SahihiTafsiri yako ni potofu kabisa.
Kinachotakiwa ni kutoa taarifa siyo kuomba kibali. Polisi wanachotakiwa ni kutoa ulinzi. Kama kuna shida ya kupata ulinzi, Polisi watakitaarifu chama husika. Na chama husika kitaamua kuendelea na mkutano bila ulinzi wa polisi au kuahirisha mpaka watakapokuwa na uhakika wa kupata ulinzi wa Polisi.
Kama Polisi watakuwa na mashaka yoyote ya kiusalama, watashauriana na chama husika, na kisha chama hicho kitafanya maamuzi ya kuahirisha au kuendelea.
Polisi hawana mamlaka yoyote kisheria wala kikatiba ya kuruhusu au kuzuia mkurano wa cha cha siasa.
Mkandamizaji kamwe hawezi kuridhia hayo. Yeye maumivu yanuonezi hayamgusi hivyo haoini umuhimu.Sijui yale maridhiano yametufikisha wapi?
Basi ACT waombe mkutano Mbeya au Iringa
fullcup, hii tafsiri unaitoa wapi ndugu yangu. Watu wenye mawazo na mtazamo kama nyie ni hatari kwa hili taifa kuliko mnavyoweza kufikiria kwa ujinga wenu.Unatoa taarifa polisi na polisi wataruhusu au kukataa kutokana na mtazamo wao wa kiusalama. Maana yakitoka yakutokea lazima wajibie, kutoa taarifa au kuomba ruhusa ni lugha TU lakini jambo ni kupata uhalali wa tukio
fullcup, hii tafsiri unaitoa wapi ndugu yangu. Watu wenye mawazo na mtazamo kama nyie ni hatari kwa hili taifa kuliko mnavyoweza kufikiria kwa ujinga wenu.
Kwa hapa Tanzania badala ya kuwalinda wananchi na mali zao, polisi Tanzania mara nyingi ndio huwa chanzo cha vurugu na uharibifu wa mali katika hii mikutano.
Hali hii ni matokeo ya chama tawala kuamini polisi wapo kuwalinda wanachama wao na viongozi wao kwa kuhakikisha mabaya yao hayaanikwi kwa wananchi.