SahihiTafsiri yako ni potofu kabisa.
Kinachotakiwa ni kutoa taarifa siyo kuomba kibali. Polisi wanachotakiwa ni kutoa ulinzi. Kama kuna shida ya kupata ulinzi, Polisi watakitaarifu chama husika. Na chama husika kitaamua kuendelea na mkutano bila ulinzi wa polisi au kuahirisha mpaka watakapokuwa na uhakika wa kupata ulinzi wa Polisi.
Kama Polisi watakuwa na mashaka yoyote ya kiusalama, watashauriana na chama husika, na kisha chama hicho kitafanya maamuzi ya kuahirisha au kuendelea.
Polisi hawana mamlaka yoyote kisheria wala kikatiba ya kuruhusu au kuzuia mkurano wa cha cha siasa.