Mkuu wala liberal approach haihitajiki kwani kifungu kipo wazi kabisa kuwa kukaa mita mia mbili toka sehemu ya kupigia kura sio kosa. Ila haisemi mkiwa hapo muwe kwa ajili ya kulinda kura. Kwa hiyo watu wakae mita hizo mia mbili ila polisi wakija wasiseme tupo hapa tunalinda kura hata kama mioyoni mwao lengo ni kulinda kura.
Usichokijua ni kuwa sheria ya Uchaguzi inasema siku ya kupiga kura hakutakuwa na mikusanyiko ya kisiasa.Mikusanyiko yote ya kisiasa mwisho wake ni siku ya mwisho wa kampeni ambayo ni tarehe 24 octoba 2015.Ukikusanya watu wako siku hiyo ya uchaguzi wawe wana UKAWA au CCM wakajikusanya mahali ni kosa kisheria.
Pili kwa mujibu wa sheria zinazohusu mikusanyiko ni lazima kutoa taarifa polisi kuwa kutakuwa na mkusanyiko mahali fulani na kwa lengo gani. Hivyo kama kurtakuwa na watu wenye lengo la kukusanyika popote inabidi wawasilishe maombi yao polisi wakijieleza wao ni akina nani ili wapewe ulinzi wa polisi
Tatu kuna sheria ya ardhi.Unaposema utakusanyika hapo kwenye mita 200 hilo eneo ni mali ya baba yako au mama yako? Huyo mwenye miliki ya hiyo ardhi karidhia? Hivyo kama kuna watu watakaotaka kukusanyika ni lazima wapeleke kibali cha mwenye eneo kuwa karidhia eneo lake litumike kwa mikusanyiko.Na kwamba mikusanyiko hiyo haitakuwa kero wala bugudha kwa wakazi wa eneo husika,majirani n.k Maana kama watu watajiamulia kukusanyika hiyo mita mia 200 bila mwenye eneo lake kuridhia ina maana ni uvamizi wa ardhi ya mtu bila ridhaa yake.Na huo ni uvunjifu wa amani kwenye eneo la watu.Hivyo Mahakama lazima iangalie maslahi ya wenye maeneo maeneo yao yasije vamiwa SIKU YA KUPIGA KURA NA KUKALIWA KWA MABAVU na hao wanaojiita walinda kura.
Polisi kwa kuliona hilo kuwa kutakuwa na uvunjaji sheria kwa watu kuvamia maeneo ya watu na kujikusanya wakasema kila mtu aende kwake asubirie kwake.Sababu vituo vya kupigia kura haviko mbali na makazi ya watu.Kwa nini watu wakae kwenye viwanja vya watu? Mahakama iliangalie hilo
Kwangu sikubali mtu akusanyike WALA KUWEKA MAKALIO YAKE KWENYE ENEO LANGU NITAITA DEFENDER NA GARTI LA WASHA WASHA HARAKA WAJE NA MABOMU NA VIRUNGU WAONDOE WAVAMIZI KWENYE ENEO LANGU.
Hawa akina KIBATALA wanataka kuleta vurugu na ugomvi kati ya wenye maeneo na hao watu anaotaka wakusanyike hizo mita mia mbili sababu sio kwao ni kwa watu.
Eti bila haya lowasa na mbowe wanatoa amri mkimaliza kura kaeni mita 200.Hilo eneo wanaloamrisha watu wakae ni la baba yake au mama yake lowasa au mbowe.Sheria ya ardhi iheshimiwe majaji msimamie hilo kwa maslahi ya wenye maeneo yao.Mkiwakubalia mnawaweka wenye maeneo matatizoni.