Uchaguzi 2020 Kulikuwa na ulazima gani kununua ndege za kibiashara kwa cash kuliko kununua matrekta na kuyagawa kila kijiji ili kulitupa jembe la mkono?

Ningeshangaa kama hii hoja ya watalii isingeibuka kwenye uzi huu, kabla ya hizo ndege hapakuwepo na mashirika mengine ya ndege yaliyoleta wageni hapa nchini? ama ndege hizi za ATCL zina kivutio cha ziada kitakachopelekea wageni wazipande kwa wingi kumiminika Tanzania?
Wewe ungekuwa sawa ungejua umuhimu wa kuingiza pato kupitia Atcl na watalii kwa pamoja.
 
Binafsi nimewahi kupanda ndege mara moja tu ukubwani na utotoni sidhani kama nimewahi kupanda. Nililipa 120k tu kwenda Mbeya na kurudi kwa Fast Jet 2015 kabla midege yetu haijapata sifa hizi.

Sasa hizi ndege zimeleta faida kwa kundi lipi kama tangu awali kabla ya ujio wa haya ma bombardier na Airbus za Magufuli huduma bora na rahisi zilikuwepo?

- Je, nauli zimeshuka kwa Watanzania?
-Je,pato linaloingia kupitia hizi ndege ni kubwa kuweza kuboresha sekta ya kilimo au afya?

*Tunaomba hesabu ya mapato na matumizi yatokanayo na hizi ndege.

Magufuli ungenunua trekta kila kijiji, na wananchi wangekuwa wanachangia fedha kidogo tu kwaajili ya Mafuta, repair na ujira wa operator wa tractor ungetukuzwa zaidi na wananchi. Umaskini ungepotea kabisa by reality hapa nchini na vijana wangerudi kijijini kulima.

Kuna mtu mmoja alisema ukijenga nyumba bila baraka ya watoto nyumba hiyo haitakuwa na baraka. Sasa naanza kumwelewa yule mtu .
Ushamba na ulimbukeni ni mzigo kwa taifa letu
 
ikiwa yesu pamoja na utukufu wake bado alipigwa vita na kudharauliwa magufuli ni nani asipigwe vita?

taifa kumiliki ndege linapata hadhi na thamani kubwa kimataifa bt nyie mazuzu mlozoea kupinga kila kitu lazima mpinge tu
 
Anapandisha bei za kupanda ndege bila kupandisha mishahara, hapohapo ananyanyasa wafanyabiashara kwa kodi lukuki, sijui alitegemea nani azipande hizo ndege mpaka zilete faida. Hakukuwa na ulazima wa kununua ndege nyingi kwa cash. Meko anatumia vibaya kodi zetu hapaswi kupewa tena kazi.
Ndege alinunua ili apande yeye na wanaccm wenzake.
 
Kiuchumi, unapokuwa na hela ambayo haitoshi mfano Nchi zote za ulimwengu wa tatu; kuna kitu kinaitwa Opportunity cost
Namaanisha ,ukinunua kitu kimoja lazima kingine kikose/kisubiri
Lakini pia, lazima tukubaliane kuwa Kila mtu anaweza kuwa na mawazo yake anayo amini yatachochea uchumi ila mwingine akafikiri tofauti na ndio sababu watu/viongozi kila mmoja ana wakati wake wa kuleta mabadiliko.
Nikupe mf: Kwa mtu akiajiriwa mara ya kwanza wakati hana kitu chochote na mshahara hautoshi; kuna ataona muhimu sana kwake ni Kitanda na Godoro, mwingine muhimu sana ni TV na mwingine muhimu sana Music system nk
Kimsingi hao wote wapo sahihi japo kila mtu anaweza kujadili kivyake......kilichotokea hapo ni opportunity cost
Namaanisha; hata hivyo vingine vitafanyika tena labda kwa uzuri zaidi kwani atakuwa amemaliza upande mmoja
SAMAHANI HAPO NIMEJADILI KIUCHUMI

"amemaliza upande mmoja
SAMAHANI HAPO NIMEJADILI KIUCHUMI"

Macro / micro ?
 
Binafsi nimewahi kupanda ndege mara moja tu ukubwani na utotoni sidhani kama nimewahi kupanda. Nililipa 120k tu kwenda Mbeya na kurudi kwa Fast Jet 2015 kabla midege yetu haijapata sifa hizi.

Sasa hizi ndege zimeleta faida kwa kundi lipi kama tangu awali kabla ya ujio wa haya ma bombardier na Airbus za Magufuli huduma bora na rahisi zilikuwepo?

- Je, nauli zimeshuka kwa Watanzania?
-Je,pato linaloingia kupitia hizi ndege ni kubwa kuweza kuboresha sekta ya kilimo au afya?

*Tunaomba hesabu ya mapato na matumizi yatokanayo na hizi ndege.

Magufuli ungenunua trekta kila kijiji, na wananchi wangekuwa wanachangia fedha kidogo tu kwaajili ya Mafuta, repair na ujira wa operator wa tractor ungetukuzwa zaidi na wananchi. Umaskini ungepotea kabisa by reality hapa nchini na vijana wangerudi kijijini kulima.

Kuna mtu mmoja alisema ukijenga nyumba bila baraka ya watoto nyumba hiyo haitakuwa na baraka. Sasa naanza kumwelewa yule mtu .
Nakupongeza kwa mada hii.
 
Eti kila Kijiji kipewe trekta akili Huna Kuna vijiji Ni wafugaji sio wakulima na Kuna vijiji hawalimi hulima mazao ya kudumu Kama mikorosho ,Chai ,kahawa nk

Kuna vijiji viko maeneo ya milima yenye
Kuna vijiji Ni vya wavuvi hayo matrekta watalima kwenye maji? Chadema hamna akili

Eti kila Kijiji!!!!
Hakuna kiji kisicho na wakulima, vinginevyo utuambie wanaishi kwa nyama au samski tu na kwamba hawaishi kwa nafaka na mboga.
 
Wakishalima watasafilishaje mazao yao?
Au mnataka walime kisha viozee ndani na wapate hasara kisha mseme hapakuwa na mikakati?
Serikali kwa awamu zote wamejitahidi upande wa barabara, ni wakati muafaka kabisa kuwekeza kwenye kilimo kwa dhati kabisa. Takribani robo tatu ya wananchi wanategemea kilimo na ukiwekeza hapo utabadilisha uchumi wa wengi.
 
Binafsi nimewahi kupanda ndege mara moja tu ukubwani na utotoni sidhani kama nimewahi kupanda. Nililipa 120k tu kwenda Mbeya na kurudi kwa Fast Jet 2015 kabla midege yetu haijapata sifa hizi.

Sasa hizi ndege zimeleta faida kwa kundi lipi kama tangu awali kabla ya ujio wa haya ma bombardier na Airbus za Magufuli huduma bora na rahisi zilikuwepo?

- Je, nauli zimeshuka kwa Watanzania?
-Je,pato linaloingia kupitia hizi ndege ni kubwa kuweza kuboresha sekta ya kilimo au afya?

*Tunaomba hesabu ya mapato na matumizi yatokanayo na hizi ndege.

Magufuli ungenunua trekta kila kijiji, na wananchi wangekuwa wanachangia fedha kidogo tu kwaajili ya Mafuta, repair na ujira wa operator wa tractor ungetukuzwa zaidi na wananchi. Umaskini ungepotea kabisa by reality hapa nchini na vijana wangerudi kijijini kulima.

Kuna mtu mmoja alisema ukijenga nyumba bila baraka ya watoto nyumba hiyo haitakuwa na baraka. Sasa naanza kumwelewa yule mtu .
Mkinipa kura tuu.. Naongeza nyingine tano
 
Kwel ujinga na ushamba ni mzigo mzto
Eti kila Kijiji kipewe trekta akili Huna Kuna vijiji Ni wafugaji sio wakulima na Kuna vijiji hawalimi hulima mazao ya kudumu Kama mikorosho ,Chai ,kahawa nk

Kuna vijiji viko maeneo ya milima yenye
Kuna vijiji Ni vya wavuvi hayo matrekta watalima kwenye maji? Chadema hamna akili

Eti kila Kijiji!!!!
 
Kijiji gani kina heka zisizozidi 10?
Tuanzie hapa kwanza
Wewe unaongelea tractor la kijiji??? Ardhi ni ya wana vijiji, yaani kwa kiswahili chepesi ni ya individuals na ardhi zao zipo scattered, hapa una eka 2, pale eka 4 na kuendelea,
Sasa economically sio efficient kuwa na patches of land ya kupima here and there , ndio maana nakwambia ni juu yangu Mimi na wewe tujiunge kwa njia moja au nyingine tulime kwa pamoja tractor likija linapiga eka 10 na zaidi.

Sasa vikundi vidogo vidogo ni rahisi ku manage.

Tatizo la tractor la kijiji watu wasio kuwa na uchungu nalo ni shida kuli manage ktk matumizi ya kila siku na ktk repair.

Kama hulijui hilo utakuwa unaishi sayari nyingine.

Hata china wameisha toka huko unakofikiria wewe.
 
Serikali kwa awamu zote wamejitahidi upande wa barabara, ni wakati muafaka kabisa kuwekeza kwenye kilimo kwa dhati kabisa. Takribani robo tatu ya wananchi wanategemea kilimo na ukiwekeza hapo utabadilisha uchumi wa wengi.
Tatizo nyie mko mjini mnaona mabarabara mnadhani yamefika vijijini, kuna shemu ya km 50 bado watu wanasafili kwa tsh 8000 kitu ambacho wangelipa kwenye rami 3000, hivo huyo mtu anaumia na gharama
Sasa kusafirisha mazao bei itakuwa kiasi gani?.
 
Mkuu huko sahihi kabisa, lakini uwekezaji kwenye miundombinu ya kilimo haukwepeki na hakuna kisingizio chochote kitakachokubalika kuhalalisha jambo hilo. Awamu hii kuna mambo tumeyafanya ambayo hayakuwa na umuhimu wowote huku tukitelekeza sekta ya kilimo. Hili jambo halihitaji kusubiri hizo barabara, hayo mambo yanaweza fanywa kwa pamoja kidogo kidogo
 
Wazo zuri
i wish miaka 5 ijayo viongozi waboreshe upatikanaji wa hizi zana ili wanakijiji waache kulima na mkono.,

Zipatikane japo kwa kukodisha kwa bei ndogo ama free kwa zamu na utaratibu fulani utakaowekwa
 
Wakishalima watasafilishaje mazao yao?
Au mnataka walime kisha viozee ndani na wapate hasara kisha mseme hapakuwa na mikakati?
Nmekuelewa vzuri sana tatizo sio matrekta Wala nn, tatzo ni masoko tu yanahitajika. Watu wanalima sana na mazao yao wanayauza bei rahisi mno na mengine kuoza kbs kabla ya kuyauza. Matrekta mengi tu huko vijijini hekari moja anakulimia kwa elfu arobain tu. Watafuteni masoko uone watu watakavyoipasua hii ardhi ya Tanzania
 
Wewe unaongelea tractor la kijiji??? Ardhi ni ya wana vijiji, yaani kwa kiswahili chepesi ni ya individuals na ardhi zao zipo scattered, hapa una eka 2, pale eka 4 na kuendelea,
Sasa economically sio efficient kuwa na patches of land ya kupima here and there , ndio maana nakwambia ni juu yangu Mimi na wewe tujiunge kwa njia moja au nyingine tulime kwa pamoja tractor likija linapiga eka 10 na zaidi.

Sasa vikundi vidogo vidogo ni rahisi ku manage.

Tatizo la tractor la kijiji watu wasio kuwa na uchungu nalo ni shida kuli manage ktk matumizi ya kila siku na ktk repair.

Kama hulijui hilo utakuwa unaishi sayari nyingine.

Hata china wameisha toka huko unakofikiria wewe.
Wewe unawaza kua Trekta la Kijiji basi kila mtu ana amri nalo, sivyo hivyo, ondoka kwenye mawazo hayo.

Trekta anakabidhiwa mtu atakaekua "Custodian", atakaewajibika kwa lolote. Ardhi ni ya wanakijiji lakin wengine hawalimi sababu gharama za kulima ni kubwa. Likiwepo hilo trekta ambalo wanakijiji watagharamia Gharama Pekee za kuliendesha basi Wengi watashawishika kulima
 
Back
Top Bottom