Nafikiri sio kweli. Nilisikia Zitto pia anasema kuwa asilimia 71 ya wa Tanzania hawamjui mzee Mwinyi. Nafikiri hizo statistics ni za kubumba tu. Ukifanya analysis wakati mzee Mwinyi anastafu urais mwaka 1995 mpaka Leo imeshapita miaka 29.Kwa maana hiyo,kwa mtizamo wako na mtizamo wa Zitto Kabwe kwa miaka 29 iliyopita wamezaliwa watu wengi Sana zaidi ya watu waliokuwepo miaka 29 iliyopita. Hawa watu waliokuwepo ,yaan waliokuwa wamezaliwa tayari, mwaka 1995 , yaani miaka 29 iliyopita tu assume kuwa walizaliwa kuanzia 1960.Waliozaliwa mwaka 1960 mwaka 1995 walikuwa na miaka 35 na sasa wana miaka 64.Na hata kama wengine wamekufa bado wapo wengi, kwa kuwa mtanzania wa miaka 60 ndio anastafu na ni wa kawaida tu. Waliozaliwa mwaka 1970 mwaka 1995 walikuwa na miaka 25 wakati mzee Mwinyi anastafu na sasa wana miaka 54.Hawa bado ni wabichi sana hata kama wemekufa wengine. Waliozaliwa mwaka 1980 wana miaka 44 na ni wengi tu. Nafikiri, wa Tanzania wengi wanamjua Mzee Mwinyi. Kwan waliokuwepo wakati hakiwa ni Rais ni wengi kuliko waliozaliwa baada ya yeye kustaafu.