakala wa forodha, mawakala wa bima za magari, wasafiri wavukao nk.

4. Hakuna anayeweza kuvuka kuingia Rwanda pasipo sababu wala idhini ya idara zote husika za huko yaani immigration, usalama na polisi.

5. Upande wa Rwanda wafanyakazi maisha ni kula kwa viwango vya mishahara yao.

6. Kuhusiana na Tanzania itoshe kusema huku ndiko kwenye ulaji wa urefu wa zile kamba zetu. Yaone magari ya wafanyakazi huku. Ama Kwa hakika wanalamba asali kweli kweli.

7. Eneo la serikali huku limesheni hadi wasiohusika. Kuvuka kuja Tanzania ni bwerere ambapo kama hata wapiga debe kutoka Rwanda wanajifanyia shughuli zao Tanzania kwa raha zao tumebakiza nini?

Yapo mengi ya kushangaza ila itoshe kusema kwa hakika sisi ni shamba la bibi.

Tuendelee kulea hali hizi hadi lini?
KoTe hujo nakuacha nakupinga katika miundombinu mzee.
HAPA EAST AFRICA NA CENTRAL NI KENYA PEKEE INAYOFUANA NA SISI INTERMS OF INFRASTRUCTURE.
KWA UZURI WA VYOTE HIVYO TUNAITOA MWANZA TUU RWANDA NZIMA HAIIPATI.
AMA NAITOA KIJITONYAMA KIGAMBONI NA KIJICHI INATOSHA KUPAMBANA NA RWANDA NZIMA.
 
Back
Top Bottom