Habari za muda huu ndugu zangu wa jamiiforums.
Eti wataalam wa mipango miji, kulikuwa na umuhimu gani kwa kiwanja cha soccer cha Uhuru pamoja na ule wa Benjamin William Mkapa kujengwa sehemu moja?
View attachment 2419759
Eneo ulipojengwa uwanja wa Mkapa lilikuwa eneo la wazi na ndio sehemu ambayo chuo cha ufundi stadi cha VETA kilikuwa kinatumia katika kufunza madereva wachanga.
Nilisoma shule ya msingi Kibasila mwaka 1999 hivyo ninapajua sana eneo lile. Kabla ya ule uwanja wa Mkapa kujengwa kulikuwa na geti dogo la kuingilia shule ya secondary ya JKT Jitegemee (Jiteute) miaka hiyo pamoja na mnara wa ndege vita ya jeshi iliyoanguka wakati wa kuwapokea rasmi mashujaa wa vita ya Kagera. Hivyo lile eneo ninalijua vema tu.
Kwanini uwanja wa Mkapa haukupelekwa Boko au Bunju kama walivyofanya hospitali ya Muhimbili kujenga branch Mloganzila na ukizingatia kipindi kile maeneo ya njia ya Bagamoyo hayakuwa expensive kama ilivyo sasa?
MSAADA: Kwa wataalama wa mipango miji kulikuwa na umuhimu wowote wa kuwa na viwanja viwili vya soka eneo moja?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.