Kulikoni vyama vya Siasa kuomba ruhusa Polisi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Sheria kuhusiana na mikutano inavitaka vyama vya siasa kutoa taarifa polisi, siyo kuomba ruhusa.

IMG_20221004_203850_913.jpg

Kuwaendekeza hawa ndugu tutajikuta mwana si wetu.

Kuheshimu sheria hakuwezi kuwa jambo la upande mmoja.
 
Unatoa taarifa polisi na polisi wataruhusu au kukataa kutokana na mtazamo wao wa kiusalama. Maana yakitoka yakutokea lazima wajibie, kutoa taarifa au kuomba ruhusa ni lugha TU lakini jambo ni kupata uhalali wa tukio
 
Tafsiri haiwezi kuwa ya upande mmoja. Kunapokuwa na utata kwenye lugha huwa kuna mahakama za kutafsiri iibidi kuwarejea wahusika waliotunga katiba kueleza walichomaanisha.

Kwa mujibu wa katiba kutoa taarifa si kuomba ruhusa.

Bila mpambano wa kudai haki zetu kikamilifu tutashuhudia mengi kutoka kwa mabwana hawa ikiwamo hata kuporwa haki za kuishi.
 
Tafsiri haiwezi ya kuwa ya upande mmoja. Kuapokuwa na utata kwenye lugha huwa kuna mahakama za za kutafsiri iibidi kuwarejea wahusika waliotunga katiba kueleza walichomaanisha.

Kwa mujibu wa katiba kutoa taarifa si kuomba ruhusa.

Bila mpambano wa kudai haki zetu kikamilifu tutashhudia mengi kutoka kwa mabwana Hawa ikiwamo hata kuporwa haki za kuishi.
Mkuu sentences zako tatu za mwisho umehitimisha vema,haki haiji in a golden 🍽, inapiganiwa sometimes kwa jasho la damu, Iran 🇮🇷 yale maandamano damu zaidi ya 80 zimeshamwagika na mapambano yanaendelea (elewa chanzo ni kwa msichana aliyekufa akiwa in a police custody),hapa tunakuja humu JF wahusika wa haki wanasoma wakiwa na vikombe vya chai, maana they now nothing will happen, tutapiga kelele then jiiiii,kila kukicha sasa vijana wengi wanakufa in police custody hakuna push back, cold ❄ case's nyingi tu na maisha yanaendelea
 
Mafanikio katika mapambano yetu yako kwenye kupigania haki zetu. Haupo mbadala kwenye haki.

Kunaingia tatizo haki zinapokuwa na standards tofauti:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote
 
Unatoa taarifa polisi na polisi wataruhusu au kukataa kutokana na mtazamo wao wa kiusalama. Maana yakitoka yakutokea lazima wajibie, kutoa taarifa au kuomba ruhusa ni lugha TU lakini jambo ni kupata uhalali wa tukio
Huo ni ushenzi mbona mikutano ya ccm inafanywa kila wakati.
 
Unatoa taarifa polisi na polisi wataruhusu au kukataa kutokana na mtazamo wao wa kiusalama. Maana yakitoka yakutokea lazima wajibie, kutoa taarifa au kuomba ruhusa ni lugha TU lakini jambo ni kupata uhalali wa tukio
Tafsiri yako ni potofu kabisa.

Kinachotakiwa ni kutoa taarifa siyo kuomba kibali. Polisi wanachotakiwa ni kutoa ulinzi. Kama kuna shida ya kupata ulinzi, Polisi watakitaarifu chama husika. Na chama husika kitaamua kuendelea na mkutano bila ulinzi wa polisi au kuahirisha mpaka watakapokuwa na uhakika wa kupata ulinzi wa Polisi.

Kama Polisi watakuwa na mashaka yoyote ya kiusalama, watashauriana na chama husika, na kisha chama hicho kitafanya maamuzi ya kuahirisha au kuendelea.

Polisi hawana mamlaka yoyote kisheria wala kikatiba ya kuruhusu au kuzuia mkurano wa cha cha siasa.
 
Ajabu na kweli upinzani umechagua kuomba ruhusa badala ya kutoa taarifa.
 
Mkuu sentences zako tatu za mwisho umehitimisha vema,haki haiji in a golden 🍽, inapiganiwa sometimes kwa jasho la damu, Iran 🇮🇷 yale maandamano damu zaidi ya 80 zimeshamwagika na mapambano yanaendelea (elewa chanzo ni kwa msichana aliyekufa akiwa in a police custody),hapa tunakuja humu JF wahusika wa haki wanasoma wakiwa na vikombe vya chai, maana they now nothing will happen, tutapiga kelele then jiiiii,kila kukicha sasa vijana wengi wanakufa in police custody hakuna push back, cold ❄ case's nyingi tu na maisha yanaendelea
Yaani ni mambo ya hovyo sn
 
Vyama vya upinzani viandae na vifanye mikutano ya hadhara,

POLISI wapewe tu taarifa, HAPANA kuomba RUHUSA, ni kinyume Cha Katiba.

Njooni ground muongee na wananchi, Nchi hii Ina utawala wa Sheria, hivyo ni HAKI kufanya mikutano ya hadhara.

Kwa mwendo huu sheria itabadilishwa itakuwa hakuna kufanya mikutano mpaka kupata ruhusa ya polisi. Kwa maana ilipokuwa kutoa taarifa tu, tulijikita kwenye kuomba ruhusa.
 
Huu ndo muda pekee muafaka wa kuiangusha CCM, hapatakuwa na fursa adhimu zaidi ya hapa.

Vyama vya siasa vianze mikutano, bila purukushani na POLICCI, haijaitwa siasa ya Kweli Bado!!!!!
 
Kwa uzoefu nilionao sijawahi ona police wakiruhusu mikutano ya vyama inayohusisha viongozi wakuu wa chama bila visingizio vya hapa na pale kwa miaka ya hivi karibuni labda nyuma sana enzi za Kikwete .

Watakubali vipi kama nasi tunaridhia wasipotoa ruhusa wasiyokuwa na mamlaka nayo?

Sasa sheria inabadilishwa Ili rasmi iwe kuwaomba ruhusa.

Wa kulaumiwa nani?
 
Back
Top Bottom