Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Hii ID yako ya infantry soldier haiakisi uelewa wako wa masuala ya kivita.

Yaani kitendo tu cha wajerumani kuondoka na fuvu lake hakikushitui. Kwao ni MTU aliyewatesa mno katika mapambano ya msituni.

Eti mtu anayejiua ni dhaifu. Mbona Hitler alijiua kwa kujitumbukiza kwenye acid.

Hata Gaddafi kwa taarifa yako alitaka kujimaliza na bastola yake dhahabu kabla hajawahiwa. Katazame video ya mauaji ya Gaddafi.

Alafu Mkwawa hakujiua kwa sababu ya hofu pekee ila ni kanuni ya kivita unapozidiwa na hakutaka kuwakatisha tamaa wanajeshi wake kwa sababu ikiwa wangemuua yeye kama kiongozi ingekuwa rahisi kuwamaliza wengine.

Alaf unafananishaje mazingira ya kifo cha mkwawa na cha Gaddafi, ikiwa mkwawa alipambana na bunduki kwa mishale kwa asilimia kubwa na tena akipambana na mojawapo ya mataifa makubwa yenye jeshi kubwa na teknojia ya kisasa huku yeye akiwa hata sio taiga bali empire iliyo ndani ya taifa, huku akiwa na teknolojia duni.
 
Mkuu, kwenye comment yako moja hapo nyuma ulisema kwamba, askari/kiongozi hujiua ili kuweza kutunza siri. Sasa ina maana Gadaffi na Saddam walikuwa hawana siri za kutunza?
Suala la siri ni muhimu sana katika mikakati ya kijeshi bila kujali adui ni inferior kiasi gani,kwa mtu mwenye elimu /historia nzuri kuhusu Ngome ya Yesu (Fort Jesus) ya Mombasa anaweza akatuongoza, kumbuka Gaddaf zilitumika pesa zake mwenyewe alizoficha Ulaya kumuua mwenye mali ambazo zilikuwa ni nyingi mno,adui walihitaji lazima afe ili wale kwa ulaini pesa waliyomuibia,pia lazima nchi iwe na vurugu ili waibe mafuta kiulaini,Mtwa Mkwawa ni shujaa zaidi ya hao unaowasifu kwa sababu nyingi sana ila kwa kuwa watu weusi hatutafiti,hatusomi na hatuandiki historia zetu wala kuweka record,machifu wengi tu walipigana na wazungu na wakashinda lakini kwa wakati huo alikuwa anaandika mzungu,sijui kama angethubutu kusema sisi wazungu tulishindwa vita mara kumi.
 
Mkuu upo sawa lakini kwa upande mwingine ataona alistahili kuitwa shujaa! Mhehe huyo alipambana na wajerumani kwa muda wa miaka minane akitumia magobole na silaha za jadi huku jamaa wakiwa na silaha nzuri! Aliwahenyesha mpaka msituni, Kuna mengi sana aliyafanya katika kupambana na wakoloni hao! Lait kama ingewezekana kuyarecord na kuyaonyesha matukio ya mapambano yake ilikuwa ni kama Filamu moja inaitwa "The Hard Way"!
Babu yetu huyo alipambana sio mchezo aisee! Alilazimika kujiua sababu alijua kuwa alikuwa ameshawaumiza na ameshawasumbua sana hivyo mateso ya kikatili ambayo wangempa yangekuwa si ya kawaida!
 
Asante kwa ufafanuzi kuhusu wakinga na wabena
 
Kujiua ni uoga wa maisha mkuu na waoga kamwe hawatauona ufalme wa Mungu. Mzalendo hajiua hata siku moja.
Mkuu wewe ni muandishi wa hizi makala, na unajua kabisa Majasusi huwa wanakuwa na vidonge vya sumu midomo mwao ili wakikamatwa na kuteswa wajiue ili kulinda siri., unafikiri ni uoga huo??


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
kwani siku ya mshujaa wanakumbukwa walio hai au wale waliokufa
 
Hapa kwenye upande wa haki ninakuunga mkono kwa maana ukoloni uliacha madhila makubwa sana kwetu sisi waafrika kwa ujumla.
 
Naona udhaifu katika swali lako:
1. Mifano iko mingi ambako watu walijiua katika hali za mapigano wakiona hawawezi kushinda, wakiona umuhimu wa kutokamatwa, na bado wengi waliwatazama au wanawatazama kama mashujaa.

Mifano kadhaa inahusu watu wanaojua wanatunza siri fulani ambayo inapaswa kutunzwa - basi walijiua ili wasikamatwe na kulazimishwa kufichua siri (mbinu zilikuwa nyingi tangu kale, kuanzia mateso hadi ulevi na madawa..)

Mfano mashuhuri zaidi labda ni watetezi wa ngome ya Masada nchini Israeli miaka 1948 iliyopita. Katika vita ya Wayahudi dhidi ya Waroma mwaka 73/74 walizingirwa na jeshi la Waroma waliofaulu kuvunja ukuta. Katika usiku kabla ya shambulio la mwisho watetezi waliamua kujiua wote. Kuna taarifa juu ya hotuba ya kamanda Myahudi Eleasar ben Jaʾir aliyetaja sababu: Wake wetu waliopo watabakwa na kuuawa baadaye, watoto wetu watauzwa kama watumwa, na Waroma watapora mali yetu. Hivyo waliteua wanaume 10 waliopewa kazi ya kuchinja wengine, na hatimaye kujiua wenyewe. Kabla ya mauaji walichoma mali yao yote yenye thamani. Waroma waliposhambulia, walikuta maiti tu, na wanawake 2 pamoja na watoto 5, waliofaulu kujificha. - Hao watetezi wa Masada wanatazamiwa kama mashujaa katika Israel ya leo. Katika miaka ya 1956 - 1991 jeshi la Israel lilipeleka askari wapya wote huko kwenye maghofu ya Masada ili wale kiapo cha mwanajeshi kwenye mahali ambako hao watetezi wa zamani walikufa.
Kwa hiyo kujiua hakusemi kitu chochote kuhusu swali la shujaa.

2. Sababu yangu ya pili: huleti ufafanuzi je shujaa machoni pako ni nini au nani.
 
Mkuu, ninaona umeandika maelezo meeeengi na kujaribu kujitetea askari wanaojiua kwa kuogopa mapambano na kisha kujaribu kutumia mfano wa Wayahudi kama ndio justifications bora.

Askari anayejiua kwa kuogopa kupambana, awe muafrika, mwaarabu, mchina au mzungu, huyo kwangu mimi sio shujaa hata kidogo ukilinganisha na yule aliyekamatwa na kisha kuuwawa...
 
Mkuu, ni siri gani ambazo mhehe angeweza kuzificha mfumo wa taarifa wa taifa kubwa kama Ujerumani aliyetawala takribani 90% ya Ulaya nzima kabla ya WWII?...
Kwa mfano hupendi kutoa majina ya hao waliokusaidia?
Menginevyo tafadhali jipatie kitabu cha historia yenye ramani. Ujerumani haikutawala %90 za Ulaya kabla ya Vita Kuu ya Pili.
Tena Mkwawa alikufa miaka mingi kabla ya Vita Kuu ya Kwanza.
 
Yaani kitendo tu cha wajerumani kuondoka na fuvu lake hakikushitui. Kwao ni MTU aliyewatesa mno katika mapambano ya msituni.
Fuvu la Mkawa lilichukuliwa na Wajerumani kama TROPHY. Soma comment yangu #29...
 
Eti mtu anayejiua ni dhaifu. Mbona Hitler alijiua kwa kujitumbukiza kwenye acid.
Mpaka sasa bado dunia haijui Hitler alitowekaje duniani. Kuna wanaodai aidha USA au USSR kuna mmoja aliwahi kumkamata kisha akamficha...
 
Sina ya kujitetea hapa hata kidogo. Kaka tafadhali jaribu kusoma historia ya Mkwawa. Siku zake za mwisho alikuwa mgonjwa. Hakuweza kukimbia tena. Hakuwa na sababu kuogopa mapambano maana hakuwa na uwezo wa kupigana. Nahisi alichoka na hakutaka kukamatwa, katika hali yake uwzekano mkubwa wangemkamata hai. Katika gobori lake alikuwa na risasi 1 tu. Waliomfuata walikuwa kundi dogo.
Kama angekamatwa aliweza kuwaza wangemrudisha Iringa kama mfungwa na kumnyonga pale hadharani.
Na labda kumpiga hadi anatoa majina yote ya hao waliomsaidia katika miaka yake ya vita ya msituni.

Menginevyo, ukiona maelezo yangu kuhusu mfano wa watetezi wa Masada yalikuwa mengi - heri usiandike kuhusu historia. Maana kwa somo la historia unahitaji kusoma. Mengi! Sana!

Nimekupa mfano wa hao watetezi waliojiua na leo wanakumbukwa kama mashujaa wa kitaifa. Pinga tu, ukiweza kutaja sababu.
 
Alafu Mkwawa hakujiua kwa sababu ya hofu pekee ila ni kanuni ya kivita unapozidiwa na hakutaka kuwakatisha tamaa wanajeshi
Mbona Saddam Hussein hakujiua? Ina maana himaya ya wahehe ya miaka hiyo ya zamani ilikuwa na siri nzito kuzidi Iraq ya mwaka 2003?...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…