Kulikuwa na jaribio la Mapinduzi Chadema, Sasa wavamia Uchaguzi!

Mtunzi wa hekaya za Hutaki unaacha.Ameanza tena kazi ya utunzi wa hekaya za kumpinga Lissu.Ni chawa pro max wa mwenyekiti Mbowe ambaye anaishi mjini kwa kulelewa na Mbowe.Sasa anafanya juhudi kubwa ili kumharibia mtu anayeonekana ni tishio kwa "master" wake.Si umeona anamuita "master" hapo?

Maandishi mengi halafu ni uongo tuu Ni propaganda tuu zilezile za Jason Bourne na Hutaki Unaacha.Miaka imebadilika.Watu wamebadilika.Wanachadema sio tena manyumbu ya kuamini kila "ubunifu" na propaganda za mweyekiti.

Muhimu ni kuwa hata wewe unajua watu wanataka mabadiliko.Unasema itazaliwa chadema mpya baada ya uchaguzi.Hakuna chadema mpya itakayokuja kama Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti.Chadema mpya na yenye nguvu zaidi ipo mikononi mwa Lissu.Chadema maslahi haiitajiki tena.Wakati umebadilika.Watu hawataki chadema yenye machawa waandika hekaya ili kulinda mkate wao wa kila siku

Watu wamechoka na mfumo wa siasa za makao makuu.Watu wanataka chama cha kitaifa ambacho nguvu yake ipo kila sehemu.Eti ili chama kionekane
kinafanya mkutano wa ushawishi Misungwi basi ni lazima Mbowe au watu kutoka makao makuu waende Misungwi.Kwanini watu wa Misungwi wao wasiwe na ushawishi kwa wanachadema wa Misungwi na kuwe
zeshwa kueneza chama hadi misungwi ndanindani huko bila watu kwenda kwa chopa kuleta nguvu?

Huo ni mfumo uliowekwa makusudi na Mbowe ili aendelee kusikika yeye na machawa wake wa makao makuu na kuonekana ni watetezi pekee wa wananchi.Na bado mtu kutoka Maduma huko ndanindani ambapo hata hiyo chadema anayojifanya anaipenda,hajaipeleka huko vijijini kwao,anakuja hapa kuandika propaganda dhidi ya mgombea uenyekiti ambaye ndiye chaguo la wanachadema wengi nchi nzima.Kisa ni wanalindwa na kulelewa na mfumo uliopo wa kiongozi anayekubalika na CCM!

Fikiria tu hili.Upinzani unapambana na chama tawala.Kuna wagombea wawili wa nafasi ya uenyekiti wa chama cha upinzani.Mmoja anaungwa mkono na wafuasi wengi wa upinzani na mwingine anaungwa mkono na chama tawala.Yani chama tawala kinamuunga mkono mmoja wa wagombea wa nafasi ya uwenyekiti wa chama cha upinzani,na bado kuna majuha wa upinzani wanaungana na chama tawala kumkaanga mtu asiyetakiwa na chama tawala!Inachekesha sana.

Watu mmeamua kutetea maslahi yenu bila aibu.Tutapambana nanyi mpaka mwisho tuwashinde nyinyi na wenzenu wa chama tawala kupiga chini kikundi cha chadema maslahi kwakuwa awamu hii kimejiweka wazi na tumekishtukia.
 
Maria Sarungi ni CCm na anatumika na mfumo.
 
Hujajibu swali langu, kama aliweza kutoa elimu akiwa makamu leo anashindwa nini kuendelea kutoa hiyo elimu akiwa kwenye nafasi yake hadi autake uenyekiti.
 
Hujajibu swali langu, kama aliweza kutoa elimu akiwa makamu leo anashindwa nini kuendelea kutoa hiyo elimu akiwa kwenye nafasi yake hadi autake uenyekiti.
Soma post no 221 utapata kitu
Usipoelewa bhas utakuwa na makamasi kichwani.
 
Ndio maana wanamitandao na wanaharakati wanahangaika sana kila siku wanaanzisha poll ili kuonyesha Lissu anakubalika, mwanzo nilitaka kuhadaika nilipoujua ukweli nikaachana nao.

Nimeshamwambia Lissu Maria Space haiwezi kumpatia kura.
Ni lazima mtu timamu ajiulize sana, nguvu kubwa sana inayotumika kumnadi Lissu inatoka ndani ya CHADEMA au nje ya CHADEMA?

Unaweza kuona kabisa CCM wamechanganyikiwa sana na huu uchaguzi wa CHADEMA, ni wazi kwamba kuna mgombea mmoja ni mtu wao, je ni nani? Tutamgundua vipi?
 
Aanzishe chama chake, kwani hiyo cdm kaanzisha Mbowe, au amekaa muda mrefu hadi unaamini ni chake?
MBOWE SIYO CHAKE ASILANI NI CHA WANACHADEMA NA WATANZANIA WENGINE. NI JUKUMU LA MBOWE KUHAKIKISHA CHMA HAKIFII KWENYE MIKONO YAKE. AFANYEJE? MPE USHAURI
 
Takataka tupu
 
Kama hakubaliani na aliowakuta kiustaarabu aanzishe chake, leo mimi nikihamia CCM siwezi kwenda na kuanza kuwapangia cha kufanya ndio hekima na busara inavyotaka.
Ana miaka 20 sasa kwenye hicho chama, ni wangapi hao aliowakuta? Halafu suala sio kumkuta mtu, bali ni kuwa na mawazo sahihi. Unasema leo ukienda ccm, ina maana umekosa mifano kabisa ukaona utolee mfano wa ccm? Daaa kazi ipo.
 
Mtu hata kama humewezi pambana naye, hata akikupiga atakuheshimu. Kwenda kujinyenyekeza ni kumfanya akuone bonge la poyoyo.
 
MBOWE SIYO CHAKE ASILANI NI CHA WANACHADEMA NA WATANZANIA WENGINE. NI JUKUMU LA MBOWE KUHAKIKISHA CHMA HAKIFII KWENYE MIKONO YAKE. AFANYEJE? MPE USHAURI
Akae pembeni maana kama chama ni cha wanacdm, basi wapo wengi wanaweza kuchukua nafasi yake bila chama kukwama.
 
Kwahiyo mwaka 2000 kulikuwa na uchaguzi mpaka ushangae mbunge mmoja?

Hata huyo mbunge mmoja waliachiwa Chadema kwa sababu ccm walimtosa Kessy.

Kura yako moja Kawe ndio ya kushangaa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…